Hamisa Mobetto penzini na Kigogo wa Yanga!

Hamisa Mobetto penzini na Kigogo wa Yanga!

Nimesoma heading na paragraph ya mwisho tu.

Hamisa apewe kombe lake!

Alikua anashindana na kina nani kubadili wanaume mpaka yeye akawa mshindi na inahitajika apewe kombe lake?

Tumefikia Dunia ambayo umalaya ni sifa? yani tunashauriwa malaya tumpe maua kwa kubadili wanaume?
Hizi ni lugha za mjini wewe mgalikoko utajulia wapi? Uwe unauliza kwanza acha kiherehere.
 
Sema anaonekana anafanya kwa usiri mkubwa sana

Anaonekana anamuheshimu sana mkewe

Huyo danga hamisa ajiandae kuachwa tu kama alivyoachwa na wengine
Kabisa, jamaa yuko vizuri sana na hawezi kukubali kuharibu reputation yake kwa wadangaji.
Huyu atapita tu, na hata wakiendelea ni kimyakimya hatutokaa tuone mapichapicha.

Ila awe makini na Hamisa, anajua kutunza 'risiti' zake.
 
View attachment 3005811

Mwanadada mrembo, mwanamuziki, muigizaji, mjasiriamali na mwanamitindo Hamisa Mobetto 29, yuko mapenzini na Kigogo kutoka klabu ya soka ya Yanga.

Mwanadada huyo na kigogo wapo katika penzi la kificho kwa takribani mwezi wa pili sasa.

Penzi lilimea SA, Ubuntu Botho!
Wawili hao walikutana kwenye ndege wakati wa kuelekea kwenye mechi ya marudiano ya mashindano ya Klabu Bingwa Afrika, CAFCL dhidi ya miamba ya Soka ya Afrika ya Kusini Mamelody Sundowns.

Kigogo huyo kijana mwenye haiba ya kitanashati na mwenye sifa kuu tatu wazipendazo zaidi wanawake kutoka kwa wanaume… tall, dark and handsome jina lake hutajwa kwa kutanguliwa na taaluma yake.

Inataarifiwa kwamba wawili hao walizama penzini punde tu walipokutana kwenye ndege, na hadi kutua S.A penzi lilishachipua!

Taarifa zaidi zinasema hata uwanjani walienda kwa gari moja, na walikaa jukwaa moja!

Aziz Ki atumika kuokoa jahazi!
Mwamba kutoka Ouagadougou, Stephen Aziz Ki anatajwa kutumika kuinusuru ndoa ya Kigogo huyo wa Yanga mara baada ya mkewe kushtukia mchezo.

Kama mnavyotujua wabongo huwa tunanyimana michongo ila sio umbea, taarifa zilimfikia mke wa Kigogo ambaye aling’aka na kupelekea ndoa kuwa rehani!

Mwamba Aziz ambaye anatajwa kama mchezaji pendwa zaidi na Kigogo huyo klabuni hapo, ilibidi atumike kutengeneza mapichapicha ya kumpoza mke wa Kigogo.

Ndio yale mliyoona mara wako pamoja wakitokea uwanja wa ndege, wakikumbatiana uwanjani na kwingineko yote yale ni maigizo, Ki hana mahusiano ya aina yoyote na Hamisa bali alitumika kumnusuru boss na mshkaji wake kuepuka dhahma kutoka kwa mke wake.

Penzi hatarini kuvunjika muda wowote!
Baada ya wambea kumsanua mke wa Kigogo, inasemekana wapenzi hao wako hatarini kuachana muda wowote kutokana na suala hilo kumkalia vibaya Kigogo.

Mke wa Kigogo ni dada wa anayetajwa kama mfadhili wa taasisi ya anakofanyia shughuli zake Kigogo. Hilo linamuweka pabaya zaidi Kigogo kwani endapo akiendelea kutoka na mrembo huyo kimapenzi huwenda kibarua chake kikawa hatarini kwani mfadhili hatoweza kuvumilia kuona dada yake akinyanyasika juu ya penzi hilo la mumewe na Hamisa.

Hamisa kiboko, sio mchezo!
Jamani Hamisa apewe kombe lake, ikishindikana basi hata maua maana anastahili. Ndani ya miaka hii mitatu ameshatoka na vigogo kutoka kwenye klabu zote 2 kubwa nchini, achilia mbali kuzaa na wanaume wawili maarufu na wamiliki wa redio 2 kubwa nchini!

