Hapa ndio ninapokuwa na walakini na uwepo wa Mungu

Unaweza ukawa unaabudu vinyago huko uliko afu ukasema huna dhambi.

Mungu anawapenda watu wake wasimema nae mda wote na ukishinda hapo ulipo utafurahi sana. Soma kisa cha Ayubu. Na uzuri mambo yote yameandikwa ili kujua Mungu anatuwazia nini. Soma Hana, Soma Ibrahim na Sarah,
 
Kwamba huna dhambi basi wewe utakuwa unakula ubwabwa na kuku kila siku pasipo changamoto ya maisha? Sasa utamjuaje Mungu pasipo changamoto.?
 
Basi wewe shikilia kuwa Mungu hayupo ila huku kwenye sifa za Mungu achanako maana hatuwezi kuelewa kwa sababu unahoji uhalisia wa sifa za kitu ambacho unadai hakipo.

Sifa hazipingani na uhalisia bali wewe unaleta lawama kwa Mungu kwa kutofanya kitu ambacho hakuahidi kufanya. Msingi wa hoja yako ndio hauna uhalisia. Maana huo upendo na uwezo wa Mungu hautokuwa na kikomo kwenye nini anatakiwa kufanya na kutofanya, atakuja mwengine atasema kwanini asifanye watu wote tukawa mabilionea kusiwepo masikini kama Mungu ana uwezo? Mwengine atasema kama Mungu ana uwezo kwanini asizuie tusiwe wazee tubaki vijana tu? Mwengine atasema kwanini hajafanya tukaishi huko mbinguni?
 
Hakuna hizo hoja kabisa.
Hivyo visa vingi ni vipi?
Hakuna Mungu huu ndio ukweli.
Visa kuanzia huko ulikotoa kisa cha shetani kukosea na kutosamehewa kuna visa vingi vilivyoeleza upendo wa Mungu na kusamehe kwa Mungu, na hata maisha halisi ya sasa yanaonyesha upendo wa Mungu.

Kusema hakuna Mungu huo ni mtazamo wako usiseme huo ndio ukweli, ndio maana tuna Agnostics ambao hawaamini Mungu pia ila hawadai hakuna Mungu kama usemavyo wewe, lakini pia kama ingekuwa madai ya kuwa hakuna Mungu ndio ukweli usio na shaka basi isingekuwa inatokea tunaona atheists wengine wanaachana na huo ukweli na kuja kuwa waamini Mungu.
 
Mimi sitaki isiwe imani.

Kuwa na imani na kuamini ni haki yako ya kikatiba kabisa. Unaweza kuchagua kuamini chochote utakacho hata mawe, miti, mapango, majabali n.k

Lakini ukianza kudai kwamba imani yako ina ukweli lazima uthibitishe hilo.
Ulazima wa kuthibitisha unatoka wapi? Ina maana nikisema imani yangu ni ukweli ninavunja sheria? Au ninakuwa namkosea mtu mwengine kusema imani yangu ni ukweli?

Ina maana tafsiri ya imani ni uongo?
 
Hayo mashaka juu ya Mungu ndo dhambi kubwa uliyonayo. Tubu na uondoe mashaka juu ya mwenyezi Mungu.
 
Ulazima wa kuthibitisha unatoka wapi? Ina maana nikisema imani yangu ni ukweli ninavunja sheria?
Huvunji sheria.

Ukijisemea tu wewe mwenyewe haina shida.

Ila ukianza kuuaminisha uma kuhusu imani yako bila uthibitisho. Huko ni kusambaza taarifa za uongo.
Au ninakuwa namkosea mtu mwengine kusema imani yangu ni ukweli?
Humkosei mtu kumwambia kuhusu imani yako.

Ila ukianza kumfosi mtu akubaliane na imani yako bila uthibitisho na ukweli hapo ndio kuna makosa.
Ina maana tafsiri ya imani ni uongo?
Msingi wa imani ni kutokuwa na uhakika wala uthibitisho

Imani bila uthibitisho ni uongo ndio.
 
Kwanza mimi sihitaji ninyi binadamu muhangaike kumuelezea na kumtetea huyo Mungu aonekane yupo.

Huyo Mungu kama yupo, Ajitokeze hadharani mwenyewe ajidhihirishe yupo yeye mwenyewe.

Uongo ndio huwa unahangaikiwa sana uonekane ni ukweli.

Kumbe ni uongo.

Vivyo hivyo, Huyo Mungu kama yupo aje mwenyewe ajidhihirishe.
 




Huyu ndugu yetu ana shida

 
Hayo mashaka juu ya Mungu ndo dhambi kubwa uliyonayo. Tubu na uondoe mashaka juu ya mwenyezi Mungu.
Huyo Mungu, Kwa nini aliumba binadamu wenye mashaka juu ya uwepo wake?

Huyo Mungu, Alishindwaje kuumba binadamu wasio na mashaka kuhusu uwepo wake?
 
Lete
Lete ushahidi usio na shaka kuhusu uwepo wake.

Kwa hiyo akiamini nyonzo ndio shonvi naye autambue kuwa ukweli?

Ukweli hakuna Mungu hapa duniani.
 
Kama ni hivyo mbona hatuoni duniani dini kuzuiliwa kwa sababu zinaeneza mafundisho yao ya imani waziwazi kwa watu ambao unasema ni kusambaza uongo? Hebu elezea nielewe.

Huko kumfosi mtu kukubali imani ndio kunafanyikaje hebu toa mifano wewe ushawahi kufosiwa kukubali imani bila kinyume na ridhaa yake au umeona humu JF watu wakifosiwa kukubali imani fulani?

Unasema msingi wa imani ni kutokuwa na uhakika na uthibitisho halafu hapo hapo unasema imani hiyo hiyo isipokuwa na uthibitisho ni uongo, hivi kweli hata wewe umeelewa kweli mkuu?
Yani msingi wa imani ni kutokuwa na uthibitisho ila hapo hapo unataka kuonyesha kuwa kuna imani zenye uthibitisho na ambazo zimekosa uthibitisho, kwa kweli ni ngumu kuelewa hapo.
 
Unaposema Huna dhambi tiyari unaamini mungu yupo. Mkuu mi nahisi hizo nichangamoto tu.jrbu kutafakali upya maisha yako kuna manmna tu.
 
Kama ni hivyo basi usingekuwa unajiingiza kwenye mabishano ya kuhusu Mungu, maana ni sawa na kukuta watu wanajadili tuhuma za Kikwete kumfunga Babu Seya kwa sababu za wivu wa mapenzi halafu ukajiingiza katika hayo majadiliano mwenyewe kisha unasema kwanini watu wamtetee Kikwete na sio Kikwete ajitokeze ajitete mwenyewe tuhuma zake.
 
...Hujaeleza Kipi kinachokufanya Ukwazike ! Ni vigumu kupata Msaada wakati wewe hujakuwa Muwazi !
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…