Hamphrey Polepole aikubali Katiba Inayopendekezwa na kusema kuwa ni ya wananchi si ya Wanasiasa

[h=3]POLEPOLE: Mambo 70 muhimu ya wananchi yaliyofutwa[/h].................Mambo haya yalikuwa kwenye rasimu ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba ambayo Mwenyekiti wake alikuwa Jaji Joseph Warioba. Leo tunaendelea na maeneo mengine 20. 20. Misingi ya utendaji wa Jeshi la Polisi

Rasimu ya Warioba ilipendekeza kwamba katika utekelezaji wa majukumu yake, Jeshi la Polisi la Jamhuri ya Muungano litazingatia (a) Viwango vya juu vya kitaaluma na nidhamu miongoni mwa wafanyakazi wake; (b) Ulinzi na ukuzaji wa haki za binadamu; (c) Kanuni za uwazi na uwajibikaji; na (d) Kukuza uhusiano na jamii. Warioba akaendelea kusema, Jeshi la Polisi, katika kutekeleza majukumu yake, litashirikiana na vyombo vinavyohusika na kupambana na uhalifu vya nchi washirika katika kufanya uchunguzi na kushughulikia makosa ya rushwa na ufisadi.

Misingi hii yote imefutwa na Katiba Inayopendekezwa.

21. Kuhusu Wabunge wa Kuteuliwa

Wananchi walipendekeza Rais asiwe na mamlaka ya kuteuwa wabunge na baadhi ya sababu zao ni Kutekeleza kikamilifu dhana ya mgawanyo wa madaraka. Kuwa na wabunge wanaotokana moja kwa moja na ridhaa ya wananchi kupitia kura zao na kuwa na wabunge walio huru katika kutekeleza majukumu yao. Rasimu ya Warioba ilipendekeza katika Ibara ya 113(2)(b) kumpa Rais nafasi ya kuteua wabunge watano wanaowakilisha watu wenye ulemavu na ikumbukwe kwamba wabunge hawa watano wanachaguliwa na watu wenye ulemavu wenyewe na Rais anafanya kazi ya kuwateua, hii ni tofauti na Rais kuwateua yeye mwenyewe. Ukisoma kifungu cha 45(2) utaona utaratibu wa kisheria unawekwa kuhakikisha watu wenye ulemavu wanashiriki katika nafasi za uwakilishi.

Katiba Inayopendekezwa katika Ibara ya 129(2)(c) inampa Rais uhuru wa kuchagua wabunge wasiozidi kumi kutoka watu wenye sifa ya kuwa wabunge. Pendekezo hili ni kinyume na maoni ya watumishi wa Ofisi ya Rais Tume ya Utumishi wa Umma na kukiuka msingi wa wabunge kuwa wawakilishi wa wananchi moja kwa moja.

22. Kuhusu sifa ya kielimu kwa mbunge

Rasimu ya Warioba ilipendekeza sifa mojawapo ya kuwa mbunge ni kuwa na elimu isiyopungua kidato cha nne na ajue kusoma na kuandika lugha ya Kiswahili au Kiingereza. Baadhi ya sababu za kuunga mkono pendekezo hili ni pamoja na maendeleo ya sayansi na teknolojia pamoja na changamoto zilizoko katika sekta za uchumi, elimu na utandawazi ipo haja ya mbunge kuwa na elimu ya kutosha kuweza kukabiliana na changamoto zinazosababishwa na mabadiliko haya.

Katiba Inayopendekezwa inapendekeza sifa mojawapo ya kuwa mbunge ni kujua na kusoma lugha ya Kiswahili au Kiingereza. Pendekezo hili liko mbali kabisa na chini ya kiwango cha maoni ya watumishi wa Ofisi ya Rais Tume ya Utumishi wa Umma.

23.Nafasi za Makatibu Wakuu na Naibu Makatibu Wakuu Kikatiba

Rasimu ya Warioba ilipendekeza kuwako na nafasi kikatiba za Makatibu Wakuu watakaoteuliwa na Rais kutoka miongoni mwa watumishi waandamizi katika utumishi wa umma kama watakavyopendekezwa na Tume ya Utumishi wa Umma. Kila Katibu Mkuu atakuwa kiongozi na Mtendaji Mkuu wa Wizara ya Serikali aliyopangiwa na Rais na atashika nafasi ya madaraka ya Katibu Mkuu na kutekeleza majukumu yake kama itakavyoainishwa katika sheria za nchi.

