Harmonize ni mbumbumbu wa sheria, mchanga wa mahusiano na mshamba bado wa umaarufu

Harmonize ni mbumbumbu wa sheria, mchanga wa mahusiano na mshamba bado wa umaarufu

Ndugu Mshana Jr, kwa heshima uliyo nayo hapa JF, kweli ulikua na haja yoyote kuleta hayo mambo ya hovyo hapa?
Lugha kama hizo na jumbe(sijui uwingi wa ujumbe) kama hizo ni mara ya kwanza kuziona?
Sidhan kama ulikua na haja ya kuleta hizo propaganda hapa, ulitakiwa uwe neutral,lakini andiko lako lina biasness, kuonesha kuna upande unaushabikia!
Kimsingi kama ushamba hakuna asiye mshamba na kama kutojua sheria, hakuna aliye mkamilifu, inategemea sheria umeichukuliaje kuifasiri na ukaeleweka kwa wasimamia sheria, nje ya hapo kila mtu ni layman kwenye sheria.

Dogo kaachia hii:

CHAZA una hakika umesoma na kuelewa kweli nilichoandika? Au mahaba ndio yamekuongoza kujibu ? Unasema nisiwe bias kivipi? Sikuongelea wasanii in general bali mtu mmoja ambapo kwa nilichoandika kitakufaa hata wewe! Sikukurupa kuandika hii mada .. Hebu soma comment ya Viol hapa[emoji1541][emoji1541][emoji1541]

Kuna wazee mtaani kwetu walitukanana kesi zikaanza imedumu miaka 14 ,kila mtu anaonyesha umwamba wa hela ,iliwafilisi Hadi wakaanza kuuza mashamba hamna anayekubali ni mwendo wa kukata rufaa ,mwisho wa siku wakakaa chini wenyewe wamalize kimila na ikaisha wakiwa wameshafilisika
 
Kitu kimoja kuhusu pesa nyingi: Hufunua undani wa mtu katika uhalisia wake....!!! Hata wewe ukizipata leo tutakujua tuu.. Waswahel wanasema pata pesa tujue tabia yako....

Shule ni muhimu sana sana kile kitendo cha kukaa darasani miaka kibao hutufunza mengi hata tusipofaulu mitihani..japo baadhi hawaelimiki hata wafike mpaka chuo kikuu.

Kuna wachache waliobahatika kuwa na akili na maarifa ya kuzaliwa nayo... Hawa ndio ambao huelimika bila hata ya kusoma sana
Ni wepesi kushika vitu vipya
Ni wepesi kuwa wabunifu
Ni wepesi kubadilika kuendana na mazingira yaliyopo nknk

Harmonize kiasili shule hamna na hii si dhambi hata kidogo bali ni mfano wa mamilioni ya watoto wetu waliokosa shule kwa sababu mbalimbali... Mazingira ya umasikini, ndugu wazazi na hata jamii vimezima ndoto za vijana wetu wengi kielimu.

Kuna wale wachache ambao automatically walijiona kabisa kuwa shule sio sehemu yao, hao walijiona kabisa vipaji na vipawa vyao viko kwenye sanaa mbalimbali, biashara nk

Harmonize ni nmojawapo aliyekosa elimu kwa sababu zozote zile na kuja kuibukia kwenye sanaa ya mziki.. Na amefanya vema kwakweli mpaka hapo alipofikia.. Kutompongeza kwa hili ni wivu.

Katika njia yake ya kutafuta mafanikio zaidi amejikuta anakabiliwa na changamoto kadhaa ... Ambapo anahitaji timu makini, somi na yenye weledi kuweza kumvusha.

Mahusiano
Kwa umri wake na pesa kiasi aliyonayo, haya anayofanya sasa wala si ajabu sana..hata wewe ungefanya na pengine zaidi... Lakini Harmonize kwenye future ya carrier yake ya mziki anahitajika kuwa na washauri weledi zaidi.

Inajulikana wazi hawa mabinti vibibi wa bongo movie walivyo makaburi ya pesa na matajiri wa skendo... Hawa wapo tangu enzi za mapapaa kina Msofe, wazee wa bandari, wauza unga, watoto wa mjini nknk.. Leo hii ndio aje kudate nao na kurusha picha za mahaba mazito mitandaoni!? Haya ni majambazi ya cash..na yakishakuchuna na kukuchoka yanakutengenezea skendo kisha yanakupiga chini.

Sheria
Kwa maisha anayoishi Harmo ya mziki, ya mitandaoni ya competition kwenye game, ya kupokonyana madanga ya mjini ya kuoneshana umwamba nk.. Kuna vitu haviepukiki hata atafanyeje navyo ni kuundiwa kashfa hata za uongo..kama naye alivyofanya kwa wengine.. Aishi kibon touni, akipatwa hapa naye anatafuta pa kumpata mtu wahuni ndivyo wanavyomalizana.

