Hata Mwl Nyerere ilifikia kipindi akaitwa kiongozi asiyeambilika, lakini hatujawahi kusikia viongozi waliomfuata wakimkosoa hadharani ughaibuni

Idugunde

JF-Expert Member
Joined
May 21, 2020
Posts
6,404
Reaction score
6,969
Mbona mkuu wa nchi yetu kama anafanya ndivyo sivyo? Kuongoza nchi kumbe kazi sana. Upo nje kwenye ziara ya kikazi alafu unaeleza kwenye media kubwa kama NY times kuwa mtangulizi wako alikuwa stubborn, hii inaleta picha gani?

Hukuwa na raha wakati unafanya nae kazi pamoja kiasi cha kumchukia kwa kutofuata ushauri wako wakati wewe ulipokuwa msaidizi wake?

Ulifanya nae kazi huku ukiwa na kinyongo maana alikuwa mkaidi?

Ina maana ulikuwa unacheka nae hadharani lakini moyoni humtaki sababu ni stubborn?

Lakini mbona hata Mwl Nyerere inasemekana wazi kabisa alikuwa mkaidi juu ya kufuata ushauri wa wasaidizi wake mpaka ilifikaia hatua akaitwa baba haambiliki, hatujawahi kusikia Mzee Mwinyi au Mkapa wakimnanga huko mamtoni?

Inasemekana alishauriwa masuala mengi tu na akakaidi, mfano aliambiwa asihamishe watu kwenye miji yao kwa ajili ya vijiji vya ujamaa lakini akawahamisha. Jambo ambalo lilileta lawama kubwa. Lakini hatikusikia akipondwa huko nje. Alishauriwa asiijifanye yeye ni superpower wa Afrika lakini akakag'ag'ania kupeleka majeshi Msumbiji, Zimbabwe na Uganda ,mataokeo yake Tanzania ikakwama kiuchumi.

Tunajichafua sisi Watanzania huku wazungu wakitucheka.
 
Mbona mkuu wa nchi yetu kama anafanya ndivyo sivyo? Kuongoza nchi kumbe kazi sana. Upo nje kwenye ziara ya kikazi alafu unaeleza kwenye media kubwa kaka NY times kuwa mtangulizi wako alikuwa stubborn, hii inaleta picha gani?

Tunajichafua sisi watanzania huku wazungu wakitucheka.

Muache atoe ya moyoni mwake ili tumuelewe hakuwa pamoja naye katika baadhi ya mambo.
 
Mbona mkuu wa nchi yetu kama anafanya ndivyo sivyo? Kuongoza nchi kumbe kazi sana. Upo nje kwenye ziara ya kikazi alafu unaeleza kwenye media kubwa kaka NY times kuwa mtangulizi wako alikuwa stubborn, hii inaleta picha
Kumbe wewe bado hujui kwa nini anafanya hivyo?

Huu ni wakati wake wa kujijengea jina, sifa ya kuwa kiongozi mzuri (anadhani hivyo).

Huko alikokwenda kuyasemea haya kuna maana kubwa kwake. Ni kwa wakubwa wa dunia, kwa hiyo hao wakimkubali, anajihisi wengine wote watamtambua.

Huyu ni kiongozi hafifu sana.

Hivi ulishamsikia Pence akilalamika juu ya Trump, pamoja na uhayawani wote wa Trump? Hata Biden haendi Ulaya kulalamika juu ya mtangulizi wake.
 
Mbona mkuu wa nchi yetu kama anafanya ndivyo sivyo? Kuongoza nchi kumbe kazi sana. Upo nje kwenye ziara ya kikazi alafu unaeleza kwenye media kubwa kaka NY times kuwa mtangulizi wako alikuwa stubborn, hii inaleta picha gani?

Hukuwa na raha wakati unafanya nae kazi pamoja kiasi cha kumchukia kwa kutofuata ushauri wako wakati wewe ulipokuwa msaidizi wake?

Ulifanya nae kazi huku ukiwa na kinyongo maana alikuwa mkaidi?

Ina maana ulikuwa unacheka nae hadharani lakini moyoni humtaki sababu ni stubborn?

Lakini mbona hata Mwl Nyerere inasemekana wazi kabisa alikuwa mkaidi juu ya kufuata ushauri wa wasaidizi wake mpaka ilifikaia hatua akaitwa baba haambiliki, hatujawahi kusikia Mzee Mwinyi au Mkapa wakimnanga huko mamtoni?

