Hamza Johari: Timu ya Uchunguzi wa Mkataba wa DP World iliteuliwa na Hayati Magufuli, Rais Samia anaendeleza mchakato

Hamza Johari: Timu ya Uchunguzi wa Mkataba wa DP World iliteuliwa na Hayati Magufuli, Rais Samia anaendeleza mchakato

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] ya ndani yanazidi kuwekwa Wazi johnthebaptist

-
“Timu ya uchunguzi [kuhusu bandari] iliteuliwa na Hayati Magufuli. Kimsingi ni mwendelezo wa kazi, sio kitu ambacho kimekurupuka ghafla, ni mchakato wa muda mrefu wa serikali kuhakikisha tunakuwa na bandari yenye ufanisi.”

Huko ndani inaonekana kuna wajinga wengi kweli. Yaani kwenda kutengeneza uwongo kama huu wanaona wamefanya kazi kubwa na kutumia akili sana.

Namwonea huruma Rais Samia kwa kukosa watu wenye akili wa kuweza kumsaidia.
 
Kinachozidi kushangaza

Mbona inatumika nguvu kubwa sana kutetea hawa waarabu..
Nguvu inatumika kutetea biashara iliyotumia mtaji mkubwa sana mpaka dakika hii. Ni biashara inayokwenda kutupaisha kiuchumi ukizingatia volume nzima ya kinachotegemewa kuja ni kikubwa sana kutoka DRC.

Rais Tshisekedi alifanya ziara nchini ya siku kama tatu hivi, siku ya kwanza kabisa akaenda bandarini kutazama ukarabati umefikia hatua zipi, na ni wakati wa JPM.
 
Wanasheria wanasema kwa Bunge kuridhia Ule Mkataba umeshakuwa Sheria

Kuna Hoja tena hapo bwashee?!
Wanasheria wetu hao wa kusaini viapo wenye ofisi zao kariakoo na mitaa ya uswahilini ni majanga matupu.

Wanasahau kuwa ipo mikataba ya kibiashara itakayosainiwa siku zijazo ndio yenye umuhimu kuliko huo wa bungeni, inao uwezo wa kuvunja mkataba mama uliopitishwa bungeni.

Ni suala la uelewa tu
 
Bandari wapewe SUMA JKT wanatosha kwa kweli!

Ni Jeshi letu Wananchi
 
Hivi hawa watu wanatuonaje watanzania? Hakuna anaekataa uwekezaji nyie wahishimiwa. Tunakataa vifungu vya hovyo vilivyomo kwenye mkataba huo. Mbona hamtaki kutusikiliza? Kwa nininaving'ang'ania? Kwa nini hamtaki vibadilishwe? Kuna nini nyuma ya pazia?
SAWASAWA 👍
 
😂😂😂😂 ya ndani yanazidi kuwekwa Wazi johnthebaptist

-
“Timu ya uchunguzi [kuhusu bandari] iliteuliwa na Hayati Magufuli. Kimsingi ni mwendelezo wa kazi, sio kitu ambacho kimekurupuka ghafla, ni mchakato wa muda mrefu wa serikali kuhakikisha tunakuwa na bandari yenye ufanisi.”

Tatizo ni mkataba mbovu acheni kuleta siasa hapa. Mchakato wa maboresho ya bandari ulianza muda mrefu ndio maana Bandari za Dar, Mtwara na Tanga zilikuwa zinachimbwa kuongeza kina chake lakini maswala ya DP World yameanza baada MOU iliyosainiwa Dubai baada ya Rais Samia kuhudhuria maonyesho huko Dubai. Hata Mkataba wenyewe kwenye preamble umeonyesha mchakato ulianzaje hakuna sehemu yoyote unamtaja Hayati Rais Magufuli bali ni Rais Samia. Huyo Hamza ana weweseka bure tu kama kulinywa aendelee tu kulinywa!
 
Kwani wengine walipataje hiyo Teknolojia?
Suma JKT ni akili zile zile za kirasimu za kitanzania. Hawa DP World sio waarabu kama tunavyokuja na akili mbovu za kibaguzi, hawa ni wazungu wataalam wanaoajiriwa na waarabu kufanya hizi shughuli wakiwa na uzoefu wa kutosha.

Waswahili hatuna professionalism kwenye masuala ya kitaalam.
 
Kwani wakiwa Waarabu kuna tatizo gani?

Mbona ASAS ni Mwarabu na ana visima vya Mafuta Saudia na tuko naye CCM fresh tu tena Mnec
 
Mimi ngoja hao DP world waje nipate kibarua changu sina cha kupinga Mimi naungana na SSH
 
Back
Top Bottom