Rais anaweza, kwa mapendekezo ya Tume ya Utumishi wa Umma, kumteua mtumishi mwandamizi katika Utumishi wa Umma kuwa Naibu Katibu Mkuu. Kila Katibu Mkuu atakuwa mshauri wa mwisho kwa Waziri kwa masuala yote ya utendaji na atatoa ushauri kwa Baraza la Mawaziri katika vikao na Kamati zitakazoitishwa na Katibu wa Baraza la Mawaziri. Katibu Mkuu au Naibu Katibu Mkuu hatashika madaraka yake hadi awe ameapa mbele ya Rais kiapo cha utii na uaminifu au kiapo kingine chochote kinachohusu utendaji wa kazi zake kitakachowekwa kwa mujibu wa sheria za nchi.

24. Kamati Maalumu ya Makatibu Wakuu

Rasimu ya Warioba ilipendekeza kuwapo kikatiba kwa Kamati Maalum ya Makatibu Wakuu itakayoongozwa na Katibu Mkuu Kiongozi ambayo itakuwa na majukumu ya kuchambua na kulishauri Baraza la Mawaziri juu ya masuala mbalimbali kabla ya kuwasilishwa na kufanyiwa uamuzi na Baraza hilo na itatekeleza majukumu mengine kama itakavyopangiwa na Baraza la Mawaziri.

Katiba Inayopendekezwa imefanikiwa kufuta msharti hayo yote mahususi licha ya kwamba huu ulikuwa wakati muafaka wa kuiimarisha sekta ya utumishi wa umma kikatiba ili iendelee kutuhudumia wananchi ikiwa na ari, kujiamini na kutenda kwa weledi pasina ya kuvurugwa na mara kadhaa na wanasiasa wabaya.

25. Malengo mahususi ya kiuchumi

Masharti yafuatayo katika malengo mahususi la kiuchumi yamefutwa na Katiba Inayopendekezwa;-kuwaletea wananchi maisha bora kwa kuondoa umaskini

kuweka mazingira bora kwa ajili ya kuanzisha na kuendeleza vyombo vya uwakilishi wa wakulima, wafugaji na wavuvi kuhakikisha kuwa kila mtu mwenye uwezo wa kufanya kazi anapata fursa ya kufanya kazi, kwa maana ya kufanya shughuli yoyote halaliinayompatia kipato kuweka utaratibu wa usimamizi wa kiuchumi nauandaaji wa mipango, kuwezesha malengo ya muda mfupi, muda wa kati na muda mrefu kutekelezwa.

26. Haki ya kutokuwa mtumwa

Katiba Inayopendekezwa imefuta masharti yaliyokuwa yanapiga marufuku mtu kulazimishwa kufanya kazi bila hiari yake, hii ni kinyume na sheria na mikataba ya kimataifa ambayo Tanzania imeiridhia.

27. Uhuru wa habari na vyombo vya habari

Katiba Inayopendekezwa imeweka masharti “pokonyezi” (claw-back clauses) kwenye ibara ya Uhuru wa Habari na Vyombo vya Habari. Rasimu ya Warioba inatoa wajibu kusambaza habari na taarifa kwa wananchi. Katiba Inayopendekezwa inatoa wajibu wa kusambaza habari na taarifa sahihi na za ukweli kwa wananchi.

Kuweka maneno taarifa sahihi na za ukweli ni kuminya haki hii, Katiba inapasa kuweka msingi na sheria ingetoa ufafanuzi. Kuweka hapa kutapelekea kutumika kifungu hiki ndivyo sivyo. kuzingatia miiko ya taaluma ya uandishi na utangazaji wa habari ni suala la sheria na kanuni, na ikumbukwe ulimwengu wa leo hautegemei pekee wanataaluma wa habari kutoa habari, kifungu hiki kitaminya haki hii. Kwa kuweka maneno haya katika masharti ya ibara hii, Uhuru wa Habari na Vyombo vya Habari uko mashakani kabisa.

28. Haki ya Elimu na Kujifunza

Wananchi walipendekeza kutolewa kwa elimu bora ya msingi bure na bila vikwazo ikiwemo kupata elimu bora inayotolewa nje ya utaratibu wa umma kwa gharama nafuu.

Masharti yafuatayo yamefutwa na Katiba Inayopendekezwa:-

Kila mtu ana haki ya: kupata fursa ya kupata elimu bora bila ya vikwazo;

kupata elimu bora ya msingi bila ya malipo na inayomtayarisha kikamilifu mwanafunzi ama kuendelea naelimu ya ngazi inayofuatia au kuweka msingi wa kuanzakujitegemea; kupata elimu bora inayotolewa nje ya utaratibu wa umma kwa gharama nafuu.

29. Haki ya Mtoto

Wananchi walipendekeza kutolewa ulinzi zaidi kwa haki za mtoto na Rasimu ya Katiba Mpya Toleo la Pili iliweka masharti yaliyoelekeza mamlaka ya nchi kuweka utaratibu wa Kisheria utakaowezesha utekelezaji na usimamizi wa haki za mtoto kwa kufuata msingi wa kutoakipaumbele kwa maslahi na manufaa ya mtoto. Masharti haya yamefutwa na Katiba Inayopendekezwa na kufanya haki zilizowekwa katika Ibara hii kuwa kiini macho.

