MAGARI7
JF-Expert Member
- Mar 5, 2016
- 2,401
- 1,303
Je, yuko wapi kwa sasa na anafanya nini.?!Magariz,
Daisy yu hai.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Je, yuko wapi kwa sasa na anafanya nini.?!Magariz,
Daisy yu hai.
Magariz,Je, yuko wapi kwa sasa na anafanya nini.?!
Pasco,Mkuu Maalim
Mohamed Saidasante kwa taarifa, kutujulisha kumbe enzi zile ni Nyerere ndio alikuwa anatia watu jela na kuwafunga tuu!, ila haikusemwa watu hao waliofungwa na Nyerere, walikuwa wanafunguliwa na nani kutoka vifungo hivyo vya Nyerere?!. Mimi nilidhani ungesema ni serikali ya Nyerere!, kumbe ni Nyerere!, asante!.
Kwa msio jua kilichotokea Zanzibar baada ya mapinduzi yale matukufu ya 1964, wapinzani wa Karume walikuwa wana vanish into thin air, hata unywele haukuonekana (taarrifa zisizothibitishwa zilisema walininginizwa majiwe shingoni, kutiwa ndani ya magunia na kutoswa baharini). Kufuatia Mwalimu Nyerere kuwa ni mcha Mungu, hakuridhishwa na kinachoendelea kule, hivyo ili kuwanusuru waliotofautiana na Karume, aliwachukua na kuwafunga huku bara ambayo hiyo ndio salama yao!, hivyo ndivyo Nyerere alivyowanusu wengi akiwemo Col. Mafudha, Abrahman Mohamed Babu na baadhi ya Makomredi, vinginevyo saa hizi, tungekuwa tunazungumza mengine!.
Kiukweli shukrani ya punda ni mateke!, asingekuwa Nyerere na Muungano, baada ya yale Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, sijui ingelikuwaje kwa race fulani kule Zanzibar, halocust ingekuwa ni afadhali maana angalau ulipatikana japo mfupa au hata majivu!, Zanzibar hata unyayo tuu ulipokanya mara ya mwisho,usingeonekana, sii unywele wala ukucha!. Badala ya kushukuru ndio kwanza watu humu wanabeza!.
Kwa amsiomjua Nyerere, japo nchi yetu ina adhabu ya kifo, katika utawala wake wa miaka 23, alisaini hati moja tuu ya kunyongwa kwa Mwamwindi!. Aliyefuatia ni swala tano!, uliza alisaini hati ngapi na watu wakanyongwa!.
Vitu vingine bora tuacheni tuu!, harakati za kumtangaza Nyerere ni Mwenye Heri, zinaendelea!.
Pasco
Mkuu Maalim Mohamed Said, kwanza nakiri sina nijuacho, na sio zaizi yako, na hata hayo Mapinduzi Matukufu nimeyajua kwa kusoma tuu na kuhadithiwa!.Pasco,
Unachokijua wewe ni, ''mapinduzi matukufu,'' huna kingine.
Ni kweli waliofungwa jela za Bara walinusurika kuuawa.
Lakini iweje umshukuru mtu aliyekukata mkono kwa kukurudishia kidole gumba?
Pasco,
Hebu jitulize na isome historia kwanza kabla hujataka kupambana na mimi.
Watoto wa mjini wana Kiswahili chao.
Wanasema, ''Mimi si saizi yako.''
Maana ukinivaa utapwaya.
Pasco,Mkuu Maalim Mohamed Said, kwanza nakiri sina nijuacho, na sio zaizi yako, na hata hayo Mapinduzi Matukufu nimeyajua kwa kusoma tuu na kuhadithiwa!.
Sipambani na wewe bali tunatofautiana tuu kwa mmoja wetu kuwalisha watu urongo humu, na baadhi yetu kukataa kuumeza urongo huo !.
