Hapa jirani yangu pana nyumba haijawahi kukaliwa na watu tokea ikamilike kujengwa. Ni mwaka wa 10 huu, mpaka geti linaanza kuoza. Nijitwalie?

Hapa jirani yangu pana nyumba haijawahi kukaliwa na watu tokea ikamilike kujengwa. Ni mwaka wa 10 huu, mpaka geti linaanza kuoza. Nijitwalie?

Kuna nadharia mbili hapa.

1. Yawezekana mmiliki alikuwa anamjengea mchepuko. Ili siku moja aje amfanyie surprise. Lkn kabla ya surprise jamaa akapata ugonjwa ama ajali na kufariki. Kwahiyo si mchepuko wala familia waijuao nyumba hii.

2. Mmiliki alipoikamilisha alipigwa kifungo cha miaka 30 au zaidi jela.

Je, nijitwale hii nyumba? Vipi kama nadharia ya 2 ndiyo sahihi? Akitoka jela na kurudi uraiani itakuwaje? Ingawa kuna usemi wa kiswahili unanipa moyo "cha kuokota siyo cha kuiba, mwenye mali mpumbavu".
Ingia tu mkuu utolewe bikra na viumbe visivyoonekana.

Utapigwa katerero kila siku bila kumuona anayefanya hivyo ndio utajuwa dunia ni nzito.
 
Mwaka 2009 tulienda na rafiki yangu Bunju kununua Viwanja,tukaanza kujenga mdogomdogo lakini rafiki yangu (RIP)alijenga fasta ikabaki kupaua tu(kumbuka wote tulikuwa mabachela). Siku moja anatoka site akapata ajali Tegeta(aligongana na Lori),alifariki palepale. Huyu rafiki yangu tulikuwa tumepanga nyumba moja Sinza(yeye Chumba chake,mimi changu lakini sebule,jiko nk tunashea. Tangu tunanunua Viwanja mpaka anafariki hakuna aliyewahi kumpeleka site ndugu,rafiki wala jamaa. Hivyo nyumba niliiokota kwa style hiyo,niliipaua,nikaifanyia finishing na sasa nakula Kodi. Lakini kwa kuwa tulikuwa tumeshibana sana hivyo huwa najitajidi kuwatumia Pesa Wazazi wake Moshi kila mwezi,na wamekuwa kama Wazazi wangu na wananiita mwanao.
SWALI KWA NINI SIKUIPA TAARIFA FAMILIA HIYO?huyu Marehemu rafiki yangu ndie aliyekuwa amesoma kwao,Kaka na Dada zake wote ni wale waleviwalevi waliojichokea tu,hivyo kama ningetoa taarifa naamini wangeshauri nyumba iuzwe tu wapate Pesa ya kunywea pombe. Tangu niikamilishe mwaka 2011 mpaka leo nakula Kodi tu,Hati nilishaipata kwa jina langu na maisha yanasonga.
Ulimuua rafiki yako
 
Kuna nadharia mbili hapa.

1. Yawezekana mmiliki alikuwa anamjengea mchepuko. Ili siku moja aje amfanyie surprise. Lkn kabla ya surprise jamaa akapata ugonjwa ama ajali na kufariki. Kwahiyo si mchepuko wala familia waijuao nyumba hii.

2. Mmiliki alipoikamilisha alipigwa kifungo cha miaka 30 au zaidi jela.

Je, nijitwale hii nyumba? Vipi kama nadharia ya 2 ndiyo sahihi? Akitoka jela na kurudi uraiani itakuwaje? Ingawa kuna usemi wa kiswahili unanipa moyo "cha kuokota siyo cha kuiba, mwenye mali mpumbavu".
Humo wanaishi majini.

Ameitoa hiyo kama zawadi
.
 
Ushauri wangu,mtafute ndugu yako wa mbali mpange ajifanye kuja hapo kama hiyo nyumba ni yake then akuone jirani mtafute watu waifanyie usafi na ukarabati.
 
Back
Top Bottom