Wanasema kwamba kama hujabatizwa huwezi kuielewa biblia kwani wanasema ikisemwa upanga wewe utajua kua ni upanga hivyo hivyo.
Pia wanasema ikisemwa msichana wewe utajua ni msichana hivyo hivyo kwa sababu kama hujabatizwa hujafunuliwa ili uweze kufahamu parables za kwenye biblia ambazo Yesu alizitumia sana.
Ubatizo:
Hii ni ibada kuu na ya msingi katika dini ya Kikristo ambayo hata watoto wachanga nao huusishwa nayo pia!
Kwa ujumla wake, ibada hii (ya ubatizo) imeshamiri sana katika Ukristo.
Hata hivyo, pamoja na kuwemo katika orodha ya ibada za Kikristo, lakini kwa mujibu wa maelezo ya Biblia tukufu, asili ya ibada hiyo (ya ubatizo) imetokana na dini ya kipagani (Mithraism).
Uthibitisho wa hayo tunaupata katika maelezo ya Biblia yafuatayo:
"Ibada ya (ubatizo) kutosa mwili majini ni mfano wa utakaso au wakujitengeneza upya.
Ibada kama hiyo ilijulikana na kutendeka katika dini za kale za kipagani na dini ya Kiyahudi pia (kama ubatizo wa waongofu Mdo 2:10; Waesseni)'.
(Tazama Biblia ya Wakatoliki, Imprimatur M. Mihayo Archbishop of Tabora, February, 1967, kwenye maelezo ya Mathayo 3:6 uk. 879).
Maelezo hayo ya Biblia hapo juu yanathibitisha wazi kwamba ibada hiyo ya ubatizo inatokana na dini za kale za kipagani na kamwe haitokani na dini ya Yehovah.
Nasema ibada hiyo (ya ubatizo ya kipagani) katu haitokani na Yehovah, kwa sababu tangu mapema Yehovah alikwisha wakataza na kuwaonya wanadamu kutenda ibada yoyote (kama hiyo ya ubatizo) ya watu wa mataifa (yaani wapagani) kama asemavyo (Yehovah) katika maandiko yafuatayo:
"
Utakapokwisha kuingia katika nchi akupayo BWANA, Mungu wako, usijifunze kutenda kwa mfano wa machukizo ya mataifa yale".
(Kumbukumbu la Torati 18:19)
Mkristo anaweza kutaka kuutetea ubatizo kuwa ndio ondoleo la dhambi. Lakini wakrito wote wanakiri kuwa Bw. Yesu hakuwa na dhambi, je iweje asiye na dhambi kama bw. Yesu abatizwe?
Huu kama si uzushi ni kitu gani?