30.Haki za watu wenye Ulemavu

Wananchi na hasa watu wenye ulemavu walipendekeza mamlaka ya nchi kuweka utaratibu wa sheria utakaowezesha watu wenye ulemavu kushiriki kwenye nafasi za uwakilishi.

Katiba inayopendekezwa imeondoa jukumu hili na tafsiri yake ni kwamba wawakilishi wa watu wenye ulemavu wataendelea kuteuliwa pasina ya kuwa na msingi wa kikatiba na kisheria kuhakikisha watu wenye ulemavu wanawachagua wawakilishi wao tofauti na sasa.

31. Haki za wanawake

Wananchi waliotoa maoni hasa wanawake na wanaume walipendekeza kwa sauti moja kuona haki za wanawake zinalindwa, zinahifadhiwa, zinatolewa na kutekelezwa kwa wakati na mamlaka za nchi. Wananchi walipendekeza kuona wanawake wanalindwa dhidi ya unyonyaji na ukatili. Katiba Inayopendekezwa siyo tu imefuta kifungu kinachomlinda mwanamke dhidi ya unyonyaji bali pia imefuta masharti elekezi yaliyokuwamo katika Rasimu ya Warioba ambayo yalikuwa yanazielekeza Mamlaka za nchi kuweka utaratibu wa kisheria utakaosimamia masuala yanayohusu utekelezaji wa masharti ya Ibara hii ikiwa ni pamoja na kukuza utu, heshima, usalama na fursa za wanawakewakiwemo wajane.

32. Haki za wazee

Katiba Inayopendekezwa imefuta masharti yaliyokuwa yanaelekeza “kutambua utu wa wazee na kuheshimiwa kwao pasipo kudharauliwa”.

33. Wajibu wa Raia

Katiba Inayopendekezwa imefuta masharti yaliyokuwemo katika Rasimu ya Warioba juu ya mamlaka ya Bunge kutunga sheria kwa ajili ya kuwawezesha raia kutekeleza masharti ya ibara hii. Kufuta masharti hayo ni kuacha Katiba bila utaratibu mzuri wa kuhakikisha raia wanawajibika kwa taifa letu.

34. Hifadhi ya Haki za binadamu

Katiba Inayopendekezwa imefuta haki na uhuru ambao umeainishwa katika mikataba ya kikanda na ya kimataifa kuhusu haki za binadamu ambazo Jamhuri ya Muungano imeridhia. Huu ni mfano mbaya kabisa hasa kwa Taifa linaloheshimu haki za binadamu kama zilivyoainishwa katika mikataba ya kikanda na kimataifa ambayo Tanzania imeridhia.

Itaendelea...............
 
POLEPOLE: Mambo 70 muhimu ya wananchi yaliyofutwa

.................Mambo haya yalikuwa kwenye rasimu ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba ambayo Mwenyekiti wake alikuwa Jaji Joseph Warioba. Leo tunaendelea na maeneo mengine 20. 20. Misingi ya utendaji wa Jeshi la Polisi

Rasimu ya Warioba ilipendekeza kwamba katika utekelezaji wa majukumu yake, Jeshi la Polisi la Jamhuri ya Muungano litazingatia (a) Viwango vya juu vya kitaaluma na nidhamu miongoni mwa wafanyakazi wake; (b) Ulinzi na ukuzaji wa haki za binadamu; (c) Kanuni za uwazi na uwajibikaji; na (d) Kukuza uhusiano na jamii. Warioba akaendelea kusema, Jeshi la Polisi, katika kutekeleza majukumu yake, litashirikiana na vyombo vinavyohusika na kupambana na uhalifu vya nchi washirika katika kufanya uchunguzi na kushughulikia makosa ya rushwa na ufisadi.

Misingi hii yote imefutwa na Katiba Inayopendekezwa.

21. Kuhusu Wabunge wa Kuteuliwa

Wananchi walipendekeza Rais asiwe na mamlaka ya kuteuwa wabunge na baadhi ya sababu zao ni Kutekeleza kikamilifu dhana ya mgawanyo wa madaraka. Kuwa na wabunge wanaotokana moja kwa moja na ridhaa ya wananchi kupitia kura zao na kuwa na wabunge walio huru katika kutekeleza majukumu yao. Rasimu ya Warioba ilipendekeza katika Ibara ya 113(2)(b) kumpa Rais nafasi ya kuteua wabunge watano wanaowakilisha watu wenye ulemavu na ikumbukwe kwamba wabunge hawa watano wanachaguliwa na watu wenye ulemavu wenyewe na Rais anafanya kazi ya kuwateua, hii ni tofauti na Rais kuwateua yeye mwenyewe. Ukisoma kifungu cha 45(2) utaona utaratibu wa kisheria unawekwa kuhakikisha watu wenye ulemavu wanashiriki katika nafasi za uwakilishi.

