Hamjagundua watangazaji vituo vya redio wameanza kung'olewa!?

Ndio maana yake watakuwa walikuwa na zile certificate za STJ chuo cha kina Sinta wa Inaniuma sana ya Juma Nature ...
Hivi alishawahi kufanya kazi za uandishi huyu shemela kwa kaka kiroboto!?
 
Kwahiyo mwandishi asipokuwa chawa wa mzenji ananyimwa usajili bila sababu sio?
 
Mtu hawezi kukaa darasani miaka kadhaa alafu akawa hajui kitu ila yule ambaye hajasoma ndio akawa anajua. Anaweza kuzidiwa ubunifu, passion n.k lakini sio kwamba hajui kitu
 
Tetesi nimeskia waajiriwa lazima kuwa na vyeti...

So wengi wanapigwa chini
Naona poa tu wapungue watu waliokuwa wanafanya upuuzi kwenye media walifanya shamba la bibi media! mtu anajua komedi au mwigizaji au kapata kaumaarufu kidogo kichaka ilikuwa media wabaki influenza
 
Mtu hawezi kukaa darasani miaka kadhaa alafu akawa hajui kitu ila yule ambaye hajasoma ndio akawa anajua. Anaweza kuzidiwa ubunifu, passion n.k lakini sio kwamba hajui kitu
huyu kama hana ndugu janjajanja alikuwa kwenye media basi yeye mwenyewe ndo wale wa elimu sio muhimu muhimu ni kipaji kwenye utangazaji na uandishi
 
Mnataka kusema Masoud Kipanya hasikiki tena pale Mjengoni ?

Kitenge najua alipata zero form four Ila masoud kipanya je
 
Kwani kwenye hizo media houses hakuna News Trainee programs kama BBC au CNN? Maana akina Richard Quest, Fareed Zakaria, Anderson Cooper, Sanjay Gupta, Wolf Blitzer na wengineo hawakusoma journalism ila walipata tu intership na trainee programs zinazoendeshwa na mashirika kama BBC, CNN na kadhalika.
 
Du basic certificate tu mkuu.
watu wasome waende shule hiyo elimu ndogo sana Kwa sehemu walizopo.
kama hawataki Sheria zilazmishe.
 
huo ni utaratibu wa huko ulaya hapa waandishi sheria yao ilishasema mwisho diploma kama unataka kuwa mwandishi wa habari!
 
Mnataka kusema Masoud Kipanya hasikiki tena pale Mjengoni ?

Kitenge najua alipata zero form four Ila masoud kipanya je
kwani alisoma uandishi au kutengeneza kirikuu naona kirikuu anazitendea hwakh!
 
Hii ni nzuri.
Fani ilivamiwa, ukiwa na kaumaarufu tu, basi wewe ni mwanahabari na mchambuzi maalum
naunga mkono mwanabodi, watu wamewekeza halafu jitu limepata tu umaarufu linasema mimi mwandishi wa habari au mtangazaji...waende darasani
 
Kitabu kiheshimiwe jamani, watu wamesota huko darasani, Elimu inadhaurika mjue.
Waje kwa makeshia na wahasibu pia siyo kujua kalikuleta unajifanya mhasibu.
kabisa hao manesi tu lazima wasajiliwe na kupewa leseni...hata waganga wa kienyeji wanaotuunganisha na freemason na wao kuna takwa wasajiliwe na baraza la tiba asili sasa hawa waandishi walikuwa ndio taaluma ambayo ukijua kusoma na kuandika na ukawa na kaumaarufu kidogo tu unaenda kujipachika humo!!
 
noma sana huenda tukaanza kuona mabadiliko kwenye vyombo vya habari upuuzi ulizidi yule masanja amesomea kumbe naendelea kumsikia
Sema waTZ wengi wanafanya kazi kwa mazoea!! Ndo mana kwa mf waandishi unakuta full blah blah na kusifia upumbavu halafu fact ziro kabisaa🚮
 
Sema waTZ wengi wanafanya kazi kwa mazoea!! Ndo mana kwa mf waandishi unakuta full blah blah na kusifia upumbavu halafu fact ziro kabisaa🚮
wengi weupe sana yaani...unasikiliza redio au TV maswali wanayouliza wakati wa interviews mpaka unajiuliza "huyu ni mtangazaji kweli? kasomea? au wamemuokota sehemu wakampa microphone aje aulize maswali, weledi ulikuwa sufuri kabisa!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…