Ukweli ni kwamba hali ya kisiasa ya sasa hapa nchini inakatisha tamaa sana.
Ukisoma maandiko mengi humu ndani ya wenye mrengo wa upinzani, wanailaumu ccm kuwadhoofisha huku wakisahau kwamba hakuna chama siasa chenye jukumu la kuruhusu chama pinzani kisitawi.
Ukiwa kama mpinzani unalazimika kutumia njia yoyote kuhakikisha chama chako kinavutia raia wa kawaida Kwa wingi, kikishaungwa mkono kiwango hicho hata mkiibiwa kura hao watu hawatakubali.
Hali tuliyonayo Kwa sasa hapa nchini tuna wapinzani dhaifu sana wanaonunulika wabinafsi wababe na wengi wao wako pale Kwa maslahi yao binafsi.
Katika mazingira ya namna hii hakuna mwamko mkubwa sana huku mtaani unaoleta kashkash kama za mwaka 2010 ambapo hata ccm wenyewe walikuwa wamejikatia tamaa.
Kwa sasa taifa linazungumzia kupanda Kwa gharama za maisha, ila wapinzani wamekomaa na tume huru mara uchaguzi huru mara katiba mpya nk.
Katika muktadha kama huo akija kinana akasema tunduma njia nne Bashe akaja na mbolea nusu bei Samia akaja na elimu bure hadi form six nk itakuwa ngumu sana raia kukuelewa mpinzani kuwa unapambana Kwa Kwa niaba ya mwananchi wa kawaida.
Naomba wapinzani tubadili namna ya kufanya siasa tufanye siasa zenye ushawishi kwa watu ili tuungwe mkono na ccm istaafishwe siasa.
Tunataka vyombo huru vya kisheria,polisi,tume huru,
Ukosefu wa demokrasia ndio chanzo Cha majanga yote,
Sasa hv Kuna kikundi kinachoongoza nchi,hakihijiwi na yoyote,kinafanya kinavyotaka,nikupe mfano,hile state lodge aliyojenga Jiwe kwao chato,iwe inapokelea wageni wa Raisi ilijengwa kwa bajeti ipi,iliyopitishwa na nani?na sasa hv hiyo lodge inatumikaje!mahesabu yake yaliamuliwa na mtu mmoja kwa utashi wake,huu ni wizi na nchi haiwezi endelea kama mtu mmoja anajichukulia pesa hazina anavyotaka,kamsome Mobutu wa Zaire alivyofanya.
Loyal tour,tuliambiwa "haijatumia pesa za serikali"imechangiwa na watz""hawatajwi!!hao watz wenye upendo wanao weza kutoa pesa mabilioni kama sadaka ni kina nani!?
Kiongozi wa ccm anasimama anasema hapa hatuleti zahanati kwa vile diwani wenu ni WA upinzani,Chadema!!kwamba Ili maendeleo yaje inabidi tuchague ccm!
Maendeleo yanaletwa na Kodi zetu,