Hamza Johari: Timu ya Uchunguzi wa Mkataba wa DP World iliteuliwa na Hayati Magufuli, Rais Samia anaendeleza mchakato

Majibu ya Uchunguzi yako wapi ?
 
Hamza Johari apewe mauwa yake.

Apewe mauwa ya mayai Viza haraka sana kwa Upotoshaji.
 
Kwanini asihusike Mkuu. Mambo yanatia hasira haya.
 
Umepiga mulemule
 
Sasa aangushiwe kwani yeye alikua mwenyekiti wa kijiji au rais wa nchi? Mbona migodi alibinafsisha au siyo rasilimali hiyo.
Nani kafanya activation ya mkataba? Kulikua na ulazima gan wa kuridhia jambo ambalo halina afya kwa Taifa? Why wasilaumiwe hawa waliopo. Cz DP world hawajaanza utendaji!!
 
Nani kafanya activation ya mkataba? Kulikua na ulazima gan wa kuridhia jambo ambalo halina afya kwa Taifa? Why wasilaumiwe hawa waliopo. Cz DP world hawajaanza utendaji!!
Wewe unasema jambo halina afya umeona matokeo ya uwekezaji huo wa bandari angalau hata kwa miezi 6?
 
Wewe unasema jambo halina afya umeona matokeo ya uwekezaji huo wa bandari angalau hata kwa miezi 6?
Afya nayoisemea ni ya stage ya kimkataba! Ndan kuna mamb hayana afya kwa Taifa... Duration, terms and conditions!! Soma iyooo!!
 
Acha kumtumia magufuli Kama punching bag ya kujisafisha mbona wale waliotumbuliwa na magufuli January na Nape mliwarudisha kwa mbwembwe na kejeli na misemo ya kisabengo eti "usirithi maadui wa mwenzako" kwa hiyo na hiyo timu mlikuwa na uwezo wa kuibomoa tu,mbona kabudi na lukuvi mlimwondoa kwenye Baraza la mawaziri,mbona kalemani mlimwondoa kwenye Baraza la mawaziri,mbona bashiru mlimwondoa kwenye ukatibu mkuu kiongozi,nk,kwahiyo bandari ni nyie mmetengeneza set up ya upigaji
 
Haswa.
Kwa namna moja, inatia hasira, ila kwa namna nyingine ndio inanipa nguvu mpya....ndio inawapa Wananchi nguvu mpya ya kuenda kuhakikisha, mkataba baina ya CCM na wapiga kura wake umefika tamati.

Mapinduzi lazima yatokee ndani ya CCM yenyewe. Waondoe hofu tuuu, wanaweza.

Tukumbuke Mkakati wa Ukoloni mamboleo umechukua sura mpya. Kuna Vibaraka wake Ndani ya CCM. Tuwakatae.
 
Yawezekana mkataba huo hujausoma ndio maana umetoa hoja yako hiyo ambayo ni kinyume kabisa na hoja zinazopinga uwekezaji huo. Mimi nitaendelea kupinga huo uwekezaji kwa mkataba huo ulivyo wa hovyo hata ukirekebishwa.

DPW kama ina nia ya dhati kuwekeza Tanzania, ipitie ama kwenye Kituo cha Uwekezaji (Tanzania Investment Centre) au iingie ubia na Mamlaka ya Bandari (Tanzania Ports Authority) ambapo tayari wana MoU. Njia zote 2 zina taratibu zake, lakini siyo kuingiza Serikali Kuu (kwa maana ya nchi) kwenye mkataba usio na kikomo, labda kama nyuma ya pazia kuna jambo ambalo ni Rais mwenyewe tu analijua kwa agenda yake ya siri.

SGR ni mradi wa kimkakati unaotekelezwa na Serikali, hivyo basi, huwezi kulinganisha na mkataba unaoiweka DPW kama mwekezaji. SGR ikikamilika na kama Mamlaka ya Reli (Tanzania Railway Authority) itaona kuna tija kuingia ubia na mwekezaji kutoka nje, itafanya hivyo kwa Sheria, Taratibu na Kanuni zilizopo.
 
Kwenda kuonana moja kwa moja na bunge naamini ni taratibu tu kulingana na ukubwa wa mradi wenyewe.Hii sio biashara ya kitoto. SGR kwa sehemu kubwa imejengwa kuhudumia mradi wa aina hii.

Na reli hiyo kumbuka ilivyokutana na upinzani wakati inaanza kujengwa, Huko Rwanda Kagame keshajenga na kufungua Dry Port kwa ajili ya kuweka mzigo unaotoka pale pale Rwanda na mwingine kutoka DRC.

Kusema kwamba hakuna ukomo ni suala la uelewa juu ya kipi kisicho na ukomo. Ule mkataba MAMA uliopelekwa bungeni hauna ukomo lakini ile itakayosainiwa kwa ajili ya kuanza kwa biashara itakuwa na ukomo kulingana na mazingira yenyewe ya kibiashara.
 
Mimi sipingi uwekezaji bandari na mahitaji ya kupanuka bandari kulingana na mahitaji ya ukubwa wa mizigo hasa SGR ikianza kazi. Ninapinga ni mkataba wa IGA isipokuwa DPW iingie ubia na TPA kwa Sheria, Kanuni na Taratibu zilizopo. Serikali isimamie tu huo mkataba unatekelezwa ipasavyo
 
Tuweke Kumbukumbu sawa...Rostam wlirudi kipindi Cha Jiwe! Unakumbuka mdogo wake alipkamatwa na nyara za aserikali..baadaye Jiwe akamwachia!
 
Kwa Nini Mkataba wa Mama usiwe na Ukomo!?Bwana Chawa Mwandamizi.
 
Mpaka mmeingia kutaja jina la Magufuli ili liwasaidie kuwaamini mnachoongea...Hatutawaamini kamwe!
 
Kwa statement hii maana yake huu mkataba unashida, mbona watu wanakimbia kuwajibishwa, ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…