Katiba Inayopendekezwa katika Ibara ya 129(2)(c) inampa Rais uhuru wa kuchagua wabunge wasiozidi kumi kutoka watu wenye sifa ya kuwa wabunge. Pendekezo hili ni kinyume na maoni ya watumishi wa Ofisi ya Rais Tume ya Utumishi wa Umma na kukiuka msingi wa wabunge kuwa wawakilishi wa wananchi moja kwa moja.

22. Kuhusu sifa ya kielimu kwa mbunge

Rasimu ya Warioba ilipendekeza sifa mojawapo ya kuwa mbunge ni kuwa na elimu isiyopungua kidato cha nne na ajue kusoma na kuandika lugha ya Kiswahili au Kiingereza. Baadhi ya sababu za kuunga mkono pendekezo hili ni pamoja na maendeleo ya sayansi na teknolojia pamoja na changamoto zilizoko katika sekta za uchumi, elimu na utandawazi ipo haja ya mbunge kuwa na elimu ya kutosha kuweza kukabiliana na changamoto zinazosababishwa na mabadiliko haya.

Katiba Inayopendekezwa inapendekeza sifa mojawapo ya kuwa mbunge ni kujua na kusoma lugha ya Kiswahili au Kiingereza. Pendekezo hili liko mbali kabisa na chini ya kiwango cha maoni ya watumishi wa Ofisi ya Rais Tume ya Utumishi wa Umma.

23.Nafasi za Makatibu Wakuu na Naibu Makatibu Wakuu Kikatiba

Rasimu ya Warioba ilipendekeza kuwako na nafasi kikatiba za Makatibu Wakuu watakaoteuliwa na Rais kutoka miongoni mwa watumishi waandamizi katika utumishi wa umma kama watakavyopendekezwa na Tume ya Utumishi wa Umma. Kila Katibu Mkuu atakuwa kiongozi na Mtendaji Mkuu wa Wizara ya Serikali aliyopangiwa na Rais na atashika nafasi ya madaraka ya Katibu Mkuu na kutekeleza majukumu yake kama itakavyoainishwa katika sheria za nchi.

Rais anaweza, kwa mapendekezo ya Tume ya Utumishi wa Umma, kumteua mtumishi mwandamizi katika Utumishi wa Umma kuwa Naibu Katibu Mkuu. Kila Katibu Mkuu atakuwa mshauri wa mwisho kwa Waziri kwa masuala yote ya utendaji na atatoa ushauri kwa Baraza la Mawaziri katika vikao na Kamati zitakazoitishwa na Katibu wa Baraza la Mawaziri. Katibu Mkuu au Naibu Katibu Mkuu hatashika madaraka yake hadi awe ameapa mbele ya Rais kiapo cha utii na uaminifu au kiapo kingine chochote kinachohusu utendaji wa kazi zake kitakachowekwa kwa mujibu wa sheria za nchi.

24. Kamati Maalumu ya Makatibu Wakuu

Rasimu ya Warioba ilipendekeza kuwapo kikatiba kwa Kamati Maalum ya Makatibu Wakuu itakayoongozwa na Katibu Mkuu Kiongozi ambayo itakuwa na majukumu ya kuchambua na kulishauri Baraza la Mawaziri juu ya masuala mbalimbali kabla ya kuwasilishwa na kufanyiwa uamuzi na Baraza hilo na itatekeleza majukumu mengine kama itakavyopangiwa na Baraza la Mawaziri.

Katiba Inayopendekezwa imefanikiwa kufuta msharti hayo yote mahususi licha ya kwamba huu ulikuwa wakati muafaka wa kuiimarisha sekta ya utumishi wa umma kikatiba ili iendelee kutuhudumia wananchi ikiwa na ari, kujiamini na kutenda kwa weledi pasina ya kuvurugwa na mara kadhaa na wanasiasa wabaya.

25. Malengo mahususi ya kiuchumi

Masharti yafuatayo katika malengo mahususi la kiuchumi yamefutwa na Katiba Inayopendekezwa;-kuwaletea wananchi maisha bora kwa kuondoa umaskini

kuweka mazingira bora kwa ajili ya kuanzisha na kuendeleza vyombo vya uwakilishi wa wakulima, wafugaji na wavuvi kuhakikisha kuwa kila mtu mwenye uwezo wa kufanya kazi anapata fursa ya kufanya kazi, kwa maana ya kufanya shughuli yoyote halaliinayompatia kipato kuweka utaratibu wa usimamizi wa kiuchumi nauandaaji wa mipango, kuwezesha malengo ya muda mfupi, muda wa kati na muda mrefu kutekelezwa.

