Hamis Chaurembo: Dereva mjinga aliyeuwa abiria kwa mwendokasi Kigoma

Hamis Chaurembo: Dereva mjinga aliyeuwa abiria kwa mwendokasi Kigoma

Kwa tabia yake hiyo na mwendo aliokuwa anaenda, pamoja na majina yote hayo utafikiri walikuwa wanaishi mahali ambapo hakuna serikali kabisa

Polisi lazima wanamjua ila amewapoza sana kwa maji ya baridi kwenye vumbi lao huko

Umasikini na tamaa na ujinga unamaliza raia
Na hao utakuta walikuwa wanafurahia mwendo mpaka kumpachika majina ya kipumbavu
Hao polisi walikuwa wanasubiri hilo bomu lilipuke wajinga sana
 
Ngoma zote zilikuwa za njano

Hao wajinga karibia wote wa kakonko kibondo mpaka kasulu huwa wanakimbia sana
 
Nilipanda Probox yake kibondo to Kakonko Nashukuru Mungu siku hiyo ilikuwa saa 12:30 jioni trip yake ya mwisho ya siku. Alitembea speed ya kawaida 80-90kmh. Mungu amsamehe Hamis
 
Kila mtu anajiita sukari ya warembo kwanzia leo mimi najiita chai ya warembo
 
Tatizo tunakimbiza hizi gari alafu hazina matunzo huyo dogo nilishamuona ila nilisikitika japo sikuwa nikimfahamu sana ila stori zake nilisikia nikaona kuna asilimia ya akili zilipungua kichwani mwake. Alafu wajuzi wa mambo walishamuambia afanye yote ila asiingilie familia za watu na hakuwa akielewa sasa kifo kina mengi hicho
 
Hata kama dakika 45 ina maana kama mwendo wa kawaida tuseme KPH 80 unatumia dakika 45 hapo dakika 25 ina maana labda alikuwa anakimbia 150 KPH bila ku slow sasa kwa barabara gani Tanzania hii ukakimbia speed hiyo bila kukutana na matuta. Hapo nawazo barabara lami safi kama ulaya. Kweli barabara huko Kibondo ina quality ya mtu kukimbia 150 KPH bila kupunguza mwendo?
Ni kweli dogo alikua anatembea dk 20 au chini ya hapo kweli kabisa
 
Aliyekuwa Dereva na mmiliki wa gari ndogo, Hamis Chaurembo (27) maarufu kama SIMBA ambaye amefariki baada ya kupata ajali mbaya huko Kibondo Kigoma amezikwa jana.

Ila kuna cha kujifunza hapa kutokana na maneno ya baadhi ya marafiki zake.

"Baadhi ya A.K.A alizopambwa nazo ni pamoja na 'Mwendo wa rocket', ndege ya ardhini, Hamisi on fire' Titanic icon' Sukari ya Warembo'

"Alikuwa akitumia dk 20 hadi 25 kutoka Kibondo hadi Kakonko, watu walimpenda kwasababu ya ucheshi wake, alikuwa hana baya yeye anawasha gari hata kama amepata abiria mmoja.

"Ahadi aliyojiahidi imetimia, katika kauli zake aliwahi kusema

"Siku nikipata ajali ni lazima niondoke na abiria wote".
Wananchi ndio wajing Huwa wanashangilia na pale mmja wao akionya huonekana wa ajabu.
 
No me nimeileta kama ilivyo nikajiongeza kuchek Google earth kuhakikisha hiyo time nikaiweka
google gani wewe umekula maweed yanakuchanganya
Screenshot_20231225-161450.jpg
 
Mkuu macho,

Yupo jamaa ni bodaboda ssahiv hana miguu yote alikatwa.

Na yeye alikuwa hivi hivi, rafiki wa karibu wakawa wanamuambia ndugu acha yule jamaa ni mpemba, lakini kuna wale wanafki wanasema unajua sheikh

Alipata ajali ile miguu ulikuwa kama mlenda ukimshika, amekatwa miguu yote sahiv yupo tu kwenye kibaiskeli.

Vijana ukweli hatusikii na wala hatutaki kuambiwa.
Hizo case za kusifiana ujinga ni nyingi na zimewaachia vijana wengi sana ulemavu wa kudumu acha wale waliokufa.

Namfahamu jamaa zamani miaka ya 2006/7 alikuwa kwenye club ya ya wale jamaa wanaoinua pikipiki Baja wa maeneo ya Kinondoni na kutembea na tairi moja ya nyuma,ilikuwa hivi hivi akiinua ni miluzi na kelele za wenzake siku hiyo pale mteremko wa kutoka Morocco Hotel kuelekea Mkwajuni aliinua vibaya akacheza mistake kidogo tu akavunja spinal cord hadi leo hata kuzungusha shingo hawezi anaingia utu uzima akiwa mlemavu.

Ni vitu vya kusikitisha sana.
 
3-6 hours
3 - 6 hours??? Are you serious? Hayo ni makadirio ya mwendo wa chombo kimoja au transit?
Ungesema 3 kwa gari na masaa 6 kwa baiskeli ningekuelewa.
Kwa unavyofikiri hapo Dar to Moro inawezekana kutumia dakika 20 kwa gari?
 
Aliyekuwa Dereva na mmiliki wa gari ndogo, Hamis Chaurembo (27) maarufu kama SIMBA ambaye amefariki baada ya kupata ajali mbaya huko Kibondo Kigoma amezikwa jana.

Ila kuna cha kujifunza hapa kutokana na maneno ya baadhi ya marafiki zake.

"Baadhi ya A.K.A alizopambwa nazo ni pamoja na 'Mwendo wa rocket', ndege ya ardhini, Hamisi on fire' Titanic icon' Sukari ya Warembo'

"Alikuwa akitumia dk 20 hadi 25 kutoka Kibondo hadi Kakonko, watu walimpenda kwasababu ya ucheshi wake, alikuwa hana baya yeye anawasha gari hata kama amepata abiria mmoja.

"Ahadi aliyojiahidi imetimia, katika kauli zake aliwahi kusema

"Siku nikipata ajali ni lazima niondoke na abiria wote".
Huyu Dogo ni mpumbavu Sana na nimepanda hio gari mara kadhaa kutoka Kibondo Hadi Kakonko
 
Back
Top Bottom