Hapo kabla alianza kutoka na Kigogo kutokea Simba, japo penzi lao lilikuwa mithili ya upepo kwani halikudumu.

Lakini licha ya kutokudumu, penzi hilo lilitumika kama chambo kumpatia Mwijaku ajira Simba.

Chanzo changu nyeti kimesimamia show,

Nifah.
Waacheni watu wapanuane viiuno hakuna shida yoyote mkuu
 
Mara ngapi?? Nifah hili faili huna?

Mwaka jana miezi ya mwanzoni nimewaona Bambalaga, kona kabisa wakiwa 0 distance na machawa kama wote zilikuwa zinapita Moet zinapelekwa kwenye meza husika za kumwaga.... kuuliza uliza Dully ana apartment kisasa, ndio dada alikuwa anafikishiwa hapo..
Ninalo darling na nimeshampa mbona? Nakosaje ubuyu mkubwa hivyo?
Hilo file nilipewaga wakati la moto bi mkubwa ndio alikuwa kaingia madarakani.
 
Hizi ni lugha za mjini wewe mgalikoko utajulia wapi? Uwe unauliza kwanza acha kiherehere.
Rubbish!

Iwe lugha ya Mjini au ya Kijijini ila maana yake unataka tumpe sifa mwanamke kwa kufanya zinaa na wanaume wengi,

Kumpa mtu maua yake au kumpa kombe maana yake ni kumpa sifa anayostahili kwa kitendo alichokifanya/anachokifanya,

Mwenye kiherehere ni wewe,kama unaona Mobeto anafaidi nenda na wewe ukatafunwe hovyo ili tukupe hayo maua yako.
 
Kuna wakati nataka ni-react Kwa namna yangu lakini Kila nikiangalia pembeni namwona Mwamba anasoma comments 😅 🙌

Bora tumezeeka sasa 🤗
Ila Mkwe umempata babu, na amani ananipa tele ndio maana nawapa raha na nyie kwa ubuyu.
 
Rubbish!

Iwe lugha ya Mjini au ya Kijijini ila maana yake unataka tumpe sifa mwanamke kwa kufanya zinaa na wanaume wengi,

Kumpa mtu maua yake au kumpa kombe maana yake ni kumpa sifa anayostahili kwa kitendo alichokifanya/anachokifanya,

Mwenye kiherehere ni wewe,kama unaona Mobeto anafaidi nenda na wewe ukatafunwe hovyo ili tukupe hayo maua yako.
Mkuu punguza jazba. Haya ni mambo ya mtandaoni tuu.
 
Mkuu,
Engineer Yale macho yake Ni ya uaminifu kabisa..
Engineer unaweza kumpa kulinda shamba la miwa na ukawa na uhakika miwa ipo salama 😊

Mimi binafsi Ni mtu wakujiulizaga Sana faida na hasara zitakazo patikana in every move in life 😅😂😂
Sawa, mpe na 'shamba' lako alime pia Mkuu.
 
Hamfikii Nandy sababu ya aina ya familia ambao wote wametokea, Hamisa ndiye baba na mama wa familia yao unlike Nandera, kwahiyo wakipata pesa mmoja atanyanyuka haraka kuliko mwenzie.... Halafu

Hata huku mitaani kuna watu tuna upepo wa pesa ila majukumu sasa!!! Rafiki yangu mmoja anaitwa Manka huwa ananiambia kwenye circle yetu ulipaswa uwe na pesa kuliko wote, hajui mimi na yeye tunatofautiana mahali, so yeah Hamisa ametokea familia ya kawaida ya ugali bamia, alipo hapo ni pakubwa sana....
Ndio maana nakupendaga, Asante.
 
Kwamba achi*** ..nimemdharau sana dogo kama ni kweli...ptuuuu..pesa ulizonazo unaweza kula uchafu kama ule halafu utoe range? Ptuuuu....mbona huko duniani kuna pisi kali hata nyingine hzijaguswa kabisa , kuna mahal unaenda unalipia unaletewa pisi kali virgin kabisa ni pesa yako tu .
Wewe ndio mishe zako mjini ?
 
Back
Top Bottom