Hamza Johari: Timu ya Uchunguzi wa Mkataba wa DP World iliteuliwa na Hayati Magufuli, Rais Samia anaendeleza mchakato

Hamza Johari: Timu ya Uchunguzi wa Mkataba wa DP World iliteuliwa na Hayati Magufuli, Rais Samia anaendeleza mchakato

Tatizo tunamuona JPM kuwa ni shujaa wa taifa na tumeshalipa tafsiri potofu suala zima la DP World.

Tunadhani SSH kwa maamuzi yake mwenyewe alienda Dubai na kuingia mikataba, tunasahau kuwa hawa wawili ni wateuliwa wa chama kimoja cha siasa. Wanatekeleza ilani moja ya uchaguzi.

Tumembagua na kumtusi SSH tukisahau chanzo halisi cha huu mradi ni nani, tukashindwa hata kujiuliza gharama kubwa ya ujenzi wa SGR kwa kuilinganisha na mradi huu wa waarabu.

Siasa kuzitafakari inamtaka mtu atulize kichwa chake vizuri.
Ukiwa Raisi wewe ndio final say. Huwezi kubariki upuuzi halafu uchekewe kwa kichaka cha ilani ya CCM. Raisi ni top wa serikali na top wa CCM na ndio maana magufuli aliendesha nchi kwa namna ambavyo aliona sahihi na hakukuwa na mtu wa kumpinga.
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] ya ndani yanazidi kuwekwa Wazi johnthebaptist

-
β€œTimu ya uchunguzi [kuhusu bandari] iliteuliwa na Hayati Magufuli. Kimsingi ni mwendelezo wa kazi, sio kitu ambacho kimekurupuka ghafla, ni mchakato wa muda mrefu wa serikali kuhakikisha tunakuwa na bandari yenye ufanisi.”

Rais wa awamu ya tano,hakuwa Malaika ,kuna maamuzi mengi alifanya kwa masilahi binafsi au Kijiji Cha Chato alichotoka,kwa mfano ujenzi wa Chato International airport,Chato Zonal Referral hospital, kununua ndege kwa Cash kinyume taratibu na kanuni za fedha za Umma, masuala ya makinikia ambayo watanzania tuliaminishwa kupata virukuu,lakini tumelipwa fedha kiduchu na wazungu wale.Kwa hiyo timu ya uchunguzi wa uendeshaji wa Bandari,ni miongoni mwa maamuzi ambayo hayakuwa sahihi,ndiyo maana wamependekeza bilateral- Agreement yenye mapungufu mengi (fundamental mistakes) yenye kuleta maswali mengi,kuliko majibu. Ushauri wajumbe wa timu ya uchunguzi wachunguzwe na wao,tunamashaka nao na wameipotosha Serikali ya awamu sita
 
Watanzania wengi ni wajinga hawajui serikali inafanya mambo kwa mipango endelevu tusiwalaumu.
 
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ ya ndani yanazidi kuwekwa Wazi johnthebaptist

-
β€œTimu ya uchunguzi [kuhusu bandari] iliteuliwa na Hayati Magufuli. Kimsingi ni mwendelezo wa kazi, sio kitu ambacho kimekurupuka ghafla, ni mchakato wa muda mrefu wa serikali kuhakikisha tunakuwa na bandari yenye ufanisi.”

Uzuri jina linaonekana la Samia case closed
 
Ukiwa Raisi wewe ndio final say. Huwezi kubariki upuuzi halafu uchekewe kwa kichaka cha ilani ya CCM. Raisi ni top wa serikali na top wa CCM na ndio maana magufuli aliendesha nchi kwa namna ambavyo aliona sahihi na hakukuwa na mtu wa kumpinga.
Rais anao washauri haamui peke yake. Hawa wanaosambaza chuki hawaongelei mchango wa wasaidizi wa Samia katika maamuzi yote anayoyafanya.

Hawajiulizi juu ya utekelezaji wa sera kazi anayoifanya SSH akiwa ni mrithi wa JPM anayetekeleza ilani moja na hayati.

Chuki za kijinga na ubaguzi wa rangi haviwezi kuwa ni suluhisho la matatizo yetu ya miaka mingi.
 
