Wanafikiri, au wameshauriwa, au wamedanganywa??
Hapana kwa yote. Ni wapuuzi!
Wamepuuza Wananchi, wanawachonganisha Wananchi.
Kwa uhakika mkubwa, hakuna uhusiano wa moja kwa moja wa kamati iliyosemwa na iliyoanzishwa wakati wa JPM, kwamba ilipewa jukumu la kutafuta ufanisi wa Bandari na mapitio ya mkataba huo. Hakuna.
Inatosha kusema kwamba ufanisi wowote uliotafutwa ulikuwa kwa njia yoyote au sura au fomu, ukaguzi wa mkataba mkononi.
Ila, pia ni kwa asili, kwamba utawala wowote ukiwa unataka kuboresha baadhi kama si wote wa mashirika yake yote na kuongeza au kuboresha ufanisi huwa wanafanya hivyo ili(mashirika-hapa bandari) waweze kufuata sera ambazo ziko mkononi na kwamba inaona kufanya hivyo kuwa na manufaa na tija kwa muda mrefu, kwa mustakabhali wa Nchi. Na uhakika, kuwatwisha DPW haikuwa sera wala nia ya Uongozi chini ya JPM
Sio sahihi kwa mleta mada, au Johari kutaka kuunganisha juhudi za kuongeza ufanisi wa kamati zilizoundwa huko nyuma na Udhaifu wa serikali hii.
CCM hii madarakani ni Lazima wapumzishwe. Ni Lazima kwa Usalama na Mustakabhali wa Nchi. Huu upotoshaji wa hali hii, inadhihirisha , kama wadau wengine wanaodai humu kuwa kuna Jinamizi katika mkataba huo.