aise
JF-Expert Member
- May 16, 2018
- 5,175
- 16,488
Hadithi ya Nuhu unaiamini kabisa mkuu?Hahaha! Kiburi chako kinanikumbusha watu wa Nabii Nuhu alivyotumwa kwa watu wake awapatie ujumbe kutoka kwa Mungu. Qur'an inanukuu:
Wakamwambia Nabii Nuhu:"Kwani wewe waliyokufuata ni watu gani? Ni watu wadhalilifu, watu hohehahe! Hatujaona hata businessman mmoja kakafuata wewe! Mtu tajiri na pesa zake kaamua kukufuata, ingekuwa hivyo, angalau ungetushtua juu ya utume wako!"
Wakamdharau na hawakuishia hapo bali walimwambia Nuhu na Qur'an inanukuu vilevile:
"Hakuwa huyu Nuhu isipokuwa ni mtu tu kama sisi. Lengo lake kutangaza utume anataka kujifanya yeye apate cheo na ubora juu yetu."
"Huyo ni mtu tena kama mfano wenu ninyi. Kama Mungu kweli alikuwa anataka kutuletea Mtume, basi huyo Mtume asingekuwa ni mwanadamu, angekuwa ni malaika."
Hii dunia yupo aliyeifanya iwepo! Wanasayansi wenyewe wanaochunguza anga wakiangalia kanuni na nidhamu za maumbile ya huko namna yanavyokwenda wanakubaliana bila shaka yupo anayesanifu hii hali!
Halikadhalika, bila shaka yupo aliyekuleta. Kuwa na akiba, usiwe na kiburi. Ila ukisema potelea mbali na ukaendelea na utaraibu wako nayo si mbaya! Kwani potelea mbali nayo ni njia utakuwa umeichagua mwenyewe.
Fanya maamuzi sahihi! Ishi kwa kufakari!
Tukianza kuichambua hiyo hadithi ina mapungufu mengi mkuu. Wewe kama unaamini ilikuwa kweli endelea kuamini.
Mimi naiona kama hadithi nyingine tu za kupoteza muda