Hata hiki kidubwasha tunaagiza China!

Hata hiki kidubwasha tunaagiza China!

View attachment 2879915

Kwani hapo VETA, UDSM, UDOM na huko kwingine mnaenda kusoma nn?., maana kama kuendesha nchi mmeshindwa, kila kitu mnaharibu!

Wasomi msiokuwa na msaada wowote kwa nchi yenu, mnashindwa hata kuunda kidubwana local kama hicho mnakimbilia kuunda magari mtayaweza?

Kwa sasa wengine mnakimbilia kwenye ufugaji wa kuku broiler, kweli?. Msomi uliyesoma enginering unaanzaje kufuga kuku broiler eti ndo kazi yako ya kuendesha maisha na umebweteka kabisa.

Wengine mnakimbilia kusoma kozi za ONLINE kutengeneza sabuni za magadi, mtu umesoma miaka 4 halafu chuo halafu unakuja kusoma kozi ya siku moja na inakusaidia maisha, asa mnafuata nn huko chuo?, mnaenda kusoma ili mturingishie mtaani kuwa mlisoma vyuo?

Nchi ya ajabu sana hii...
Kwani mkuu. Wewe una kipi ulichokibuni Kama mtanzania?
 
Sio kukosa teknolojia. Tatizo hatujali, tunaongea sana. Wewe juhudi wanazofanya CCM kubaki madarakani, hadi wanatumia vyombo vyote vya dola, mpaka KJT! Ingekua imewekeza kwenye maendeleo tungekua tunakimbizana na SA. Lakini hatujali, wananchi hatujali na serikali ya ccm haijali. Wote hatujali. Upinzani unajitahidi kutuamsha tusilale lakini ndio kwanza tunaimba pambio mama yuko kazini.
South Africa wenye viwanda ni wazungu ndugu zao Ulaya wanawapa teknolojia na mitaji

Hata tungefanyaje hatuwezi shindana na South Africa Kiuchumi

Kule waafrika wachovu kama Tanzania tu
 
Tatizo hapo sio wasomi kama unavyowanga hapa. Hii ni issue ya uwekezaji, ni biashara lazima awepo mtu wa kuweka mtaji kufanikisha hilo. Ukitoa mambo ya ubunifu, uzalishaji wa hiyo kitu unahitaji watu wa kada tofauti tofauti.

Utahitaji mtu wa manunuzi, kununua hizo materials kwa ajili ya uzalishaji.

Utahitaji eneo kwa kununua au kukodi ili kusimika mitambo kwa ajili ya kuhifadhi materials, uzalishaji na kuhifadhi hizo bidhaa.

Utahitaji mitambo kuchakata hizo materials kuzalisha hiko kifaa.

Utahitaji nguvu kazi katika kila hatua ya uzalishaji kufanikisha hilo.

Utahitaji mtu wa mauzo kufanikisha faida inapatikana na uzalishaji unakua endelevu.

Shughuli katika hatua zote hizo zinahitaji fedha, hivyo hilo swala ni swala la uwekezaji wa fedha za kutosha tu na wala sio swala la kutupia lawama hawa wahitimi.
Umemuelewesha vyema, watu wanawananga madokta wetu hawawezi kutengeneza hata panado ila hawajui ni gharama kiasi gani inatumika mpaka dawa inakua tayari kwa matumizi ya binadamu. Maarifa pekee hayatoshi lazima kuwe na watu wa kuweka mzigo.
 
Huwezi endesha viwanda kwa chuma cha screpa. China waliwahi jaribu wakashindwa. Kinachotakiwa ni chuma safi, kingi na cha bei rahisi. Mfano huko Liganga tungechimba na kusafisha tupate chuma safi. Mtu akitaka kuunda chochote awe na uhakika wa chuma.
Hiyo huwezi ndiyo umeshajitia loki. Hakuan duniani wanaonunuwa na kuhuisha "scrap" kama Pakistan. Umeenda pasipo.

