Kamati Kuu Chadema ina mamlaka kuwafuta uanachama wabunge, lakini katika kulifanya hili, taratibu kwa mujibu wa katiba ya Chadema, hazikufuatwa.
Kamati Kuu Chadema, sio mamlaka ya nidhamu ya Halima Mdee, ilipata wapi mamlaka kumtimua?.
P
Mkuu Joka.. ili Mbunge wa viti maalumu aapishwe lazima bunge lipatiwe barua na Nec kuwa ameteuliwa kuwa mbunge wa viti maalumu.
Sasa je, walijipeleka Bungeni bila hata nyaraka? NEC hawana nyaraka kwenye mafaili yao ?
Halima Mdee ni Mwenyekiti wa Bawacha alitechaguliwa na Mkutano Mkuu, moja ya majukumu makubwa ya Bawacha ni kuwajengea uwezo Wanawake wa Chadema kuingia kwenye vyombo vya uwakilishi...Pasco unazidi kupotosha.
..Halima hakuadhibiwa kama Mwenyekiti wa Bawacha, au Mjumbe wa Kamati Kuu.
..Alipojipeleka bungeni hakufanya hivyo kama sehemu ya majukumu yake kama Mwenyekiti wa Bawacha.
..Halima aliadhibiwa na Kamati Kuu kama mwanachama wa kawaida aliyejipeleka bungeni bila ridhaa ya chama.
Mimi ni muelimishaji umma, na elimu yangu pia daasa saba. Isiite watu mijitu!.Unahangaika na mijitu iliyopata F darasa la saba.
Halima Mdee ni Mwenyekiti wa Bawacha alitechaguliwa na Mkutano Mkuu, moja ya majukumu makubwa ya Bawacha ni kuwajengea uwezo Wanawake wa Chadema kuingia kwenye vyombo vya uwakilishi.
Baada ya Chadema kupewa nafasi 19 za viti maalum, Chadema kama chama kilizikataa, now take it from me once and for all kuwa hao wabunge 19 hawakujiibukia tuu Bungeni kwa kuchipukia kama uyoga, consultations, lobbying and advocacy ilifanyika, waka seek authorization form wenye chama na wakapewa a go ahead kuwa they are doing that on their own risks.
Yote yalifanyika Mdee kayafanya kama Mwenyekiti wa Bawacha. Mtu akiishachaguliwa kuwa kiongozi, huwezi kumtuhumu chochote as mwanachama wa kawaida.
Baada ya Dr. Slaa kutofautiana na Mwenyekiti wake kwenye issue ya kumpokea Lowassa, Dr. angeweza kujenga hoja kuwa Chadema kama chama hakikumtuma Mbowe amlete kubwa la mafisadi kuwa mgombea wao!. Jee wangeweza kumfukuza Mbowe as mwanachama wa kawaida?.
CC ya Chadema sio mamlaka ya nidhamu ya NKM, lakini walimtinua Zitto Kikangroo kama sasa CC ya Chadema sio mamlaka ya nidhamu ya Mwenyekiti wa Bawacha, haina uwezo huo!. Kilichofanyika ni Ukangaroo tuu, na haya yanafanyika kwasababu Chadema wamezoea vya kunyonga "Mzoea vya kunyonga vya kuchinja Haviwezi". Hongera Halima Mdee na Makamanda wote kwa kugomea wito wa kienyejienyeji
P
Uziri wa JamiiForums kila ujinga unapatiwa tiba stahiki… safi.Acha kupotosha mkuu ni lini majina yanapelekwa kabla ya uchaguzi wakati siku zote viti maalum vinakuwa confirmed na Kamati kuu baada ya matokeo kuonyesha taswira ya political landscape?
Sasa whether walipewa barua ya uteuzi na Mbowe or Mwalimu katiba ya chama inakubali hiyo process?? Je taratibu za NEC zinakubali barua iandikwe na yeyote tu bila vikao vya maamuzi??
Of course katiba na miongozo ya CHADEMA haikubali Hilo so mpaka hapo kichama hawakuteua wabunge. Sasa kilichopo waliamua kufanya maamuzi ya kuwavua uanachama (Sio kuwavua ubunge) na sababu kuu ni wao kugoma kuja kuhojiwa na Kamati kuu juu ya yaliyotokea hivyo Ile dharau ndio ilipelekea wafukuzwe na sio kwenda bungeni!!!
Sasa basi, whether walifoji or whether Mbowe aliwatuma bungeni, je wao kufukuzwa kwa kutoitikia wito wa Kamati kuu na kwenda na kinyume na msimamo wa chama unahusiana nini na uhalali wao kuteuliwa???
Hapa kilichopo ni maamuzi ya baraza kuu yaheshimiwe so whether Mbowe or wateva kawapa barua haituhusu wanachama.
Mkuu JokaKuu, mwanachama wa kawaida, akiishakuwa kiongozi wa kuchaguliwa, huo uongozi is infused with h/er/I'm, you can't separate the two. Viongozi wa kuteuliwa ndio wanaweza kutenguliwa kiongozi wa kuchaguliwa hawezi kutenguliwa uanachama kabla ya kutenguliwa uongozi...angekuwa amefanya hayo kwa kutumwa na chama na akapeleka mrejesho kamati kuu sawa.
..lakini aliyoyafanya yalikuwa nje ya utaratibu na sio kwa mujibu wa majukumu yake ya mwenyekiti wa Bawacha.
natamani hii kesi isikilizwe tujue mbivu na mbichiMnajipa moyo kama watoto. Mnataka kusema akina Halima walifoji barua ya kujiteua?
🤓🤓🤓
👇
View attachment 2273831