Halima Mdee na wenzake Washinda kesi dhidi ya CHADEMA. Waendelea kuwa wanachama wa CHADEMA. Kuendelea na Ubunge wao

Halima Mdee na wenzake Washinda kesi dhidi ya CHADEMA. Waendelea kuwa wanachama wa CHADEMA. Kuendelea na Ubunge wao

Haya hapa ni baadhi ya Maelezo ya Jaji .

View attachment 2842497
Kama tulivyotarajia , Jaji ameamua hivi .

View attachment 2842542

====

Mahakama kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es salaam imewapa ushindi Halima Mdee na wenzake 18 kwenye kesi yao waliyoiwasilisha Mahakamani hapo dhidi ya Uamuzi wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA wa kuwafukuza uanachama Wabunge 19 wakituhumiwa kwenda Dodoma kuapishwa bila idhini ya Chama.

Akisoma Hukumu hiyo Jaji Cyprian Mkeha amesema kitendo cha wajumbe wa Kamati Kuu iliyowafukuza kuwa tena wajumbe wa Baraza kuu ambalo lilisikiliza rufaa yao kinaondoa uhalali wa maamuzi ya Baraza Kuu "Baraza Kuu lilikwenda kinyume na kanuni ya kawaida ya kutokupendelea
Sherehe kubwa ufipa leo, Mbowe ana uhakika na ruzuku toka covid 19. Hongereni kwa kushinda kesi. Peopleeeeeeeeeees.
 
Kwa hukumu hii niseme tu uchaguzi wa ndani ya chama unakwenda kuvurugwa kuanzia mwenyekiti wa chama hadi mashinani tutapandikiziwa viongozi ambao hata fomu hawatochukua na haraka haraka msajili atatangaza kuwatumbua.

Nilionya kule BAWACHA wachague mwenyekiti wamezubaa sasa mdee karejea, sasa akirudi ofisini jumatatu kudai kiti chake mtafanyeje na kipo wazi?

Mbowe kwa hili hapana umeshindwa kuwa aggressive enough, wameshajua tukiporwa hatuna cha kufanya. Ilipaswa walau mmoja atekwe abinywe mpaka ataje wenzake na waliowatuma tungesolve haya maigizo ila kuendelea kucheka cheka hivi tusishangae Mdee akawa mgombea Urais 2025 bila kuchaguliwa na chama.

This is nonsense
Huyo Mbowe hamna kitu hapo boss. Ni muda sana Mbowe ameshaflop. Na kwa taarifa yako uwepo wa hao COVID huko bungeni una mkono wa Mbowe kwa namna moja au nyingine.
 
Mimi naona yawepo makubaliano ya hao cov 19 na Uongozi wa CDM! Waachwe waendelee na ubunge kwa kuwa muda uliobaki ni mfupi kabla ya uchaguzi mwingine 2025!
Makubaliano gani tena? Mbowe hawezi kukubali kukosa ruzuku hata 2025 watapewa tena viti maalum haohao covid 19.
 
Haya hapa ni baadhi ya Maelezo ya Jaji .

View attachment 2842497
Kama tulivyotarajia , Jaji ameamua hivi .

View attachment 2842542

====

Mahakama kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es salaam imewapa ushindi Halima Mdee na wenzake 18 kwenye kesi yao waliyoiwasilisha Mahakamani hapo dhidi ya Uamuzi wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA wa kuwafukuza uanachama Wabunge 19 wakituhumiwa kwenda Dodoma kuapishwa bila idhini ya Chama.

Akisoma Hukumu hiyo Jaji Cyprian Mkeha amesema kitendo cha wajumbe wa Kamati Kuu iliyowafukuza kuwa tena wajumbe wa Baraza kuu ambalo lilisikiliza rufaa yao kinaondoa uhalali wa maamuzi ya Baraza Kuu "Baraza Kuu lilikwenda kinyume na kanuni ya kawaida ya kutokupendelea
Acha upotoshaji, pitia maamuzi yote siyo kurukia vipande.
Amesemaje juu ya maamuzi ya Kamati kuu kuwafukuza?
Hata hilo la halmashauri kuu huo ni uhuni wa mahakama za mchongo
Katiba ya Chadema ina watambua wajumbe wa kamati kuu kuwa wajumbe wa halmashauri kuu.
Ila jigoo akiwika au asiwike juta kucha tuu.
Majaji wa bongo wamekuwa wasoma hukumu sio watoa haki.
 