Daaah yaan na hili mnataka kumuangushia jumba bovu JPM? NB; Pambaneni na hali zenu kuna uovu ndan ya mkataba tafuteni namna ya ku solve!!
Sasa aangushiwe kwani yeye alikua mwenyekiti wa kijiji au rais wa nchi? Mbona migodi alibinafsisha au siyo rasilimali hiyo.
 
Yani nilivyoona Rostam Aziz amerudi basi nilijisemea tu huyu mtu safari hii ana hasira kuliko mwanzoni.

Sasa anatuibia mpaka bundle za Tigo, yani ukiweka GB moja usithubutu kufunguwa video utakoma ubishi, kwenye hili la DP kama Rostam hausiki mninyonge nife.
Ondoa imani potofu wewe wakati DP world inaanzishwa rostam alikua analima viazi kwao igunga huko tabora hao warabu wana pesa chafu waulize wamarekani.
 
Yani nilivyoona Rostam Aziz amerudi basi nilijisemea tu huyu mtu safari hii ana hasira kuliko mwanzoni.

Sasa anatuibia mpaka bundle za Tigo, yani ukiweka GB moja usithubutu kufunguwa video utakoma ubishi, kwenye hili la DP kama Rostam hausiki mninyonge nife.
Hahaha [emoji38]
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] ya ndani yanazidi kuwekwa Wazi johnthebaptist

-
β€œTimu ya uchunguzi [kuhusu bandari] iliteuliwa na Hayati Magufuli. Kimsingi ni mwendelezo wa kazi, sio kitu ambacho kimekurupuka ghafla, ni mchakato wa muda mrefu wa serikali kuhakikisha tunakuwa na bandari yenye ufanisi.”

Ivi ni JPM aliye kwenda Dubai kufungua nchi, ?
 
Daaah yaan na hili mnataka kumuangushia jumba bovu JPM? NB; Pambaneni na hali zenu kuna uovu ndan ya mkataba tafuteni namna ya ku solve!!
Wanafikiri, au wameshauriwa, au wamedanganywa??

Hapana kwa yote. Ni wapuuzi!

Wamepuuza Wananchi, wanawachonganisha Wananchi.

Kwa uhakika mkubwa, hakuna uhusiano wa moja kwa moja wa kamati iliyosemwa na iliyoanzishwa wakati wa JPM, kwamba ilipewa jukumu la kutafuta ufanisi wa Bandari na mapitio ya mkataba huo. Hakuna.

Inatosha kusema kwamba ufanisi wowote uliotafutwa ulikuwa kwa njia yoyote au sura au fomu, ukaguzi wa mkataba mkononi.

Ila, pia ni kwa asili, kwamba utawala wowote ukiwa unataka kuboresha baadhi kama si wote wa mashirika yake yote na kuongeza au kuboresha ufanisi huwa wanafanya hivyo ili(mashirika-hapa bandari) waweze kufuata sera ambazo ziko mkononi na kwamba inaona kufanya hivyo kuwa na manufaa na tija kwa muda mrefu, kwa mustakabhali wa Nchi. Na uhakika, kuwatwisha DPW haikuwa sera wala nia ya Uongozi chini ya JPM

Sio sahihi kwa mleta mada, au Johari kutaka kuunganisha juhudi za kuongeza ufanisi wa kamati zilizoundwa huko nyuma na Udhaifu wa serikali hii.

CCM hii madarakani ni Lazima wapumzishwe. Ni Lazima kwa Usalama na Mustakabhali wa Nchi. Huu upotoshaji wa hali hii, inadhihirisha , kama wadau wengine wanaodai humu kuwa kuna Jinamizi katika mkataba huo.
 
JPM alikuwa na akili timamu. Kamwe asingeweza kufanya ujinga kama huu.
 
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ ya ndani yanazidi kuwekwa Wazi johnthebaptist

-
β€œTimu ya uchunguzi [kuhusu bandari] iliteuliwa na Hayati Magufuli. Kimsingi ni mwendelezo wa kazi, sio kitu ambacho kimekurupuka ghafla, ni mchakato wa muda mrefu wa serikali kuhakikisha tunakuwa na bandari yenye ufanisi.”

Mleta mada amepotosha umma kwa kuunga unga. JamiiForums nayo, kwa ajili ya kuongeza Trafiki, wamenyamazia uwongo huu wa hali ya Juu.

Nimesema, Uwasilishaji wake wa Mada humu ndani huwa ni tata.
 
Back
Top Bottom