Dini zumetufunzwa kuwa na shukani katika madogo ili tuweze kupewa makubwa!, ni Nyerere ndiye aliyetupatia uhuru, kwa hili pekee hana budi kuenziwa na kushukuiwa daima!. Wengine hatuna uvumilivu wa kuona licha ya kutangulia mbele ya haki, kila uchao, unakuja humu na posti zako za udini ulikubuhu mtu kisha kumbeza!.
Kama mtu amehukumiwa kifo kwa upanga, na sheria ya upanga ule ni kupigwa kwa pigo moja tuu!, inapotokea yule mkata upanga akakuepushia kifo na badala ya kukata shingo, upanga ukashukia kwenye mkono na kukata mkono hivyo kuepuka kifo, mtu aliyesalimika kifo, atamshukuru mchinjaji kwa kumuepushia kifo badala ya kumlaani kwa kumkata mkono!.
Hao walionusuishwa kifo na Nyerere huko walipo wanamshukuru Nyerere, who are you kumbeza kila uchao?!.
Mimi japo sii mwanazuoni na sii mwandishi kuyaandika yote niliyoyasikia, lakini nimezungumza na Sheikh Mkuu Hemed Bin Jumaa Bin Hemed, Sheikh Kassim Bin Juma, Sheikh Nurdin, Sheikh Yahya Hussein, Sheikh Comorean, Sheikh Jabir, Omar Matata na wengine wengi, misimamo yao naijua na shukrani zao kwa Nyerere nazijua huku waliko wanakusoma na kukushangaa jinsi unavyombeza humu!.
Maadam wewe wasema ''Mimi si saizi yako, ukinivaa utapwaya", kiukweli nimekuvaa na nimepwaya and here I rest my case!, endelea kulisha watu urongo, wa kumeza watameza, wa kutema watatema hadi watakapotokea saizi yako ndio labda watatunusuru na urongo wenye kupandikiza mbegu za chuki za udini kwa kisingizio cha kuhifadhi historia!
Asante.
Pasco
Pasco,
Hakuna anaekataa kuwa Mwalimu Nyerere ndiye aliyeoongoza mapambano dhidi
ya Waingereza.
Historia hii imeandikwa na sote tunaikubali ila ninachosema mimi ni kuwa mbona
hakuwa peke yake katika mapambano hayo?
Licha ya hilo kuwa hakuwa peke yake ninachosema mimi ni kuwa mapambano ya
kudai uhuru yalianza kabla yake.
Na kuthibitisha hilo ndipo nikaandika kitabu cha Abdul Sykes nikitumia njia ya
''biographical approach.''
Nimekuwekea Kamati ya Siasa katika TAA ambayo Abdul Sykes aliipa jina la TAA
Political Subcommittee kama nyaraka zake zinavyoonyesha na hii ilikuwa 1950.
(Annual Report of the Secretary of Tanganyika African Association, 7 January, 1951.
Sykes' Papers).
Katika taarifa hii Abdul kaeleza mengi kuhusu juhudi za kuja na chama cha siasa.
Soma kitabu changu yote nimeeleza kwa urefu na mapana yake.
Nyaraka hizi zipo na sasa zina umri wa miaka 66 na zilikuwa mikononi kwa marehemu
Ally Sykes hadi alipofariki.
Abdul Sykes awe muongo mkweli uwe wewe kwa kuzungumza na Omari Matata
ambae hakuna anaemjua katika histori ya Tanganyika?
Nyerere hakuweko katika kamati hii.
Nimekuwekea majina ya wanakamati wote na hawa ndiyo waliouanda TANU 1954.
Lipi la uongo nililosema mimi.
Sasa ngoja nije katika saikolojia ya watu unaodai kuwa ulizungumzanao kuhusu
historia ya TANU.
Labda hukuwa unajijua wala hukuwa unajua hali ya wakati ule ulipozungumzanao.
Kwa watu hawa kama Sheikh Kassim Juma na Nurdin Hussein wewe ulikuwa
mpelelezi umetumwa kuwachimba na ndiyo maana wakakufurahisha kwa kukupa lile
ambalo ndilo lililokuwa likitakiwa liwe.