Jionee juu hapo post #75. Kama haikutoshim nakuongeza hapa uone scrap zinavyofanywa Pakistan, tena tabata yao tu:

View: https://youtu.be/OvK9mBPrkS4?si=SBHG-n2coL_RazUl
 
Kwani mkuu. Wewe una kipi ulichokibuni Kama mtanzania?
Umemuuliza swali kama ambayo bilionea wa Marekani amewahi sema Kwa wanaoponda Pesa na kusema Pesa ni kitu Gani ? Akasema hakikisha kwanza una pesa nyingi sana ndipo useme pesa ni kitu gani .Sio Mtu lofa halafu anasema pesa ni kitu Gani halafu anakuomba Hela kikimbana Cha kumbana
 
bado hajaanza uzalishaji

Kufungua kiwanda cha hivyo vitu ambavyo mnaona ni vidogo si mchezo ujue
HIvi mnadhani watu hawapendi kuwekeza huko ?

Mfano umefanikiwa kutengeneza hiko kimoja..malighafi utakua nazo za kutosha ?
Tunaishi poor developing country ,raw-material zipo ila technology ya kupata Hizo material bado ni poor,Umeme ni kisanga,urasimu mwingi ,bado Mtu anataka miracle kutoka Kwa vijana wanaotoka familia duni bila mtaji wa connection,hii so sawa
 
Umemuelewesha vyema, watu wanawananga madokta wetu hawawezi kutengeneza hata panado ila hawajui ni gharama kiasi gani inatumika mpaka dawa inakua tayari kwa matumizi ya binadamu. Maarifa pekee hayatoshi lazima kuwe na watu wa kuweka mzigo.
Hao madokta wameshindwa nn kuwashauri wenye maamuzi wakachukua mikopo ya kuendeleza ujuzi na maarifa kwa wananchi?
Kwani mkuu. Wewe una kipi ulichokibuni Kama mtanzania?
 
Sidhani kama shida ni wasomi , sera za nchi ndio zinazotufikisha huku kuwatukana hao wasomi wakati wanamaliza elimu tayari wanakuwa directed kisera unafikiri kosa ni la kwao?

Ni mara ngapi mafundi simu kariakoo wamekamatwa kwa kubadili IMEI namba za simu ,hizo ni product za watu wa IT , ila hakuna sera za kuwapa uhuru wafanye kazi wanakamatwa unafikiri kuna mwingine atathubutu? Sishangai kwa hicho sababu hata toothpick tunaagiza china. Toothpick nayo inahitaji elimu ya chuo?
 
Wewe unasema hicho? Hata sinfdano tu za kushonea hatutengenezi wenyewe.

Hik nchi inachukuwa nchi na watu siyo kuja kufundisha vyuo vyetu vya ufundi.

Nenda hata "tabata" ya Krachi, Pakistan, chukuwa fundi mmoja mlipe vizuri akae miaka 5 uone atatowa mafundi wangapi. Jionee:

View: https://youtu.be/0GyDCGMrcpk?si=shXWiKPaRu78KV8U

Ukiwaangalia Wahindi Youtube wanavyounda vitu utashangaa, sisi hatujali. Kwanza nadhani umaskini (hasa ujinga) unatakiwa uendelee kukua ili tutawalike kirahisi.
 
Hao madokta wameshindwa nn kuwashauri wenye maamuzi wakachukua mikopo ya kuendeleza ujuzi na maarifa kwa wananchi?
Mkuu hii nchi mbona kama hauifahamu . Tz hii hii ambayo imekaa ki- fanya yako uende zako
 
Wachina wana viwanda vingi vikubwa...wakati wanajipanga sisi tulikuwa tumelala...gen 80-...sasa hv lawama zipo kwa 90+ gen kwamba hawawezi vitu
Kifupi, serikali iwaombe china watengeneze viwanda hapa nchini, wasomi wapate ajira
 
Wenyewe wanavimba na kujiita majina makubwa makubwa mara profesa, daktari, injinia sijui nani nani kumbe vilaza tu waliokariri!
 