Ishu ya kutishia kuwapeleka watu aliowataja kwa majina kuwa atawapeleka mahakamani awafunge na wamlipe mabilioni ya pesa ni upuuzi mtupu na hao wanasheria wake wanamlia pesa tu
Kesi za fidia kama hizo huwa na mambo mengi mno mpaka watu hukata tamaa.

Mbaya zaidi keshaanza vibaya kwa kuwataja watuhumiwa wake kwa majina na kuwahukumu tayari huku akitambua wazi kuwa mahakama pekee ndio yenye uwezo wa kuhukumu.. Mambo ya sheria ni nyoko sana keshaitia doa kesi yake.

Kwa kinachoonekana wito ama tisho la wakili wake hakuna mahali anamtaja Harmonize kwa majina yake rasmi..hapa tayari napo kuna shida.

Natambua katishia kuwa wahusika itakuwa mwisho kuonekana kwenye page zao mitandaoni...Mmh Instagram na FB kwa mfano ina mitifuano mingapi kila siku duniani, tena mibaya kabisa mpaka ikimbilie kufunga account za wambea njuka?

Ushamba wa umaarufu
Bado Harmonize ana kitete kile cha ufukara, bado hajiamini lakini mbaya zaidi ana management ambayo haiko vizuri sana au haisilizi au haimshauri vema au haina weledi na exposure ya kutosha. Kusema kwamba jina lake kalijenga kwa mabilioni ni fix za kishamba sana.

Kuona kwamba kafanyiwa figisu na wabaya wake nalo ni ushamba pia.. Kwa hapo alipo anategemea kweli akose maadui kila kona?

Ajaribu kuwapuuza aone! Ishu za kupelekana mahakamani kudaiana fidia zitamuongezea stress za kufa mtu...kuna kesi maelfu za fidia zina umri sawa na wake.. Hazijalipwa!

Na je kesi zake hizo ni jinai au ni madai?
😲😲😲 Ulipata connection 😲😲😲
 
Michael Jackson alisoma wapi..kipaji hakihitaji shule wasomi wakina Ndege wangekula wapi...
Natambua uwezo mdogo wa wengi wetu wa kuchambua mambo hivyo inanibidi kila wakati nitoe ufafanuzi.. Na wengi kati yetu huwa hatusomi mpaka mwisho bali hukurupuka ku comment..ungekuwa umesoma hij para wala usingekurupuka kujibu ulichoandika[emoji1541][emoji1541][emoji1541]

Harmonize ni nmojawapo aliyekosa elimu kwa sababu zozote zile na kuja kuibukia kwenye sanaa ya mziki.. Na amefanya vema kwakweli mpaka hapo alipofikia.. Kutompongeza kwa hili ni wivu.

Katika njia yake ya kutafuta mafanikio zaidi amejikuta anakabiliwa na changamoto kadhaa ... Ambapo anahitaji timu makini, somi na yenye weledi kuweza kumvusha.
 
Kuna wazee mtaani kwetu walitukanana kesi zikaanza imedumu miaka 14 ,kila mtu anaonyesha umwamba wa hela ,iliwafilisi Hadi wakaanza kuuza mashamba hamna anayekubali ni mwendo wa kukata rufaa ,mwisho wa siku wakakaa chini wenyewe wamalize kimila na ikaisha wakiwa wameshafilisika
Mwanasheria mkweli na mwaminifu kamwe hakushauri ukimbilie mahakamani kama hakuna sababu nzito na za msingi...mahakamani kuna upotevu mkubwa wa vitu viwili PESA na MUDA.. Kesi inaweza kuendeshwa mwaka mzima minimal time ukashinda lakini mshtakiwa wako akakata rufaa kwa sababu ndogo sana, anaeza kusema procedure zilikosewa.. Baasi..kesi inaanza upya!
 
Mara ya kwanza akakubali kuwa yule ni yeye baada ya kuona ni sifa kuonyesha maumbile yake, akaambatanisha caption [emoji2420]?? [emoji1646]?? Ila baada ya kusanuliwa kuwa huo ni ujinga na itaathiri brand yake, anarudi nyuma na kusema si mimi, wameniunganishia picha coz alishajua kwa kukiri yule ndiye, angeanza kuhukumiwa yeye kwa kurekodi na kutuma picha hizo.

Huyu jamaa shida yake ni mikurupuko na hana management inayojielewa.
 
Keshaharibu kesi tayari na hili linaweza kutumika kama ushahidi...shida ya maandishi ni kwamba hayafutiki
 
Afadhali umeliona hilo, ujue kuna miaka hapo tulikua kwenye tuzo tunakimbizana na Nigeria hata nomination, baada ya kuanza ujinga Nigeria wako mbali mno, South wametakeover na amapiano yao, wasipokaziwa hawa mbumbumbu wanaua Bongofleva iliyojengwa kwa jasho na damu, Machozi, jasho na damu
si sapoti ujinga wao, ila swala la kusema mziki unakufa kwa kiki hapana kabisa, Kama tuzo zishaletwa nyingi tu na mtu fulani still bado appreciation hakuna zaidi ya kumkatisha tamaa. Hivi unakijua kitu kilichojengwa kwa jasho na damu wewe?
 