Mimi Sheikh Kassim ni kaka yangu.
Aliwekwa ndani na hiki ni kisa mashuhuri.
Kuna khutba imepewa jina, ''Leo Nitataja Majina.''
Siku alipotoa khutba hii mimi nilikuwapo ilikuwa katika khutba ya Ijumaa Msikiti wa
Mtoro huu ndiyo wakati ule alipokuwa anapambana na serikali kuhusu madhila ya
bucha za nguruwe.
Hiyo ndiyo siku hadharani Waislam walimsikia Sheikh Kassim akieleza historia ya
Abdul Sykes na Nyerere katika kupigania uhuru wa Tanganyika.
Jiulize kipi kilichomfanya Sheikh Kassim kuvunja mwiko siku ile?
Mwiko uliokuwa umehifadhiwa kwa zaidi ya miaka 40?
Siku ile pia alimtaja na Rajab Diwani.
Mimi nimeishi ndani ya historia hii na hao wote ninaokutajia wakinijua
na mimi nikiwajua ingawa nilikuwa kijana na mdogo kwao wote.
Nawafahamu vizuri kila mmoja wao na misimamo yao ya siasa.
Pasco,
Wewe ni mgeni kwa watu hawa.
Sheikh Nurdin Hussein ni mzee wangu.
Nawajua wanae tumekua sote Kariakoo.
Sheikh Nurdin Hussein alihidhuria mkutano ule wa Mtaa wa Pemba
wa 1955 ambao Sheikh Hassan bin Amir alitoa wazo kuwa TANU
ichukue kwa makusudi mwelekeo wa ''nationalist-secularist party.''
Nina hakika Sheikh Nurdin alikuficha haya hakukueleza kwa kuwa
hakuwa anakuamini wala kukufahamu umetokea wapi.
Sheikh Nurdin aliwekwa ndani na Nyerere na kupelekwa uhamishoni
Ngombezi labda hilo pia hakukueleza.
Sheikh Ali Comorian rika langu mchezo wetu mmoja.
Baba yake Sheikh Ali Mzee Comorian alifungwa na Nyerere wakati
Sheikh Hassan bin Amir alipokamatwa na kufukuzwa Tanganyika 1968.
Kwa wote hao niliokutajia mimi si ''outsider,'' kama wewe.
Hawa ukienda wewe kutaka kuwauliza historia ya TANU tayari ushawatisha.
Hao wengine katika masheikh uliowataja wala sioni kama ipo haja ya kusema
lolote.
Mwisho mimi sijapatapo kumbeza Nyerere siwezi kukosa adabu kiasi hicho
na kama una ushahidi wa hili ulete hapa barzani watu wote waushuhudie.
Ila mimi siwezi kumpa Nyerere sifa isiyokuwa yake wala siwezi kumdhulumu
kwa lile ambalo kwa hakika anastahili kusifiwa.
Historia ya TANU na kudai uhuru wa Tanganyika ni mimi niliyokuja kuikamilisha.
