Hamisa Mobetto penzini na Kigogo wa Yanga!

Hamisa Mobetto penzini na Kigogo wa Yanga!

Tusomeni dini ndugu zangu waislamu, maisha ya dunia ni mafupi sana, why wasioane tu!

وَلَا تَقْرَبُوا الزِّنَا ۖ إِنَّهُ كَانَ فَاحِشَةً وَسَاءَ سَبِيلًا
Al-Isra' (The Journey by Night)
Wala msikaribie uzinzi. Hakika huo ni uchafu na njia mbaya.
Ndugu yangu huwa unanifurahisha na kupenda kote dini na kuijua ila huwa hukauki mitaa kama hii.

Asante kwa ukumbusho.
 
.........kwa nini walikuwa open kiasi cha mke kusmell something fishy, all in all wawe makini, coz haya mambo sometimes huwa yanapelekea kushuka kwa ufanisi wa taasisi au club.........
Wambea hawakosekani Mkuu, ila kushuka kwa taasisi hapana.
Kigogo yuko makini na sio kwamba huyo Hamisa ndio wa kwanza.
 
View attachment 3005811

Mwanadada mrembo, mwanamuziki, muigizaji, mjasiriamali na mwanamitindo Hamisa Mobetto 29, yuko mapenzini na Kigogo kutoka klabu ya soka ya Yanga.

Mwanadada huyo na kigogo wapo katika penzi la kificho kwa takribani mwezi wa pili sasa.

Penzi lilimea SA, Ubuntu Botho!
Wawili hao walikutana kwenye ndege wakati wa kuelekea kwenye mechi ya marudiano ya mashindano ya Klabu Bingwa Afrika, CAFCL dhidi ya miamba ya Soka ya Afrika ya Kusini Mamelody Sundowns.

Kigogo huyo kijana mwenye haiba ya kitanashati na mwenye sifa kuu tatu wazipendazo zaidi wanawake kutoka kwa wanaume… tall, dark and handsome jina lake hutajwa kwa kutanguliwa na taaluma yake.

Inataarifiwa kwamba wawili hao walizama penzini punde tu walipokutana kwenye ndege, na hadi kutua S.A penzi lilishachipua!

Taarifa zaidi zinasema hata uwanjani walienda kwa gari moja, na walikaa jukwaa moja!

Aziz Ki atumika kuokoa jahazi!
Mwamba kutoka Ouagadougou, Stephen Aziz Ki anatajwa kutumika kuinusuru ndoa ya Kigogo huyo wa Yanga mara baada ya mkewe kushtukia mchezo.

Kama mnavyotujua wabongo huwa tunanyimana michongo ila sio umbea, taarifa zilimfikia mke wa Kigogo ambaye aling’aka na kupelekea ndoa kuwa rehani!

Mwamba Aziz ambaye anatajwa kama mchezaji pendwa zaidi na Kigogo huyo klabuni hapo, ilibidi atumike kutengeneza mapichapicha ya kumpoza mke wa Kigogo.

Ndio yale mliyoona mara wako pamoja wakitokea uwanja wa ndege, wakikumbatiana uwanjani na kwingineko yote yale ni maigizo, Ki hana mahusiano ya aina yoyote na Hamisa bali alitumika kumnusuru boss na mshkaji wake kuepuka dhahma kutoka kwa mke wake.

Penzi hatarini kuvunjika muda wowote!
Baada ya wambea kumsanua mke wa Kigogo, inasemekana wapenzi hao wako hatarini kuachana muda wowote kutokana na suala hilo kumkalia vibaya Kigogo.

Mke wa Kigogo ni dada wa anayetajwa kama mfadhili wa taasisi ya anakofanyia shughuli zake Kigogo. Hilo linamuweka pabaya zaidi Kigogo kwani endapo akiendelea kutoka na mrembo huyo kimapenzi huwenda kibarua chake kikawa hatarini kwani mfadhili hatoweza kuvumilia kuona dada yake akinyanyasika juu ya penzi hilo la mumewe na Hamisa.

Hamisa kiboko, sio mchezo!
Jamani Hamisa apewe kombe lake, ikishindikana basi hata maua maana anastahili. Ndani ya miaka hii mitatu ameshatoka na vigogo kutoka kwenye klabu zote 2 kubwa nchini, achilia mbali kuzaa na wanaume wawili maarufu na wamiliki wa redio 2 kubwa nchini!

Hapo kabla alianza kutoka na Kigogo kutokea Simba, japo penzi lao lilikuwa mithili ya upepo kwani halikudumu.

Lakini licha ya kutokudumu, penzi hilo lilitumika kama chambo kumpatia Mwijaku ajira Simba.

Chanzo changu nyeti kimesimamia show,

Nifah.
Hii nayo ni habari? Ulitaka awe na nani kwenye mapenzi? Umaskini wako usiwe gubu kwa wenzio. Tafuta hela na umaarufu utaacha huo ubwege. Jinga sana ww
 
Ila Mkwe umempata babu, na amani ananipa tele ndio maana nawapa raha na nyie kwa ubuyu.
I'm real happy for that Mjukuu 🙏

Najua makwazo yapo, ndiyo maana hata vikombe haviachi kugongana kabatini.

Kikubwa mjue ninyi ni Binadamu, na hakuna anayedate na malaika Kati yenu

Vyema muishi Kwa kuchukuliana.

Ni maombi yangu muishi hadi muufikie Uzee pamoja🙏🙏🙏
 
Huyu kahaba ajue tu umri haujawahi kuwa rafiki kwa mwanamke au muuza K yoyote

Ajifunze kutoka kwa Sepenga na mastaa wengine kama Uwoya wametumika wametemwa kama chewing gum saivi hawana soko au limeshuka sana
Eh, jamani! Yamekuwa hayo tena?
 
Hahaha.........umesema sahihi, na kumbe alianza kudate naye kabla Mzee machache hajaaga maisha

Kuna mtu mmoja aliwahi kusema ukiwa na hela hao warembo Wana dalali wao kabisa wa kuunganisha 🙌
Pamoja na kwamba alishaolewa ila bado akawa anadanga?

Mbona mzee nasikia alikuwa na walinzi binafsi ni ngumu kuchepuka?
 
Na jihan ile familia kama ilimuelewa na upepo wa umaarufu ulianza kumjia ila nahisi kuna watu, walimshtua asiingie mkenge wa kuharibu reputation.

Kuhusu nicole na jamaa 😁😁😁 mambo ya daslam ni mengi sana
Endapo angekubali Chibu angetamba nae sana, ile ndio mali safi ya kutoka sio yule mwingine.

Nicole unaambiwa ule mtindi meneja ndio anajua raha yake, Lols.
 
Duuuhh, kwamba mimi niko nyuma sana na ubuyu wa Tz...

Kumbe Mobeto ana watoto wawili kutoka kwa wanaume wawili tofauti.

Mwanaume mwingine aliyejipatia mtoto pale ni nani mbali na Diamond?
Majizzo mmiliki wa EFM Radio.
 
Back
Top Bottom