Hamas yasema haina haja na mazungumzo mapya ya kusitisha vita

Hamas yasema haina haja na mazungumzo mapya ya kusitisha vita

Webabu

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2010
Posts
8,870
Reaction score
14,258
1723437896042.png

Wapiganaji wa Hamas chini ya kiongozi wao mpya Yahya Sinwar imesema haitashiriki kwenye mazungumzo yaliyopangwa kufanyika wiki hii.

Badala yake kundi hilo ambalo limepigana na Israel kwa takriban mwaka sasa limesema kinachotakiwa ni kutolewa kwa ratiba kamili ya kutekelezwa kwa makubaliano yaliyokwishafanyika miezi kadhaa iliyopita.

Soma Pia:
Katika salamu walizozitoa kwa waandaaji wa mkutano huo wa mazungumzo ambao ni Qattar,Misri na Marekani,Hamas imesema ni kupoteza muda bure kuzungumzia kitu hicho hicho kila siku na ni kuipa Israel fursa ya kuzidi kuendeleza mauwaji na madhila kwa wapalestina.

Hamas says it won’t take part in cease-fire talks planned for this week

Falme za kialabu waliwada ganya.leo hii wanakipata pata.Wao wanaongelea mbele ya kamera.Hamas wao wanaongelea mbele ya mitutu.
Walidhani underground zao hazitogundulika mapema.
Matokeo yake ikawa kinyume,na inasemekana underground Moja iligundurika kutokea kwa farao.

Nyau akawaambia,ngojeni nitumie hiyohiyo kuwafikia.Wakaomba msamaha kimyakimya na ndo maana unaona amepunguza ukimbelembele coz anaujua mziki ule.
 
Shart kuu hamas wawaachie mateka,hili halitekelezeki maana hamas walishawauwa mateka wote,haya maneno ni kujimwambafai tu.
Kuwaomba Hamas wawaachie mateka ni kukiri kushindwa kwa vita.Na kwa upande mwengine wapongezwe Hamas kwa maandalizi waliyofanya kupambana ambapo sasa ni mwezi wa 10 na bado wanapigana wakiwa wamezingirwa na kukatiwa misaada yote.
 
Sijajua hayo maridhiano ya awali yalikuwa na vipengele gani. Wengine wanasema hii vita inatumika kimkakati ili Netanyahu aendelee kubaki madarakani kwa muda mrefu, kama ni hivyo itachukua muda mrefu kumalizika
Mara ya mwisho makubaliano ambayo yalitangazwa sana na Biden ilikuwa ni kusitishwa vita moja kwa moja,Israel kutondosha jeshi lake Gaza na Hamas kuachia mateka wote iliobaki nao.
 
Kuwaomba Hamas wawaachie mateka ni kukiri kushindwa kwa vita.Na kwa upande mwengine wapongezwe Hamas kwa maandalizi waliyofanya kupambana ambapo sasa ni mwezi wa 10 na bado wanapigana wakiwa wamezingirwa na kukatiwa misaada yote.
Israel hawajari kabisa kuonekana wameshindwa,wao start lao ni moja tu, Hamas wawaachie mateka na wao watakuwa tayari kwa mazungumzo.
Huu ni mwezi wa 10 mnabondwa kila upande,
Harafu wewe unaongea kutokea nje ya uwanja wa mapambano unashupaza shingo watu wa Gaza Leo kesho wanaombea vita iishe.
 
Wale walio ndani ya uwanja wa mapambano ndio hao hao ambao wamechagua kifo kuliko kufru na fedheha.
Ndio maana wanauliwa na kuumizwa lakini mmoja akiinuka tu anashika japo jiwe analirusha.
 
Wale walio ndani ya uwanja wa mapambano ndio hao hao ambao wamechagua kifo kuliko kufru na fedheha.
Ndio maana wanauliwa na kuumizwa lakini mmoja akiinuka tu anashika japo jiwe analirusha.
Kumbe wao waliopo uwanja wa vita wamejichagulia kuuwawa(maana kumpiga Israel hawawezi) wewe mtanzania kiherehere chako chote hiki ni kwa ajili ya Nini?
 
Kumbe wao waliopo uwanja wa vita wamejichagulia kuuwawa(maana kumpiga Israel hawawezi) wewe mtanzania kiherehere chako chote hiki ni kwa ajili ya Nini?
Wamejichagulia kufa kuliko fedheha.Lakini masharti ya kusitisha vita yakitimizwa maisha yatakuwa mazuri kwao na kwa mayahudi.
Huo ni msimamo mzuri sana unaendana na mezani.
 
Back
Top Bottom