Pasco,
Nakuwekea kumbukumbu muhimu:
![]()
Sheikh Kassim siku alipotolewa jela hapa ni Msikiti wa Mtoro
Uncle Jei Jei,Mzee Mohammed Said, umesema huwezi kumpa sifa isiyositahiri Nyerere wala huwezi kumkosea adabu kwa kiasi anachokisema Pasco, lakini mtu akikaa akasoma mabandiko yako kwa utulivu na akili iliyowazi (open mind), atakuelewa kabisa mlengo wa maandishi yako. Mimi sina tatizo na maandishi yako kwa sababu kwanza kabisa najitambua na natumbua mnachokidai tangu siku nyingi sana. Pasco anasema maandishi yako yamejaa udini na kumdharau Nyerere kwa sababu mbili tu :kwanza, mihadhara mingi na hii historia unalotaka tuiamini kuwa ndo ya kweli inafanyika kwa asilimia kubwa misikitini (na wewe ni shahidi). Je, kizazi chenye uhalali wa kufahamu historia sahihi ya kupigania uhuru wa Tanganyika ni waislam pekee!? Pili :makongamano yenu mengi yanawalenga vijana wa kiislam na huko ndo mnaanza kuelezea negativite kuhusu Nyerere na uhuru wa Tanganyika, Je, hao wengine walioshiriki Jamii isiyokuwa ya Kiislam hawana haki ya kufahamu mchango wao!? Au kuelezea hiyo historia ya "kweli" kwa wengine mtakosa thawabu!? Kitu kingine unachotakiwa kusema kwa ukweli ambao naamini unakuuma kuusema na ndio maana hutaki kuusema ni kwamba NYERERE HAKUJIPELEKA TAA! ALITWA NA ALIOMBWA NA HAO WAZEE WALIOKUWA WANAFANYA HIZO HARAKATI ZA KUTAKA UHURU. SASA TWAMBIE, NI KOCHA GANI DUNIANI ANANUNUA MCHEZAJI ASIYEKUWA NA UWEZO WA ZIADA!? mchango mkubwa wa Nyerere upo, utaendelea kuwepo na wala hautaweza kuufuta kwani hata hao waliomuita hawakumbeza kama unavyojaribu kufanya wewe! Ingekuwa unachosema kina Afya katika Jamii usingekisemea kwenye majumba ya ibada na wanafamilia wa majumba hayo huku ukifahamu kabisa hao ni sehemu ndogo sana ya wanafamilia wanaohitaji kufahamu hao wapigania uhuru wengine na michango yao. Sio dhambi kwani sote tunafahamu uhuru haukupiganiwa na mtu mmoja, lakini hao wengine walikuwa na kiongozi wao! Na mwisho wa siku katika kikosi ukubali ukatae KIONGOZI ndio anayebeba kombe juu! Stop negativite towards Nyerere, be free to appreciate his work!
Maalim sheikh wngu alhaji Mohamed Said hapo ndio unapo nikosha nafsi yngu pasco baada kutafuta Elimu toka kwako naona anaropoka kwa vitu asivyo vijua kikubwa usichoke kumpa Elimu ila hakika ujinga wake umma wote tumeuona hakika mungu akulinde akupe umri mrefu ili tuendelee kupata Elimu toka kwakoPasco,
Unataka kupiga ala bila kujifunza chromatics.
Unataka kuizungumza historia ya Zanzibar bila kusoma historia yenyewe.
Lakini kubwa ni kuwa hata ''intellect,'' yako ni tatizo kidogo maana hata
mtu akikusoma hili linamtokea dhahiri kabisa.
Ataliona jinsi michango yako inavyokosa mantiki na matokeo yake ni haya
ya kuchanganya mambo.
Unachokijua wewe ni, ''mapinduzi matukufu,'' huna kingine.
Nikikuwekea mabandiko ya kukufikirisha unapotea kwa muda kisha unaibuka
na jambo lingine kabisa lile unalikimbia.
Ni kweli waliofungwa jela za Bara walinusurika kuuawa.
Lakini iweje umshukuru mtu aliyekukata mkono kwa kukurudishia kidole gumba?
Jana nilikuwa Zanzibar kutoa mada kuhusu Sheikh Hassan bin Amir.
Walionialika ni Mwinyi Baraka Foundation.
![]()
Kongamano la Mwinyi Baraka Foundation 12 June 2016 Ukumbi wa Baytul Amiyn
Sheikh Hassan bin Amir ni Mzanzibari na alishiriki katika kuunda TANU na ni
mmoja wa wajumbe wa TAA Political Sub Committee 1950 wajunbe wengine
wakiwa, Dr. Kyaruzi, Abdul Sykes, Stephen Mhando, Hamza Mwapachu,
Said Chaurembo na John Rupia.