26. Haki ya kutokuwa mtumwa

Katiba Inayopendekezwa imefuta masharti yaliyokuwa yanapiga marufuku mtu kulazimishwa kufanya kazi bila hiari yake, hii ni kinyume na sheria na mikataba ya kimataifa ambayo Tanzania imeiridhia.

27. Uhuru wa habari na vyombo vya habari

Katiba Inayopendekezwa imeweka masharti "pokonyezi" (claw-back clauses) kwenye ibara ya Uhuru wa Habari na Vyombo vya Habari. Rasimu ya Warioba inatoa wajibu kusambaza habari na taarifa kwa wananchi. Katiba Inayopendekezwa inatoa wajibu wa kusambaza habari na taarifa sahihi na za ukweli kwa wananchi.

Kuweka maneno taarifa sahihi na za ukweli ni kuminya haki hii, Katiba inapasa kuweka msingi na sheria ingetoa ufafanuzi. Kuweka hapa kutapelekea kutumika kifungu hiki ndivyo sivyo. kuzingatia miiko ya taaluma ya uandishi na utangazaji wa habari ni suala la sheria na kanuni, na ikumbukwe ulimwengu wa leo hautegemei pekee wanataaluma wa habari kutoa habari, kifungu hiki kitaminya haki hii. Kwa kuweka maneno haya katika masharti ya ibara hii, Uhuru wa Habari na Vyombo vya Habari uko mashakani kabisa.

28. Haki ya Elimu na Kujifunza

Wananchi walipendekeza kutolewa kwa elimu bora ya msingi bure na bila vikwazo ikiwemo kupata elimu bora inayotolewa nje ya utaratibu wa umma kwa gharama nafuu.

Masharti yafuatayo yamefutwa na Katiba Inayopendekezwa:-

Kila mtu ana haki ya: kupata fursa ya kupata elimu bora bila ya vikwazo;

kupata elimu bora ya msingi bila ya malipo na inayomtayarisha kikamilifu mwanafunzi ama kuendelea naelimu ya ngazi inayofuatia au kuweka msingi wa kuanzakujitegemea; kupata elimu bora inayotolewa nje ya utaratibu wa umma kwa gharama nafuu.

29. Haki ya Mtoto

Wananchi walipendekeza kutolewa ulinzi zaidi kwa haki za mtoto na Rasimu ya Katiba Mpya Toleo la Pili iliweka masharti yaliyoelekeza mamlaka ya nchi kuweka utaratibu wa Kisheria utakaowezesha utekelezaji na usimamizi wa haki za mtoto kwa kufuata msingi wa kutoakipaumbele kwa maslahi na manufaa ya mtoto. Masharti haya yamefutwa na Katiba Inayopendekezwa na kufanya haki zilizowekwa katika Ibara hii kuwa kiini macho.

30.Haki za watu wenye Ulemavu

Wananchi na hasa watu wenye ulemavu walipendekeza mamlaka ya nchi kuweka utaratibu wa sheria utakaowezesha watu wenye ulemavu kushiriki kwenye nafasi za uwakilishi.

Katiba inayopendekezwa imeondoa jukumu hili na tafsiri yake ni kwamba wawakilishi wa watu wenye ulemavu wataendelea kuteuliwa pasina ya kuwa na msingi wa kikatiba na kisheria kuhakikisha watu wenye ulemavu wanawachagua wawakilishi wao tofauti na sasa.

31. Haki za wanawake

Wananchi waliotoa maoni hasa wanawake na wanaume walipendekeza kwa sauti moja kuona haki za wanawake zinalindwa, zinahifadhiwa, zinatolewa na kutekelezwa kwa wakati na mamlaka za nchi. Wananchi walipendekeza kuona wanawake wanalindwa dhidi ya unyonyaji na ukatili. Katiba Inayopendekezwa siyo tu imefuta kifungu kinachomlinda mwanamke dhidi ya unyonyaji bali pia imefuta masharti elekezi yaliyokuwamo katika Rasimu ya Warioba ambayo yalikuwa yanazielekeza Mamlaka za nchi kuweka utaratibu wa kisheria utakaosimamia masuala yanayohusu utekelezaji wa masharti ya Ibara hii ikiwa ni pamoja na kukuza utu, heshima, usalama na fursa za wanawakewakiwemo wajane.

32. Haki za wazee

Katiba Inayopendekezwa imefuta masharti yaliyokuwa yanaelekeza "kutambua utu wa wazee na kuheshimiwa kwao pasipo kudharauliwa".

