Hapa jirani yangu pana nyumba haijawahi kukaliwa na watu tokea ikamilike kujengwa. Ni mwaka wa 10 huu, mpaka geti linaanza kuoza. Nijitwalie?

Hapa jirani yangu pana nyumba haijawahi kukaliwa na watu tokea ikamilike kujengwa. Ni mwaka wa 10 huu, mpaka geti linaanza kuoza. Nijitwalie?

kuna ndugu yangu alikiwa mfanyabiashara mkubwa wa mazao, kuna mkoa alienda katika shughuli zake sehemu ya faida alinunua kiwanja ambacho kilikuwa na msingi teyari.

Kwa bahati mbaya makabidhiano ya nyaraka muhimu hayakukamilika ila kwakuwa alikuwa na uhakika akawa amefuata mzigo mwingine.

Aliporudi mkoai ilipo familia yake akawapa hiyo taarifa kuwa kuna kiwanja kanunua mkoa fulani wilaya flani na jinsi kilivyo,

Wakati anajipanga ili kupeleka mzigo tena kwenye ule mkoa akapatwa na maradhi na hayakumchukua siku nyingi akawa amefariki na story ya hicho kiwanja ikaisha kwa namna hiyo.
Duuh! Wewe unanitia nguvu kwamba nijitwalie hii nyumba
 
Mimi Nina nyumba miaka 5 sijawahi kwenda na ilikamilika haishi mtu yeyote!

Kwanini hujafikiria kuwa Mwenye nyumba yupo nje ya inchi? Umefikiria kuwa kafariki au yupo jela?
Umewajengea majini waishi humo?

Nyumba yoyote iliyotelekezwa huwa ni nyumba ya majini na siku ukijichanganya kwenda kuingia katika makazi hayo jua utakutana na visanga mpaka utatamani kukimbia. Hata nyumba tunashauriwa tusijenge ya vyumba vingi ambavyo havitakuwa na matumizi matokeo yake huwa unakaribisha majini yaishi humo
 
Kuna nadharia mbili hapa.

1. Yawezekana mmiliki alikuwa anamjengea mchepuko. Ili siku moja aje amfanyie surprise. Lkn kabla ya surprise jamaa akapata ugonjwa ama ajali na kufariki. Kwahiyo si mchepuko wala familia waijuao nyumba hii.

2. Mmiliki alipoikamilisha alipiga kifungo cha miaka 30 au zaidi jela.

Je, nijitwale hii nyumba? Vipi kama nadhria ya 2 ndiyo sahihi? Akitoka jela na kurudi uraiani itakuwaje? Ingawa kuna usemi wa kiswahili unanipa moyo "cha kuokota siyo cha kuiba, mwenye mali mpumbavu".
Kwa hiyo siku hizi tumeanza kuokota hadi nyumba?Saaafiiii!Si muda naamini tutaanza kuokota magari na vichwa vya treni upya.InshaAllah!🙏
 
Akili za vijana wa sasa wapenda kitonga...

Tafuta Hela kijana...
Mkuu hizi ni zama za kula kiulaini mfano kubet, kudanga, umarioo, nk. Habari kuchanganya zege utoke jasho haipo tena. Mashine za kuchanganya zege zitafanya kazi gani? Matrekta ya kylimia na combine harvester zitanya kazi gani?

Smart work pays hard work kills.
 
Sheria ya Ardhi inatambua umiliki wa 'adverse'.

Iwapo unaitwaa nyumba/ardhi na kuitawala kwa miaka 12 bila kuhojiwa na mwenye mali na bila ruhusa yake, basi inadhaniwa kwamba nyumba ni kwako.

Na baada ya hiyo miaka 12 kupita, halafu akaja mtu kudai inabidi atoe uthibitisho kwamba ni yake.
 
Kuna jamaa aliokota nyumba.

Kuna kampuni ilikua ya ufugaji kwa msaada wa watu wa nje,badae shirika likafa,

Nyumba zilikua pembeni kidogo ya kijiji,zile nyumba kikapewa kijiji kiamue matumizi,

Ila kuna sehem walikua wanaoshea mifugo yao ni mbali kidogo na kijijini,kijiji kama cha nne hivi lakini zamana hapo ilo eneo lilikua mbali na kijiji.

Hivyo nyumba hiyo ilibaki tupu bila mtu,bahati nzuri mwaka 2006 ikajengwa shule ya kata karibu na eneo ilo,hivyo pakaanza kuwa na mahitaji.

Mwanzoni kuna kichaa alikua anakaa humo,wale machizi fresh yani sio kichaa jumla jumla,amekaa umo kwa muda kiasi akaondoka.

Kuna jamaa akaona isiwe tabu,akapasafisha,akaanza kuishi humo,badae kapiga rangi karekebisha mlimo bomoka ,basi maisha yanasonga.

Tokea 2007 mpaka saizi anaishi hiyo nyumba,historia hiyo alitupa yeye mwenyewe wakati wa sensa.

Na watu wengi wapya ilo eneo wanajua ni kwake na wenyeji wanahisi amenunua au kuna hatua alichukua
 
Sheria ya Ardhi inatambua umiliki wa 'adverse'.

Iwapo unaitwaa nyumba/ardhi na kuitawala kwa miaka 12 bila kuhojiwa na mwenye mali na bila ruhusa yake, basi inadhaniwa kwamba nyumba ni kwako.

Na baada ya hiyo miaka 12 kupita, halafu akaja mtu kudai inabidi atoe uthibitisho kwamba ni yake.
Wow! Sijui kesho niamkie ofisi za ardhi??
 
Wow! Sijui kesho niamkie ofisi za ardhi??
Sasa hapo utaharibu.

Ukienda huko maana yake unakubali kwamba hiyo nyumba ina mwenyewe na sasa unaenda kumuulizia. Yaani hujiamini.

Ipo hivi, ingia ama weka kijana, fyeka majani, deki fanya usafi.

NB: Kama ina milango usiivunje
 
Muwe mnawapa ndugu taarifa au mke au mme taarifa kwamba nina nyumba sehemu, wanaume wengi wanaogopa kugawana mirathi na mke unakuta anajenga ghorofa au nyumba ya kifahari kimya kimya, liktokea tatizo ghafla ukafariki watu baki warithi nyumba yako, watoto wanateseka.
 
Back
Top Bottom