Sheikh Hassan bin Amir ndiyo aliyiongoza TANU kuwa ''a nationalist secularist
party,'' baada ya kufanya mkutano wa siri Mtaa wa Pemba Dar es Salaam na
baadhi ya viongozi wa TANU mwaka wa 1955 wakiwamo Rajab Diwani, Sheikh
Abdallah Chaurembo, Sheikh Nurdin Hussein na wengineo.
Sheikh Hassan bin Amir alikuwa Mufti wa Tanganyika hadi alipofukuzwa na
Nyerere mwaka wa 1968 na kurudishwa Zanzibar na kupigwa marufuku
kukanyagaTanganyika baada ya ''mgogoro,'' wa East African Muslim Welfare
Society (EAMWS) uliopelekea kuundwa BAKWATA.
Lakini baada ya Sheikh Hassan kufariki mwaka wa 1979 Nyerere alihudhuria
hitma yake Msikiti wa Mtoro alialikwa na Sheikh Abdallah Chaurembo na
Sheikh Kassim Juma.
Mimi nilikuwapo hapo msiktini siku hiyo.
Ikiwa huyajui haya kwa undani maisha utahangaika na historia ya Tanganyika
kwani huu ndiyo msingi unaosimamisha si historia ya Nyerere bali historia nzima
ya uhuru wa Tanganyika na baada yake.
Pasco,
Hebu jitulize na isome historia kwanza kabla hujataka kupambana na mimi.
Watoto wa mjini wana Kiswahili chao.
Wanasema, ''Mimi si saizi yako.''
Maana ukinivaa utapwaya.
Lete ushahidi kuna kitabu kimeandika na maalim sheikh wngu alhaji Mohamed Said maisha na nyakati za abdulwahid sykes sina hakika km hicho kitabu kinauzwa misikitini tu km unavyotaka tuamini kuna kitabu kingine pia uamuzi wa ubasara wa tabora sina hakika na wala hamna ushahidi km kinauzwa misikitini tu km unavyotaka tuamini lete ushahidi wapi na lini mohamed said amemtukana au kumkashifu mwl nyerere kikubwa mnataka pia mwl apewe pia sifa zisizokuwa zake itakuwa ngumu hyo vitabu hvyo vinapatikana dukani ilala na wateja wngu ni dini zote na makabila yoteMzee Mohammed Said, umesema huwezi kumpa sifa isiyositahiri Nyerere wala huwezi kumkosea adabu kwa kiasi anachokisema Pasco, lakini mtu akikaa akasoma mabandiko yako kwa utulivu na akili iliyowazi (open mind), atakuelewa kabisa mlengo wa maandishi yako. Mimi sina tatizo na maandishi yako kwa sababu kwanza kabisa najitambua na natumbua mnachokidai tangu siku nyingi sana. Pasco anasema maandishi yako yamejaa udini na kumdharau Nyerere kwa sababu mbili tu :kwanza, mihadhara mingi na hii historia unalotaka tuiamini kuwa ndo ya kweli inafanyika kwa asilimia kubwa misikitini (na wewe ni shahidi). Je, kizazi chenye uhalali wa kufahamu historia sahihi ya kupigania uhuru wa Tanganyika ni waislam pekee!? Pili :makongamano yenu mengi yanawalenga vijana wa kiislam na huko ndo mnaanza kuelezea negativite kuhusu Nyerere na uhuru wa Tanganyika, Je, hao wengine walioshiriki Jamii isiyokuwa ya Kiislam hawana haki ya kufahamu mchango wao!? Au kuelezea hiyo historia ya "kweli" kwa wengine mtakosa thawabu!? Kitu kingine unachotakiwa kusema kwa ukweli ambao naamini unakuuma kuusema na ndio maana hutaki kuusema ni kwamba NYERERE HAKUJIPELEKA TAA! ALITWA NA ALIOMBWA NA HAO WAZEE WALIOKUWA WANAFANYA HIZO HARAKATI ZA KUTAKA UHURU. SASA TWAMBIE, NI KOCHA GANI DUNIANI ANANUNUA MCHEZAJI ASIYEKUWA NA UWEZO WA ZIADA!? mchango mkubwa wa Nyerere upo, utaendelea kuwepo na wala hautaweza kuufuta kwani hata hao waliomuita hawakumbeza kama unavyojaribu kufanya wewe! Ingekuwa unachosema kina Afya katika Jamii usingekisemea kwenye majumba ya ibada na wanafamilia wa majumba hayo huku ukifahamu kabisa hao ni sehemu ndogo sana ya wanafamilia wanaohitaji kufahamu hao wapigania uhuru wengine na michango yao. Sio dhambi kwani sote tunafahamu uhuru haukupiganiwa na mtu mmoja, lakini hao wengine walikuwa na kiongozi wao! Na mwisho wa siku katika kikosi ukubali ukatae KIONGOZI ndio anayebeba kombe juu! Stop negativite towards Nyerere, be free to appreciate his work!