Taratibu tunaanza kuipa kisogo bongofleva mara nyingi nikiwa peke yangu huwa nasikiliza muziki kusaka usingizi na miaka 2 nyuma nilikuwa nasikiliza bongofleva siku za hivi karibuni nasikiliza waganda, wanaijeria ama yule mgabon Oliver ngoma Yani miziki ya miaka hiyo na naenjoy kweli kuliko kuwasikiliza hao vinuka boksa
Hilo sidhani Kama utamaintain, labda unaishi ughaibuni huko. Lakini tambua hiki ni kipindi cha mpito tu. Na hata huko unapoona wewe ni bora pia Kuna ujinga mwingi tu , ambao hautufikii. Cha msingi sikiiiza kazi zao zinazokuvutia ujinga wao waachie wenyewe.
 
Sasa wimbo Kama huo hata usingizi hauji wa kazi gani sasa
Huo wimbo kwa mtu Kama mm najua kazi yake hasa nyakati fulani fulani. Jamani kuelimshwa yupo kaka yetu jelemiah mbona hamumsupport? Et jaman tatizo nini mbona watu wengi hamuyaishi maneno yenu au mnafanya unafiki na kupiga soga muda uende tu.
 
Hilo sidhani Kama utamaintain, labda unaishi ughaibuni huko. Lakini tambua hiki ni kipindi cha mpito tu. Na hata huko unapoona wewe ni bora pia Kuna ujinga mwingi tu , ambao hautufikii. Cha msingi sikiiiza kazi zao zinazokuvutia ujinga wao waachie wenyewe.
😂😂😂Hata kazi zao ni utopolo mtu natumia mb zangu kusikiliza mtu anaeimba nyege nyegezi, au inama nifukue tope na utumbo mwingine km huo 😂😂😂hauko serious bro, waganda wana miziki mizuri sana yenye ujumbe shida Ni lugha ila mi nawaelewa kiasi hivyo nawasikiliza sana, rwanda napo nawasikiliza baadhi huku kwetu wabadilike bado muda wanao hawajechelewa, ila kwa Sasa ndo hivyo mashabiki tumeanza kutafuta uelekeo mwingine kukidhi burudani ya nafsi zetu
 
Huo wimbo kwa mtu Kama mm najua kazi yake hasa nyakati fulani fulani. Jamani kuelimshwa yupo kaka yetu jelemiah mbona hamumsupport? Et jaman tatizo nini mbona watu wengi hamuyaishi maneno yenu au mnafanya unafiki na kupiga soga muda uende tu.
Itakuwa wewe ndie mtunzi wa hizo nyimbo mafimafi😂😂😂 hivi wimbo wa mapenzi Ni mpk utunge matusi?
 
Itakuwa wewe ndie mtunzi wa hizo nyimbo mafimafi😂😂😂 hivi wimbo wa mapenzi Ni mpk utunge matusi?
things will never be the same, usishangae hili kabisa. Wewe endelea kushikamana na ukale wako au uende na wakati. Na hii ina apply katika kila nyanja hadi kwenye tekinolojia huko. So ukiwa stagnant unapitwa na wakati na unaishi kwenye ukale wako katika ulimwengu wa kisiasa lazima utuone watu wa hovyo. Ila sikushangai kabisa ni kawaida.
 
😂😂😂Hata kazi zao ni utopolo mtu natumia mb zangu kusikiliza mtu anaeimba nyege nyegezi, au inama nifukue tope na utumbo mwingine km huo 😂😂😂hauko serious bro, waganda wana miziki mizuri sana yenye ujumbe shida Ni lugha ila mi nawaelewa kiasi hivyo nawasikiliza sana, rwanda napo nawasikiliza baadhi huku kwetu wabadilike bado muda wanao hawajechelewa, ila kwa Sasa ndo hivyo mashabiki tumeanza kutafuta uelekeo mwingine kukidhi burudani ya nafsi zetu
kwahiyo katika maktaba yote umeona nyimbo hizo tu mbili. Mbona Kuna utajir wa nyimbo nzuri tu katika tasnia yetu.
 
things will never be the same, usishangae hili kabisa. Wewe endelea kushikamana na ukale wako au uende na wakati. Na hii ina apply katika kila nyanja hadi kwenye tekinolojia huko. So ukiwa stagnant unapitwa na wakati na unaishi kwenye ukale wako katika ulimwengu wa kisiasa lazima utuone watu wa hovyo. Ila sikushangai kabisa ni kawaida.
Paka mate iteleze Kama nyoka pangoni😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂, good morning chwitiii
 
Paka mate iteleze Kama nyoka pangoni[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23], good morning chwitiii
[emoji39][emoji39][emoji39][emoji39][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
kwahiyo katika maktaba yote umeona nyimbo hizo tu mbili. Mbona Kuna utajir wa nyimbo nzuri tu katika tasnia yetu.
Nyingi zina uelekeo huo

Nachotafuta Ni burudani ya moyo sio ukakasi
 
Keshakimbilia mahakamani

Back
Top Bottom