Hata hiki kidubwasha tunaagiza China!

Kwani mkuu. Wewe una kipi ulichokibuni Kama mtanzania?
 
South Africa wenye viwanda ni wazungu ndugu zao Ulaya wanawapa teknolojia na mitaji

Hata tungefanyaje hatuwezi shindana na South Africa Kiuchumi

Kule waafrika wachovu kama Tanzania tu
 
Umemuelewesha vyema, watu wanawananga madokta wetu hawawezi kutengeneza hata panado ila hawajui ni gharama kiasi gani inatumika mpaka dawa inakua tayari kwa matumizi ya binadamu. Maarifa pekee hayatoshi lazima kuwe na watu wa kuweka mzigo.
 
Huwezi endesha viwanda kwa chuma cha screpa. China waliwahi jaribu wakashindwa. Kinachotakiwa ni chuma safi, kingi na cha bei rahisi. Mfano huko Liganga tungechimba na kusafisha tupate chuma safi. Mtu akitaka kuunda chochote awe na uhakika wa chuma.
Hiyo huwezi ndiyo umeshajitia loki. Hakuan duniani wanaonunuwa na kuhuisha "scrap" kama Pakistan. Umeenda pasipo.

Jionee juu hapo post #75. Kama haikutoshim nakuongeza hapa uone scrap zinavyofanywa Pakistan, tena tabata yao tu:


View: https://youtu.be/OvK9mBPrkS4?si=SBHG-n2coL_RazUl
 
Kwani mkuu. Wewe una kipi ulichokibuni Kama mtanzania?
Umemuuliza swali kama ambayo bilionea wa Marekani amewahi sema Kwa wanaoponda Pesa na kusema Pesa ni kitu Gani ? Akasema hakikisha kwanza una pesa nyingi sana ndipo useme pesa ni kitu gani .Sio Mtu lofa halafu anasema pesa ni kitu Gani halafu anakuomba Hela kikimbana Cha kumbana
 
bado hajaanza uzalishaji

Kufungua kiwanda cha hivyo vitu ambavyo mnaona ni vidogo si mchezo ujue
HIvi mnadhani watu hawapendi kuwekeza huko ?

Mfano umefanikiwa kutengeneza hiko kimoja..malighafi utakua nazo za kutosha ?
Tunaishi poor developing country ,raw-material zipo ila technology ya kupata Hizo material bado ni poor,Umeme ni kisanga,urasimu mwingi ,bado Mtu anataka miracle kutoka Kwa vijana wanaotoka familia duni bila mtaji wa connection,hii so sawa
 
Umemuelewesha vyema, watu wanawananga madokta wetu hawawezi kutengeneza hata panado ila hawajui ni gharama kiasi gani inatumika mpaka dawa inakua tayari kwa matumizi ya binadamu. Maarifa pekee hayatoshi lazima kuwe na watu wa kuweka mzigo.
Hao madokta wameshindwa nn kuwashauri wenye maamuzi wakachukua mikopo ya kuendeleza ujuzi na maarifa kwa wananchi?
Kwani mkuu. Wewe una kipi ulichokibuni Kama mtanzania?
 
Sidhani kama shida ni wasomi , sera za nchi ndio zinazotufikisha huku kuwatukana hao wasomi wakati wanamaliza elimu tayari wanakuwa directed kisera unafikiri kosa ni la kwao?

Ni mara ngapi mafundi simu kariakoo wamekamatwa kwa kubadili IMEI namba za simu ,hizo ni product za watu wa IT , ila hakuna sera za kuwapa uhuru wafanye kazi wanakamatwa unafikiri kuna mwingine atathubutu? Sishangai kwa hicho sababu hata toothpick tunaagiza china. Toothpick nayo inahitaji elimu ya chuo?
 
Ukiwaangalia Wahindi Youtube wanavyounda vitu utashangaa, sisi hatujali. Kwanza nadhani umaskini (hasa ujinga) unatakiwa uendelee kukua ili tutawalike kirahisi.
 
Hao madokta wameshindwa nn kuwashauri wenye maamuzi wakachukua mikopo ya kuendeleza ujuzi na maarifa kwa wananchi?
Mkuu hii nchi mbona kama hauifahamu . Tz hii hii ambayo imekaa ki- fanya yako uende zako
 
Wachina wana viwanda vingi vikubwa...wakati wanajipanga sisi tulikuwa tumelala...gen 80-...sasa hv lawama zipo kwa 90+ gen kwamba hawawezi vitu
Kifupi, serikali iwaombe china watengeneze viwanda hapa nchini, wasomi wapate ajira
 
Wenyewe wanavimba na kujiita majina makubwa makubwa mara profesa, daktari, injinia sijui nani nani kumbe vilaza tu waliokariri!
 
Usichokijua ni kwamba vingine vinatengenezwa hapa hapa bongo ila vinaandikwa vinatoka uko china, uk, usa n.k kutokana na kasumba ya wabongo kupenda vya nje, izo made in china zisikushtue ni janja janja za kibiashara tu, pia mamlaka zikijua ni bidhaa ya ndani basi utaandamwa na kodi, tozo, ushuru n.k mpaka unakuta bidhaa ya ndani inauzwa ghali kuliko ya nje, vile vile hili ni suala la uwekezaji sio rahisi kwa graduate wa machenics au injinia kuwa na pesa ya kumudu kuunda gari. Tutawasema madokta wameshindwa kutengeneza hata panadol lakini hatujiulizi gharama zinazohitajika kuanzia kwenye utafiti mpaka dawa inahalalishwa kwa matumizi ya binadamu. Graduate au dokta alieajiriwa ataweza kuwa na bajeti ya milioni 200+ afanye utafiti? TUACHE CHUKI DHIDI YA WASOMI
 
Nipo na gamba langu la karatasi kwa ajili ya kutambiana mtaani
 
Nchi ya ajabu sana hii
 
Ukiondoa chuma, vitu vingine vinavyotoka nje raw materials wanatoa wapi?
 
Pakistani maskini choka mbaya. Wanakaribia kufirisika. Huwezi fika popote kwa viwanda vya kutumia scrap metals. Utaishia kuunda makarai ya kukaangia mihogo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…