Hamna mtu mwenye tatoo mwenye tabia nzuri

Hamna mtu mwenye tatoo mwenye tabia nzuri

Leo nilikuwa na discuss na mama mmoja hivi na kadada kamoja hapa mtaani kwetu kametoboa pua

Nafikiri baada ya mazungumzo yule dada ataenda kujuta kwann? Alikuwa anasikiliza zile mada, yaani siwaamini kabsa wadada waliotoboa pua wallah
 
Bro, mimi baada ya kumaliza form four, enzi zile likizo ya Mkapa, nikachora tatoo, kabla ya hapo nilikuwa mtoto mzuri kabisa, ila baada ya matatoo,

Nikajikuta sitaki tena kushiriki ibada, nikawa kampani yangu masela, nilianza kujifunza sigara, kisha nikarukia kwenye bangi, baadae nikapotea kabisa.

Mwenendo wangu ukapotea na sikuweza kuendelea tena na masomo.

Baada ya miaka mingi kupita ndio nimeweza kurudi kwenye mstari, baada ya mateso makubwa na kupita the most difficult and hard way
Wewe hayo ni matatizo yako binafsi na kilichokukuta wewe hakiwezi kwa standard unit kwa wote waliochora tatoo, haya Messi baada ya kuchora tattoo alikuwa mtoto mbaya kama wewe?

Watu wote waliochora tattoo wana maisha mabaya kama yako? Kwanini hizo shida uzihusishe na tattoo?

Ninachokiona hapa ni wewe kutafuta justifications juu ya failures zako za kimaisha.

Halafu waafrika tuna mambo ya ajabu sana, kila kitu tunakifikiria kivyetuvyetu tu, tattoo ikuharibie maisha??[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Hii comment yako ni ushahidi tosha kuwa mambo mengi ya ulimwengu wa roho, huyajui, Hata nguvu ulizo nazo kuna uwezekano ukawa huzijui. Michoro mwilini ni hatari kwako, kwani sio ubunifu wa kimbingu but from the devil himself. Ukichora unaweka bikoni mwilini (unakuwa lango la kuingilia). Wala hawapati shida
Hivi hizi ngano huwa mnatoa wapi?[emoji23]
 
Fuatilia mwisho wao, utapata majibu, Anaweza asiadhibiwe yeye, ukapigwa uzao wake, ni kanuni ndivyo inavyosema
Nani kaisema hiyo kanuni? Basi huyo anaetoa hizo adhabu si mtenda haki, kivipi tattoo achore Messi kisha adhabu kipewe kizazi chake?

Unasema tusubiri kuona mwisho wake(Messi) kuwa utakuwa mbaya, unataka kumaanisha wasiochora tattoo kwenye miili yao huwa na guarantee ya kuwa na mwisho mzuri?

Tuonyeshe mabaya tunayoweza kuyashuhudia na kuthibitisha aliyoyapata Messi mara baada ya kuamua kuchora tattoo, achana na swagger za kuusubiri mwisho wake wakati hata wako hauujui.

Acheni porojo, mkifeli maisha msianze kutafuta sabaumbu za kuhalalisha uzembe wenu.
 
Afrika imechelewa kuendelea,
Kila kitu ni kipya kwetu acha twende taratibu tutakuja kujua ulimwengu ukoje na sie tunauchukuliaje baadae tutaenda nao sawa,

Ni suala la muda tu.
Watu wana primitive minds kiwango ambacho unabaki kushangaa tu, reference zenyewe wanatumia za vitabu ambavyo vimetoka kwa haohao wachora tattoos.

Aiseeeeh[emoji23]
 
Kwanini huwezi kujiunga na majeshi kama una tatoo?
Inategemea kujiunga na jeshi la nchi gani??, zipo nchi nyingi zinazokubali watu kujuinga hata kama wana tattoos visible kabisa.

Na nchi nyingi wanajeshi walio serve wengi wana tattoos zinazlwatambulisha vikosi vyao walivyo serve
 
Tattoos hazina nguvu yyte , wala haibadilishi tabia ya mtu. Ni watu tu na tabia zao hap walioamuwa kujichora...,

hata kabla ya kujichora wanajikuta wanatamani Lifestyles flani...!

Ukipenda tabia za kihuni itaiga au kuwa influenced kwenye kila kitu..
 
Shemeji yangu msweden,,nimejuana nae miaka mingiii,ana tattoo kubwa sana mguuni,mdada yule ana roho nzuri sijawahi kuona,na ana tabia nzuri kuliko Dada zangu bado hawana tatoo,kama ushawai kusika kituo cha Myouth center kilikua kituo chake,unajua vijana wangali wa kitanzania wamesaidiwa na kituo kileee?acheni kumhuhukumu MTU kwa style hizo,MTU mbaya ni mbaya tu haijalishi kasuka au kanyoa,unapo quote mstari wa kutojichora,quote na usiibe,usiseme uongo,usiue,usitamani,,tusinyosheane vidole
 
Tattoos hazina nguvu yyte , wala haibadilishi tabia ya mtu. Ni watu tu na tabia zao hap walioamuwa kujichora...,

hata kabla ya kujichora wanajikuta wanatamani Lifestyles flani...!