View attachment 2879915

Kwani hapo VETA, UDSM, UDOM na huko kwingine mnaenda kusoma nn?., maana kama kuendesha nchi mmeshindwa, kila kitu mnaharibu!

Wasomi msiokuwa na msaada wowote kwa nchi yenu, mnashindwa hata kuunda kidubwana local kama hicho mnakimbilia kuunda magari mtayaweza?

Kwa sasa wengine mnakimbilia kwenye ufugaji wa kuku broiler, kweli?. Msomi uliyesoma enginering unaanzaje kufuga kuku broiler eti ndo kazi yako ya kuendesha maisha na umebweteka kabisa.

Wengine mnakimbilia kusoma kozi za ONLINE kutengeneza sabuni za magadi, mtu umesoma miaka 4 halafu chuo halafu unakuja kusoma kozi ya siku moja na inakusaidia maisha, asa mnafuata nn huko chuo?, mnaenda kusoma ili mturingishie mtaani kuwa mlisoma vyuo?

Nchi ya ajabu sana hii...
Usichokijua ni kwamba vingine vinatengenezwa hapa hapa bongo ila vinaandikwa vinatoka uko china, uk, usa n.k kutokana na kasumba ya wabongo kupenda vya nje, izo made in china zisikushtue ni janja janja za kibiashara tu, pia mamlaka zikijua ni bidhaa ya ndani basi utaandamwa na kodi, tozo, ushuru n.k mpaka unakuta bidhaa ya ndani inauzwa ghali kuliko ya nje, vile vile hili ni suala la uwekezaji sio rahisi kwa graduate wa machenics au injinia kuwa na pesa ya kumudu kuunda gari. Tutawasema madokta wameshindwa kutengeneza hata panadol lakini hatujiulizi gharama zinazohitajika kuanzia kwenye utafiti mpaka dawa inahalalishwa kwa matumizi ya binadamu. Graduate au dokta alieajiriwa ataweza kuwa na bajeti ya milioni 200+ afanye utafiti? TUACHE CHUKI DHIDI YA WASOMI
 
Nipo na gamba langu la karatasi kwa ajili ya kutambiana mtaani
 
Sidhani kama shida ni wasomi , sera za nchi ndio zinazotufikisha huku kuwatukana hao wasomi wakati wanamaliza elimu tayari wanakuwa directed kisera unafikiri kosa ni la kwao?

Ni mara ngapi mafundi simu kariakoo wamekamatwa kwa kubadili IMEI namba za simu ,hizo ni product za watu wa IT , ila hakuna sera za kuwapa uhuru wafanye kazi wanakamatwa unafikiri kuna mwingine atathubutu? Sishangai kwa hicho sababu hata toothpick tunaagiza china. Toothpick nayo inahitaji elimu ya chuo?
Nchi ya ajabu sana hii
 
Unatakiwa kwanza uwe na chuma. Ukiwa huna chuma hata sindano utaagiza, ukiwa na chuma utaweza kuzalisha karibu kila kitu. Ni jukumu la serikali kuhakikisha nchi inazalisha chuma cha kutosha na kwa bei rahisi. Kama serikali bado haijaona umuhimu wa kuwa na chuma tutasubiri sana na kuendelea kulaumu wasio husika.
Ukiondoa chuma, vitu vingine vinavyotoka nje raw materials wanatoa wapi?
 
Hiyo huwezi ndiyo umeshajitia loki. Hakuan duniani wanaonunuwa na kuhuisha "scrap" kama Pakistan. Umeenda pasipo.

Jionee juu hapo post #75. Kama haikutoshim nakuongeza hapa uone scrap zinavyofanywa Pakistan, tena tabata yao tu:

View: https://youtu.be/OvK9mBPrkS4?si=SBHG-n2coL_RazUl

Pakistani maskini choka mbaya. Wanakaribia kufirisika. Huwezi fika popote kwa viwanda vya kutumia scrap metals. Utaishia kuunda makarai ya kukaangia mihogo.
 
Back
Top Bottom