33. Wajibu wa Raia

Katiba Inayopendekezwa imefuta masharti yaliyokuwemo katika Rasimu ya Warioba juu ya mamlaka ya Bunge kutunga sheria kwa ajili ya kuwawezesha raia kutekeleza masharti ya ibara hii. Kufuta masharti hayo ni kuacha Katiba bila utaratibu mzuri wa kuhakikisha raia wanawajibika kwa taifa letu.

34. Hifadhi ya Haki za binadamu

Katiba Inayopendekezwa imefuta haki na uhuru ambao umeainishwa katika mikataba ya kikanda na ya kimataifa kuhusu haki za binadamu ambazo Jamhuri ya Muungano imeridhia. Huu ni mfano mbaya kabisa hasa kwa Taifa linaloheshimu haki za binadamu kama zilivyoainishwa katika mikataba ya kikanda na kimataifa ambayo Tanzania imeridhia.

Itaendelea...............
Naona mmeo Mwendapole kakupa hii kitu nawe ulivyomchumia tumbo umecopy na kupaste, yani kwa hili unajidhirisha jinsi gani ulivyo Mchumia tumbo mkubwa humu jf, Wewe utabaki kuwa UKAWA MESSENGER full stop.
 
[h=3]humphrey polepole: katiba mpya imejaa uongo [/h]Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya TYC (Tanzania Youth Coalition), Humphrey Polepole. Watu wengi wanaendelea kuichambua Katiba Mpya Inayopendekezwa ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo Aprili 30, mwaka huu itapigiwa kura ya ndiyo au hapana.
Miongoni mwa walioichambua katiba hiyo, ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya TYC (Tanzania Youth Coalition), Humphrey Polepole ambaye pia alikuwa mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba chini ya Jaji Joseph Sinde Warioba iliyokuwa ikikusanya maoni ya wananchi na kuandika rasimu ya kwanza.
Katika maelezo yake, Polepole anaichambua katiba inayopendekezwa kuwa imejaa mambo mengi ya upotoshwaji ambayo wananchi wanapaswa kuyapima kabla ya kuamua kuipigia kura ya ndiyo au hapana. Haya ndiyo aliyoyasema:

Nimeisoma Rasimu ya Katiba Inayopendekezwa, nimeisoma yote, ni bahati mbaya inapigiwa upatu kwamba imebeba mambo ya wananchi, mambo ya wakulima, wafugaji, wavuvi, vijana na kadhalika.
Jamani hiyo ni hadaa, msingi wa muundo umebadilishwa.....................inaendelea

cc: Mmanu,Tumaini Jipya,Blaki Womani,Makusudically,Mkatanyasi,mikatabafeki,Sijuti,Henry Ford,Asante,Hercule Poirot,Intonjanda,BAK,,Yugu,Gwangambo,Mteule Junior,Elli,Nguruvi3....

bila kuwasahau wachumia tumbo wafuatao..(aka vibaraka wa lumumba)
bmbalamwezi,Ebola Hatari,MWASI MWAKENDA,claudiaeliakimu,Usisahau Kunichukia,RAPTOR 22
 
humphrey polepole: katiba mpya imejaa uongo

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya TYC (Tanzania Youth Coalition), Humphrey Polepole. Watu wengi wanaendelea kuichambua Katiba Mpya Inayopendekezwa ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo Aprili 30, mwaka huu itapigiwa kura ya ndiyo au hapana.
Miongoni mwa walioichambua katiba hiyo, ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya TYC (Tanzania Youth Coalition), Humphrey Polepole ambaye pia alikuwa mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba chini ya Jaji Joseph Sinde Warioba iliyokuwa ikikusanya maoni ya wananchi na kuandika rasimu ya kwanza.
Katika maelezo yake, Polepole anaichambua katiba inayopendekezwa kuwa imejaa mambo mengi ya upotoshwaji ambayo wananchi wanapaswa kuyapima kabla ya kuamua kuipigia kura ya ndiyo au hapana. Haya ndiyo aliyoyasema:

Nimeisoma Rasimu ya Katiba Inayopendekezwa, nimeisoma yote, ni bahati mbaya inapigiwa upatu kwamba imebeba mambo ya wananchi, mambo ya wakulima, wafugaji, wavuvi, vijana na kadhalika.
Jamani hiyo ni hadaa, msingi wa muundo umebadilishwa.....................inaendelea

cc: Mmanu,Tumaini Jipya,Blaki Womani,Makusudically,Mkatanyasi,mikatabafeki,Sijuti,Henry Ford,Asante,Hercule Poirot,Intonjanda,BAK,,Yugu,Gwangambo,Mteule Junior,Elli,Nguruvi3....

bila kuwasahau wachumia tumbo wafuatao..(aka vibaraka wa lumumba)
bmbalamwezi,Ebola Hatari,MWASI MWAKENDA,claudiaeliakimu,Usisahau Kunichukia,RAPTOR 22
Mchumia tumbo wewe kibaraka wa UKAWA endelea kucopy na kupaste, Humphrey keshakuoa wewe bado ndoa tu hapo.
 