Na bado kuna wanaotaka kwenda uchaguzi bIla katiba Mpya.

Kwa mahakama zipi za kukimbilia kukichezwa rafu na wenye vifua vyao kama ilivyozoeleka?
Ipo siku mtapata viongozi wakubwa ambao hamkuwachagua ninyi kwa mbinu hizi hizi.

Mtachaguliwa viongozi na msajili au mahakama.
 
Sio kwa hapa Tanzania, ndio maana wazungu hawako tayari mashauri Yao kusikilizwa kwenye hizi mahakama za ndani, maana wanajua ni uchafu mtupu.
Kitendo cha wajumbe wa Kamati Kuu iliyowafukuza kuwa tena wajumbe wa Baraza kuu ambalo lilisikiliza rufaa yao kinaondoa uhalali wa maamuzi ya Baraza Kuu. "Baraza Kuu lilikwenda kinyume na kanuni ya kawaida ya kutokupendelea"
 
Huwa nakipenda sana kigabu cha Mario Puzzo cha "The Godfather!"

"Kwanini ulikwenda kwao?" Jamaa anajibu "kulingana na niliyoifanyia marekani nilijua itanitendea haki"

"Sasa kwanini umekuja kwangu?" Don corleon akauliza... jamaa akajibu " Nimekuja kwako kwakua marekani imenisaliti...nilijitolea fursa zangu, nguvu na uhai wangu kuitumikia marekani lakini leo hii imenisaliti? Nimekuja kwako Don Corleone the Godfather nisaidie nipate haki ya binti yangu"

Hii ilitokea baada ya mzee mmoja binti yake kubakwa na kuumizwa vibaya sana cha ajabu wabakaji walifungwa siku tatu tu na mahakama tena baada ya vuta nkuvute nyingi sana!

Don Corleon alimsaidia kuwaua wabakaji wote wa mwanae.

Hakuna haki mahakamani hasa hizi kangaroo courts za Afrika ni ushwaini mtupu!
Kitendo cha wajumbe wa Kamati Kuu iliyowafukuza kuwa tena wajumbe wa Baraza kuu ambalo lilisikiliza rufaa yao kinaondoa uhalali wa maamuzi ya Baraza Kuu. "Baraza Kuu lilikwenda kinyume na kanuni ya kawaida ya kutokupendelea
 
..kwa hukumu hii mbona hakutakuwa na chama hapa Tz kinachoweza kufukuza mwanachama wake?
hapana hapa mahakama imeweka msingi mzuri wa Vyombo vinavyotoa hukumu kwa ndani ya vyama, kuwa impartial. Jambo ambalo halipo kwa miundo ya utoaji haki kwa vyama vyote vya siasa hapa kwetu. So i think ni maboresho ya utoaji haki na si uzuiaji wa adhabu kwa wanachama.
 
Sasa wanatoka kuwa COVID 19 Hadi Changamoto za upumuaji!!
 
Huyo Mbowe hamna kitu hapo boss. Ni muda sana Mbowe ameshaflop. Na kwa taarifa yako uwepo wa hao COVID huko bungeni una mkono wa Mbowe kwa namna moja au nyingine.
Mbowe bado hajaandaa mrithi wake kwa sasa.
 
Kitendo cha wajumbe wa Kamati Kuu iliyowafukuza kuwa tena wajumbe wa Baraza kuu ambalo lilisikiliza rufaa yao kinaondoa uhalali wa maamuzi ya Baraza Kuu. "Baraza Kuu lilikwenda kinyume na kanuni ya kawaida ya kutokupendelea"
Kwamba hiki kifungu ndio kinaonyesha mahakama zetu ni huru?
 
Back
Top Bottom