Harmonize: Nilipewa Mkataba wa kuonewa na WCB na nilisingiziwa kumroga Diamond Platnumz

Ukicheki video ya inde ft dully yule ni mondi kabisa.

Wizkd alivyo kuja Mwanza alimchana live aache kumcopy mondi
Hilo la WizKid, ndo leo nalisikia lakini siwezi kushangaa kwa sababu jamaa ni Diamond Clone mwanzo mwisho...

Nakumbuka siku nausikia wimbo ambao waliimba Harmonize, Diamond na Burnaboy... nilipata shida sana kufahamu Mond kaanzia wapi kaishia wapi na Harmonize kaanzia kwenye kipande kipi!!
 
You're right...

Jamaa ka-copy kila kitu....
 
Management inapochukua 60% wanatumia hiyo percent katika videos zako, production mpaka usafiri wa kuzunguka sehemu mbalimbali. Hivyo anayechukua 40% ana asilimia kubwa kumzidi wa 60% unless kama alikua anajigharamia hivyo vitu vingine pia.
Namimi nilitaka nijue hapo anaposema Diamond anachukua 60% kwamba anachukua yeye kama yeye ama ni pesa ya management?! Kama ni management ni sawa tu maana pale kuna kulipa videos,audios, promotion, wafanyakazi, n.k
 
Huna unalojua acha ushabiki maandazi
 
I always salute huyu mmakonde..

VIJANA KUNA VIZURI VYA KUJIFUNZA KUPITIA HUYU MMAKONDE japo naandika hii koment huku earphones zangu zinapiga INAMA ya baba tiffa
 
Huyo Mondi mkamilifu Kagombana na Dimpoz,Shetta na Ney na wote kaimba nao ngoma!
Ina maana hao wote wakorofi Mondi ndo mkamilifu?kuna shida WCB mkubali mkatae nyie wenye timu zenu!![emoji57][emoji57][emoji57]
Aliyegombana nae hapo, kidogo labda unaweza kusema Ommy Dimpo...

Shetta hajagombana nae, bali katombewa mke wake... nae ni ya kujitakia!!

Yaani mtoto wa kiume, huku ukiwa na mke mzuri kutwa kutwa unashinda kwa vito.mbi... ukigongewa ulalamike?!!

Chanzo cha tofauti na Nay wa Mitego ambacho kinatafsiriwa kwamba ni bifu wala haikuwa bifu per se bali mitazamo ya kisiasa iliyokuwa imemfanya Diamond ajali zaidi maslahi yake kuliko ushikaji!!

Na tatizo lilianza wakati Instagram inawaka moto kweli kweli... huku akina Mange wakimshambulia Makonda na JPM, hususani baada ya issue ya dawa za kulevya...

As we all know, Mond alikuwa upande wa Makonda na Serikali kwa ujumla huku Nay wa Mitego kama umjuavyo, alifikia hadi kukamatwa kipindi kile kutokana na mashairi yake!!

Sasa katikati ya lile songombingo, Nay wa Mitego akaachia track... na haina haja ya kuumiza kichwa kutaka kufahamu kwa wakati kama ule Nay angeachia track yenye maudhui ya aina gani...

Mond, akashindwa kui-post ile ngoma ya Nay wa Mitego...

Yaani akaacha kui-post ngoma ya mshikaji wake kwa kile alichoamini angemkwaza Makonda na Presdaa kwa ujumla!!

Na kwavile Mond ni maslahi ya biashara zake kwanza, akaona "kama vp, poa tu"!
 
Inasemekana jamaa alipigiwa mama yake kwanza,alichofanya yeye ni kulipiza tu,

jamaa kagombana na wengi tu ila watu hawaweki ugomvi wao na jamaa hadharani kwasababu wataonekana wao wanatafuta kiki na mashabiki maandazi watawaandama sana
 
Jamaa kanishangaza sana yaani mtu anakuchukua hujulikani umekataliwa mpaka kwenye shindano kubwa huna kitu ,anakulisha, anakuvisha, unarekodi bure, unashoot video za gharama bure, production bure ma promo bure mwisho wa siku anakupa 40% ya unachoingiza bado unaleta shombo.

duh hapa Konde nimemkataa.
 
Binadamu tuna sahau mapema sana.
 
Sawa ndo tayari ana shida sasa!kwanini akosane na hao washkaji zake wote ht kwa hayo makosa madogo au makubwa pia!

Mlikua mnasema Ruge mnyonyaji kwa dai imekua tofauti...!!![emoji55][emoji1][emoji1][emoji1][emoji2][emoji1]
 
Inasemekana jamaa alipigiwa mama yake kwanza,alichofanya yeye ni kulipiza tu,

jamaa kagombana na wengi tu ila watu hawaweki ugomvi wao na jamaa hadharani kwasababu wataonekana wao wanatafuta kiki na mashabiki maandazi watawaandama sana
Hivi ukiacha hao waliotajwa, hao wengi ni akina nani?!

Tatizo watu wanachanganya kati ya ugomvi na issue za kibiashara...

Kwa mfano, kulikuwa na misunderstanding kati ya Diamond na EATV... that's purely business!!!

Na EATV walikasirika zaidi baada ya kuandaa tuzo za muziki lakini Wasafi wakawaondoa wasanii wake wote waliokuwa nominated including Mond mwenyewe!!

Zile tuzo zikafia hapo hapo!!

Sasa sijui katika kulinda ajira ama vp, baadhi ya Watangazaji wa EATV wakauchukua ugomvi wa EATV na Diamond, wakaufanya wao!!
 
Nazungumzia wasanii wenzie achana na hizo mambo za clouds sijui eatv
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…