[h=3]Butiku ahamasisha kura ya hapana Katiba Mpya -[/h]Na Shomari Binda, Musoma
WAJUMBE wa iliyokuwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, wamewataka Watanzania kuikataa Katiba inayopendekezwa kwa kuwa haikuzingatia masilahi ya Watanzania.
Waliyasema hayo juzi katika ukumbi wa MCC, mjini Musoma kwenye mdahalo wa kujadili na kuelimisha wananchi kuhusiana na mchakato wa kupata Katiba Mpya na kuwataka kupiga kura ya hapana.
Akizungumza katika mdahalo huo, aliyekuwa Mjumbe wa Tume hiyo, Joseph Butiku, alisema mchakato wa kukusanya maoni ya Katiba, haukuandaliwa kienyeji bali ulipitishwa kisheria ambapo kazi hiyo ilifanyika kwa kujali masilahi na haki za Watanzania kwa vizazi vijavyo.
"Kuipigia kura ya Ndiyo Katiba inayopendekezwa ni kuuza utu wako, Katiba hiyo haikidhi hata kidogo masilahi ya wananchi ni Katiba inayoandaliwa kwa ajili ya masilahi ya watu fulani fulani," alisema Butiku.
Alisema Tume yao haikupindisha maoni ya wananchi ila baada ya kuikabidhi tu, wapo wajanja kwa sababu zao waliweka mambo yao kwa kupindisha baadhi ya vipengele wanavyotaka wao huku wakitupilia mbali maoni halisi ya wananchi.
Alisema baada ya baadhi ya wajumbe walipoanza kupiga kelele kutetea maoni ya wananchi, walianza kupewa vitisho na lawama nyingi.
Butiku aliwataka Watanzania kuchukua uamuzi ulio huru na kujiamini kwa kuwa wao si wakimbizi bali ni Watanzania halali na mchakato huo si wa vyama vya siasa wala watu binafsi.
"Kwa watu walio na mawazo ya kuipigia kura ya ndiyo, ni sawa na kuisusia nchi," alisema.
Mjumbe mwingine wa Tume kutoka Zanzibar, Ally Salehe, alisema Rasimu ya Warioba ilikuwa Katiba iliyotazama mbele zaidi na iliyokuwa na manufaa kwa Watanzania wote bara na visiwani, lakini cha kushangaza ilitupiliwa mbali.
Alisema maoni ya wananchi yalipuuzwa na mchakato mzima wa Katiba ulighubikwa na wanasiasa ambapo kuna mambo ambayo yanapungua na hivyo kuchangia muungano usiwe na nguvu.
Alisema Bunge la Tanzania hujadili masuala ya Muungano japo hayana masilahi ya kimuungano kwani Zanzibar kuna Bunge la kujadili masuala ya Zanzibar na kwenye maoni ya wananchi kulikuwa na vifungu vizuri vilivyokuwa bayana juu ya suala hilo lakini vimeondolewa.
Mjumbe mwingine, Humphrey Polepole, aliwaeleza wananchi kuwa Katiba inayopendekezwa kwa sasa inatazama Uchaguzi Mkuu mmoja tu ujao badala ya kutazama chaguzi zaidi ya 100 zijazo kwa masilahi ya vizazi vijavyo.
Aidha, aliwataka wananchi kupiga kura ya maoni ya kupitisha Katiba Mpya kwa uelewa na kutambua nini wanafanya na kwa faida gani ili kuondokana na Katiba ambayo itakuwa mzigo na msalaba mkubwa kwao.
Polepole, alisema lengo lao ni kutoa elimu kwa wananchi kuhusu mchakato wa kupata Katiba Mpya na si kwamba wana njama na Serikali.
"Ni ukweli usiopingika kuwa Katiba iliyopo kwenye mchakato haiwafai Watanzania walio na akili timamu na walio na shauku ya kupata haki sawa na si kuwa na taifa la matabaka
"Misingi yote iliyokuwa imepitishwa na Tume ya Warioba kama tunu ya Katiba Mpya iliondolewa ambayo ni uzalendo, uwajibikaji, uadilifu na umoja. Na badala yake wameingiza tunu nyingine bila kujua nini maana ya tunu," alisema Polepole.
Februari mwaka huu Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), itaanza uandikishaji wapiga kuwa katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura na baadaye Machi mwaka huu kampeni zitaanza na kuhitimishwa na kazi ya upigaji kura Aprili 30, mwaka huu.
Pamoja na hali hiyo, yameibuka makundi na taasisi kadhaa za kiraia zikitaka mchakato huo uahirishwe mwaka huu ili kupisha Uchaguzi Mkuu.
Hata hivyo, Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), wametangaza kutoshiriki katika mchakato wa kura ya maoni ya Katiba inayopendekezwa kwa kuitaka Serikali iahirishe mchakato huo hadi mwaka 2016.
 
