KERO Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama tumelipwa 250,000 tu ya fedha za kujikimu

KERO Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama tumelipwa 250,000 tu ya fedha za kujikimu

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Sisi ni walimu tulioajiriwa Januari 2026 katika Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama. Baada ya kudai fedha za kujikimu kwa muda mrefu, mwezi Agosti tuliingiziwa TSh 250,000/= bila maelezo yoyote rasmi. Tangu hapo, viongozi wamekaa kimya hadi leo.

Tunaomba TAMISEMI na mamlaka husika zitusaidie kutusemea na kufuatilia suala hili. Je, TSh 250,000/= ndiyo stahiki yetu yote, au bado kuna salio? Kwa nini hakuna maelezo rasmi?

Tumechoka na ukimya huu! Tunaomba uwazi, uwajibikaji na haki itendeke. Hili linaibua maswali mazito kuhusu usimamizi wa stahiki za watumishi wapya.

TUSAIDIENI KUPAZA SAUTI YETU!
 
Siasa za halmashauri na malipo ya fedha kwa kazi maalum au kujikimu kwa watumishi wa umma!ni siasa Kali sana zenye maumivu ya kutosha kwa watumishi,subra,unyenyekevu,utulivu vinaweza kukuokoa na kihoro
 
Ww ni maskini huna haki kaa utulie na ufanye kaz na kama utaki kazi kuna maskini kibao kama ww wanataka iyo kazi


Kwanza nyie bajia ndo huwa mnatumika kuiba kura sa sjui uwa mnatanguliza umaskin wenu kwa vipesa vidogo nmasahau kuna maisha baada ya uchaguzi sasa maisha yenyewe ndo hayo sasa
 
Back
Top Bottom