Lete ushahidi kuna kitabu kimeandika na maalim sheikh wngu alhaji Mohamed Said maisha na nyakati za abdulwahid sykes sina hakika km hicho kitabu kinauzwa misikitini tu km unavyotaka tuamini kuna kitabu kingine pia uamuzi wa ubasara wa tabora sina hakika na wala hamna ushahidi km kinauzwa misikitini tu km unavyotaka tuamini lete ushahidi wapi na lini mohamed said amemtukana au kumkashifu mwl nyerere kikubwa mnataka pia mwl apewe pia sifa zisizokuwa zake itakuwa ngumu hyo vitabu hvyo vinapatikana dukani ilala na wateja wngu ni dini zote na makabila yote![]()
![]()
![]()
![]()
Rubawa,
Kuuza vitabu msikitini sidhani kama ni tatizo.
Kanisa Katoliki linauza vitabu kanisani pale Cathedral Bookshop
kwa miaka mingi sana.
...hahahaha kwanza tutajuaje mama daisy ndio yupi hapo?hilo baibui alilovaa bi mwamvua(mama daisy) liko wapi hapo pichani?
"anasema hapo hapo akachukua baibui lake na kuelekea mkutanoni"
Uncle...Na pia mueleze kuwa mimi sijasema kuhusu kuuza vitabu vyako, nimeongelea mihadhara, makongamano na hutuba nyingi zinazoelezea harakati za uhuru wa Tanganyika inayofanywa na mashehe wanaodhani wanaelewe sana kilichotokea hufanyika misikitini na /au makongamano yanayohusiana na waislam. Hicho ndo nilichosema, uuzwaji wa vitabu hutegemea sana na uhitaji na uwepo wawateja katika eneo husika Sina jambo na hilo Rubawa
Mtu Chake,...hahahaha kwanza tutajuaje mama daisy ndio yupi hapo?
Kitulo,Hiyo picha inaonyesha huo ukoo wa kina Sykes ulikuwa na fedha sana mwaka 1942 Ally amevaa suti na tai!
Na ni watunzaji wazuri wa nyaraka na picha.
Nlikuwa sijui kwamba ujerumani, USA, IRAN NK kote uko sheikh mohamed said alikokuwa anaitwa na kualikwa kumbe ilikuwa mihadhara ya misikitini hama kweli nmeamini mmejaa chuki na fitina za ajabu bila sababu na Alhaji Mohamed Said muwe mnajaribu kumsoma vzuri kwanza sio kila kitu muwe mnatanguliza chuki tuNa pia mueleze kuwa mimi sijasema kuhusu kuuza vitabu vyako, nimeongelea mihadhara, makongamano na hutuba nyingi zinazoelezea harakati za uhuru wa Tanganyika inayofanywa na mashehe wanaodhani wanaelewe sana kilichotokea hufanyika misikitini na /au makongamano yanayohusiana na waislam. Hicho ndo nilichosema, uuzwaji wa vitabu hutegemea sana na uhitaji na uwepo wawateja katika eneo husika Sina jambo na hilo Rubawa
Ngova,Hii kitu imeenda shule