Butiku ahamasisha kura ya hapana Katiba Mpya -

Na Shomari Binda, Musoma

Endelea kucopy na kupaste UKAWA walishakwambia hawatakupa hela ya ugali endapo hutoingia humu Jf na kuponda mchakato wa katiba, we umeshachanganyikiwa kwa sasa unahitaji upelekwe Mirembe dom.
 
Wewe Tyta ulishaishiwa sera, hoja na maelezo, umebaki na kubeba mizigo ya watu na kutupia kwenye JF.
 
Wana macho lakini hawaoni, wana masikio lakini hawasikii, msome vizuri polepole utamwelewa
 
OHOOO! Nakushukuru. Nami nakukumbusha pia uisome Katiba Inayopendekezwa vizuri ili muda wa kuipigia kura ukifika ukapige kura na kutekeleza wajibu wako wa kikatiba.
 
Wewe acha kuongea ufamba wako humu, katiba yenyewe huijui na hata rangi yake huijui ndo ujifanye unayaona hayo, wakati imefafanuliwa vema kuwa Bunge ndo litatunga sheria ya kuelezea namna akaunti hizo zitakavyofunguliwa na nani mwenye haki ya kufungua na nani haruhusiwi kufungua, jiangalie wewe acha kukurupuka, hapatolewi chakula cha njaa humu ndani.

Acha ujinga wewe na kuudanganya umma imeandikwa ibara ya ngapi?

Ni Warioba na tume yake ndio waliiweka ibara hyo na ikaondolewa na huyu nyoka mwenye makengeza....Angalia Ibara ya 16 rasimu ya pili ya katiba
 
Kwenda zako wewe, ntazidi kukuita kijana nani unamtisha humu ndani, huna lolote wewe mchumia tumbo tu, mkubwa hatishiwi nyoka wa kuchorwa, kawatishe hao hao, kama unabisha nambie wapi nikufate afu tuone utafanya nini, we wa wapi wewe au umetoka mkoa umakuja kushangaa maghorofa town huku? Potea huko.

Post yako ndiyo naiona muda huu...

Nadhani litakuwa jambo la busara nikikupuuza maana unaogopa usichotishwa...

Sijakutisha na sina sababu za kukutisha, ila nilikuwa najaribu kukufunza njia bora za kuwasiliana na mtu usiye mfahamu...majibu yako yamenifanya nikuelewe kuwa huna communication skills....NAKUPUUZA...

Tafakari...
 
Kwenda zako wewe, ntazidi kukuita kijana nani unamtisha humu ndani, huna lolote wewe mchumia tumbo tu, mkubwa hatishiwi nyoka wa kuchorwa, kawatishe hao hao, kama unabisha nambie wapi nikufate afu tuone utafanya nini, we wa wapi wewe au umetoka mkoa umakuja kushangaa maghorofa town huku? Potea huko.

Kwa taarifa yako mimi ni mtoto wa mjini, Sinza kwa wajanja, nimesoma s/msingu hapo Mugabe, sekondari Azania, A-level Tabora Boys, JKT Mafinga, Chuo Udsm...

Kwa hiyo mimi siyo wa umri wako wala kariba yako.
 
Acha ujinga wewe na kuudanganya umma imeandikwa ibara ya ngapi?

Ni Warioba na tume yake ndio waliiweka ibara hyo na ikaondolewa na huyu nyoka mwenye makengeza....Angalia Ibara ya 16 rasimu ya pili ya katiba
Wewe mpuuzi acha uongo wako hapa, warioba hana katiba, yeye aliandika mapendekezo na sio katiba.
 
Kwa taarifa yako mimi ni mtoto wa mjini, Sinza kwa wajanja, nimesoma s/msingu hapo Mugabe, sekondari Azania, A-level Tabora Boys, JKT Mafinga, Chuo Udsm...

Kwa hiyo mimi siyo wa umri wako wala kariba yako.
Kijana vp mbona unaanika progile yako humu kwani nani kakuomba? Kama kakujibu ujinga na wewe si uwe kimya au mjibu?
 
Kuna ndugu mmoja humu ndani kanikosea adabu, nimejaribu kwa staha kumwelimisha asipende kutoa lugha chafu kwa mtu asiyemfahamu au kuwa na mazoea naye yeye akajibu nyodo...
Ameniambia mi mshamba wa mjini niliyekurupukia mji na kushangaa maghorofa...

Kama siyo wewe umebadiri id basi, elewa hivyo...

Tafakari...
 
Back
Top Bottom