Huwa mnatuhumu ufisadi wake bila kuthibitisha.
Makamba naye anagawa majiko, mbona watu hawampendi kama Magufuli?
Magufuli aliwapenda wanyonge na kuwatendea haki: wakulima, mama nitilie, machinga, bodaboda na Watanzania tunaoipenda nchi yetu hutuambii chochote kumhusu Jemedari tukakuelewa.
Alijenga miundombinu ya hii nchi kuliko Mtanzanzania yeyote kuwahi kutokea. Akaleta nidhamu na uwajibikaji. Akaanzisha miradi mingi ya Kimkakati, n.k.
Nyie vyeti feki, wauza madawa ya kulevya, mafisadi, vibaraka wa mabeberu na walamba asali wote endeleeni tu kufurahia awamu yenu hii, kutesa kwa zamu.
Ila mnaujua ukweli - Magufuli alikuwa mzalendo wa kwelikweli, hilo halina ubishi.