Hamas wavalia kombati mpya za kijeshi kukabidhi mateka. Kila mmoja kapewa begi na shahada

Hamas wavalia kombati mpya za kijeshi kukabidhi mateka. Kila mmoja kapewa begi na shahada

Inanifikirisha sana, ukizingatia Gaza pia ni kaeneo kadogo unaweza kwenda ukarudi mara kadhaa Gaza yooote, mbaya zaidi jamaa wanasema walifukua mahandaki yote.

Nina uhakika pia jamaa waliziba border zote na kucontrol movements, lakini bado walishindwa kuwapata mateka ndani ya Gaza lingine tunawaona Hamas hapo hapo Gaza tena.
Mbaya zaidi, kuna hatari Hamas wakapata wanachama wapya wenye hasira zaidi na Israeli maana wengi wameuliwa ndugu zao wasio na hatia wala uhusiano na Hamas.

Hii vita inahitaji akili zaidi kuimaliza kuliko manguvu na kuua watu hovyohovyo, mauaji yanaendeleza chuki ya vizazi na vizazi.
Mkuu umewahi kujiuliza ni kwanini Israel ilijua walipo viongozi wote wa Hamasi na ikawafyekelea mbali lakini ikashindwa kabisa kujua walipo mateka ndani ya Gaza hiyo hiyo?
 
Ni mtu mjinga ambaye ataamini Israel haikujua Mateka walipo.
Yaani iwaue viongozi karibu wote wa hamas, ijue walipo alafu wasijue mateka walipo
Shida ni kuwaokoa wakiwa hai sio kujua walipo, unaweza kujua walipo Hamas wakijiridhisha uko karibu wanatandika risasi mateka mnakosa wote
 
Acha udini wewe yaani gaza iliyoalibiwa hivyo unadai Israel imeshindwa! Duhh haya ni maajabu, kama unaamini hayo magaidi yajaribu tena kuipiga Israel.
Udini upo wapi mkuu? unajua mimi dini gani?
Nachojaribu kusema ni Israel walikuwa na lengo kuimaliza Hamas lakin wameingia makubaliano wakati Hamas bado ipo
 
Picha za wapiganaji wa Hamas wakati wa makabidhiano ya mateka zimetajwa kuwa ni ushahidi kuwa vita vya zaidi ya mwaka mmoja havikuwamaliza wapiganaji hao.

Wakati huo huo video hizo zimewaudhi mno wahafidhina wa kiisrael akiwemo Ben Giver aliyewahi kupendekeza kutumika bomu la nyuklia kupambana na Hamas. Waziri huyo na mshirika muhimu wa Netanyahu kwa hasira aliamua kujiuzulu nafafsi yake.

Mateka hao watatu kila mmoja alikabidhiwa kigegi kidogo kilichokuwa na picha,mkufu pamoja na shahada ya kuwachwa huru iliyoandikwa kwa lugha ya kiarabu na kihibru.Mmoja kati ya mateka hao alililamika kupokonywa zawadi yake hiyo kulikofanywa na kikosi cha Shinbet.

Makabidhiano hayo ya mateka ambao walipitishiwa kwa shirika la Red Cross yamefanyika katikati ya mji wa Gaza kaskazini ambao kutokana na unyama uliofanyika wa kutumia silaha nzito na kuzuia chakula na maji kwa takriban miezi miwili ya karibuni haikutarajiwa kabisa kwamba kungebaki watu walio hai hasa miongoni mwa Hamas.
View attachment 3207834
Netanyahu ndio akajakushtuka mwishoni kuwa Hamas uwezi kuitoa GAZA galama ya kuitoa kubwa sana ikiitaji pesa na uhai wawatu upotee kwawingi kaona isiwe janga kubwa zaid karusha taulo!!!
 
Kina nani hao?
Mbona viongozi wote waliokuwepo na waliwekwa kwa muda waliuwawa?

Kwa mfano, kwa sasa ni nani kiongozi wa Hamas
Ukitaka kujua kuna kiongozi soma mazingila tu siunaona kilakitu kinaenda km ilivotalajiwa mateka Nk basi jua viongoz wapo ndio wanaosimamia iyo show!!!!
 
Shida ni kuwaokoa wakiwa hai sio kujua walipo, unaweza kujua walipo Hamas wakijiridhisha uko karibu wanatandika risasi mateka mnakosa wote
Na hicho ndio kilifanya IDF ijifanye haijui walipo
 
Mkuu umewahi kujiuliza ni kwanini Israel ilijua walipo viongozi wote wa Hamasi na ikawafyekelea mbali lakini ikashindwa kabisa kujua walipo mateka ndani ya Gaza hiyo hiyo?

Kama unamajibu ni vyema ukashare nasisi, binafsi najiuliza hilo swali pia.
 
Ukitaka kujua kuna kiongozi soma mazingila tu siunaona kilakitu kinaenda km ilivotalajiwa mateka Nk basi jua viongoz wapo ndio wanaosimamia iyo show!!!!
Muhammed Sinwar ndio kiongozi wa combat kwa sasa, ni mdogo wa Yahya huenda akarithi mikoba. Anakubalika sana na Israel hawamjui sana kama ilivyokua kwa brother ake ambae walikaa nae jela kwa miaka mingi
 
Mossad wameshindwa kujua mateka wako wapi hadi CEASEFIRE DEAL ilipotokea? Shame on you MOSSAD,ISRAEL AND NETANYAHAU.

Dunia tunashukuru tu wameacha kuuwana kama kuku, for the good sake of women and children and the world's peace is restored although najua haijaisha hii but let take pose for now until next time if GOD wishes.
 
Back
Top Bottom