Ukipenda tabia za kihuni itaiga au kuwa influenced kwenye kila kitu..
Watu wana mindset za kijinga sana mkuu, yani eti kwakua jeshi lao haliruhusu tattoo basi tayari wameichukua kama universal point, Nchi nyingi tu zinaruhusu wanajeshi wao kuwa na tattoo bila shida kabisa, hebu waulize kama hayo majeshi yanayoruhusu tattoo wanayazidi kwa chochote uone majibu yao[emoji23]

Kama hawayazidi hayo majeshi kwa chochote , inakuwaje tattoo inakuwa chanzo cha udhaifu kama alivyosema hapo juu?

Ukiwaambia walete ushahidi wa wanayosema, wote wanakuja na maandiko ya vitabu ambavyo waliletewa na haohao waanzilishi wa hayo ma-tattoo, unabaki kushangaa tu.

Wamaasai kila leo wanajitia tattoos (chata) kwenye miili yao, hebu waulize wamewazidi nini cha msingi zaidi ya mapresha, visukari na stroke huku mijini??

Tabia ya mtu haiwezi kubadilika baada ya kuchora tattoo, inaonekana hivyo kwasababu wahuni wengi ndo huwa na matamanio ya kuchora. Namaanisha wahuni wengi ndo huzifuata tattoo, ndiomaana kuna watu pia ambao ni wastaarabu na wenye mafanikio licha ya kuwa na tattoo.
 
Nikiona naonywa nisifanye jambo na watu niliowakuta kwenye hii dunia silifanyi, maana najua hata kama wakisemacho sio kweli basi kwa heshima hiyo nitayoionesha basi sitokosa pongezi huko mbeleni, Ni sawa na mzazi akuambie usimrudie nyumbani kwake usiku kwa kuwa usiku ni hatari kwako ila kwa kuonyesha kiburi ukawa unaenda na kwa bahati nzuri hujawahi kukumbwa na baya lolote basi elewa bado una kesi mbeleni ya kupuuza wazazi wako.
 
Watu wana mindset za kijinga sana mkuu, yani eti kwakua jeshi lao haliruhusu tattoo basi tayari wameichukua kama universal point, Nchi nyingi tu zinaruhusu wanajeshi wao kuwa na tattoo bila shida kabisa, hebu waulize kama hayo majeshi yanayoruhusu tattoo wanayazidi kwa chochote uone majibu yao[emoji23]

Kama hawayazidi hayo majeshi kwa chochote , inakuwaje tattoo inakuwa chanzo cha udhaifu kama alivyosema hapo juu?

Ukiwaambia walete ushahidi wa wanayosema, wote wanakuja na maandiko ya vitabu ambavyo waliletewa na haohao waanzilishi wa hayo ma-tattoo, unabaki kushangaa tu.

Wamaasai kila leo wanajitia tattoos (chata) kwenye miili yao, hebu waulize wamewazidi nini cha msingi zaidi ya mapresha, visukari na stroke huku mijini??

Tabia ya mtu haiwezi kubadilika baada ya kuchora tattoo, inaonekana hivyo kwasababu wahuni wengi ndo huwa na matamanio ya kuchora. Namaanisha wahuni wengi ndo huzifuata tattoo, ndiomaana kuna watu pia ambao ni wastaarabu na wenye mafanikio licha ya kuwa na tattoo.
Kweli kabisa
 
Kwanini huwezi kujiunga na majeshi kama una tatoo? Kwanini huwezi kujiunga na upadre au uchungaji kama una tatoo?

Tatoo zinavuta nguvu hasi (negative energy) yaani hata kama ulikuwa mwema sana kabla hujachora, ukichora utajikuta tu unapata hamu ya kufanya mambo mabaya.

Mabinti wengi wenye tatoo hawaithamini tena miili yao, ndio maana wako tayari kufanywa popote ili mradi tu wapate pesa.

Wengi baada ya kuchora tatoo wakajikuta wana hamu ya bangi, sigara na madawa ya kulevya.

Hata Mungu mwenyewe ndio maana alikataza kuchora tatoos.

Law 19:28 SUV​

Msichanje chale yo yote katika nyama ya miili yenu kwa ajili ya wafu, wala msiandike alama miilini mwenu; mimi ndimi BWANA
Nawajua wana vitengo kadhaa tena PSU na wanazo na issue zao ni ganja tu hata pombe hawatumii na suti mnawaona..[emoji23][emoji23] ni urembo tu kama kupaka piko kwa madem!
 
Kwanini huwezi kujiunga na majeshi kama una tatoo? Kwanini huwezi kujiunga na upadre au uchungaji kama una tatoo?

Tatoo zinavuta nguvu hasi (negative energy) yaani hata kama ulikuwa mwema sana kabla hujachora, ukichora utajikuta tu unapata hamu ya kufanya mambo mabaya.

Mabinti wengi wenye tatoo hawaithamini tena miili yao, ndio maana wako tayari kufanywa popote ili mradi tu wapate pesa.

Wengi baada ya kuchora tatoo wakajikuta wana hamu ya bangi, sigara na madawa ya kulevya.

Hata Mungu mwenyewe ndio maana alikataza kuchora tatoos.

Law 19:28 SUV​

Msichanje chale yo yote katika nyama ya miili yenu kwa ajili ya wafu, wala msiandike alama miilini mwenu; mimi ndimi BWANA
Hizo imani ziko africa, kwa wenzetu kumkuta soja ana tattoo ni kawaida
 
Back
Top Bottom