Inasemekana alishauriwa masuala mengi tu na akakaidi, mfano aliambiwa asihamishe watu kwenye miji yao kwa ajili ya vijiji vya ujamaa lakini akawahamisha. Jambo ambalo lilileta lawama kubwa. Lakini hatikusikia akipondwa huko nje. Alishauriwa asiijifanye yeye ni superpower wa Afrika lakini akakag'ag'ania kupeleka majeshi Msumbiji, Zimbabwe na Uganda ,mataokeo yake Tanzania ikakwama kiuchumi.

Tunajichafua sisi watanzania huku wazungu wakitucheka.
Poleni yatima. Kubalini matokeo kuwa Saigon Club imeshinda,wenye chama chao wamerudi nyie makinikia ya mwendazake kausheni tu.
 
Weye unapuuzwa na kila mtu na tena ni kila siku.Jirekebishe upate kwa kucheza.Acha maluweluwe ya kudhani "mtukufu" yu hai.Utachekwa kama umebeba mapapai mifuko ya nyuma ya dela lako.
Hii mada inamhusu JPM kwa akili yako ndogo? JPM alikuwa rais wa maisha hapa Tanzania? Kwa nini mnapenda kudakia mambo makubwa?
 
Lakini mbona hata Mwl Nyerere inasemekana wazi kabisa alikuwa mkaidi juu ya kufuata ushauri wa wasaidizi wake mpaka ilifikaia hatua akaitwa baba haambiliki, hatujawahi kusikia Mzee Mwinyi au Mkapa wakimnanga huko mamtoni?
Unatoa mifano kama huu hapa ambao hauhusiani kabisa na wala haufanani na ya hawa wawili, Magufuli na Samia.

Kule kunakosemekana kutoambilika kwa Mwalimu ni baada ya mijadala na kuelezana, tena kisomi kwa hoja. Hoja hafifu zinakataliwa.

Hapa anayelalamika hatoi hoja za maana na yule anayelalamikiwa hana muda wa kusikiliza wala kueleza chochote juu ya anayoyafanya kikaeleweka.

Chukulia mfano wa COVID-19 aliyoitumia kama mfano wa Samia kutokubaliana na bosi wake.

Kuna maelezo yoyote aliyoyafikisha kwa Magufuli, yenye ushawishi kuhusu hatua zinazotakiwa kuchukuliwa dhidi ya ugonjwa huo, halafu hakusikilizwa maoni yake?

Na kwa upande wa Magufuli, alikaa chini na kueleza kiufasaha kwa nini hapakuwa na ulazima wa kufanya yote yaliyokuwa yakifanywa na dunia ?

Kwa hiyo mfano wako juu ya kutoambiwa kwa Mwalimu ni tofauti kabisa na ya hawa wawili, ambao wote hawakuwa na uwezo wa kueleza chochote kikaeleweka.
 
..tena Maza amemsitiri sana Jpm.

..angeweza kutoa siri zote mpaka za mambo ya kikatili ya awamu ya 5 lakini amekuwa mstaarabu kusema alichosema.
Nafikiri hoja hapa sio kutokosoa mambo ya kikatiri ya awamu ya tano. Kwa nini ayasemehe huko Usa?

Kwa uwezo wako mdogo unadhania kama kuna ukatiri ulifanyika awamu ya tano hausiki?

Alisemaje juu ya Lissu? Hakusema kuwa kama alipigwa risasi na askari wa Tanzania basi ansingepona maana askari wa Tanzania hawezi kukosa shabaha na kupoteza risasi 36.

Tindo tumia akili.
 
Unatoa mifano kama huu hapa ambao hauhusiani kabisa na wala haufanani na ya hawa wawili, Magufuli na Samia.

Kule kunakosemekana kutoambilika kwa Mwalimu ni baada ya mijadala na kuelezana, tena kisomi kwa hoja. Hoja hafifu zinakataliwa.

Hapa anayelalamika hatoi hoja za maana na yule anayelalamikiwa hana muda wa kusikiliza wala kueleza chochote juu ya anayoyafanya kikaeleweka.

Chukulia mfano wa COVID-19 aliyoitumia kama mfano wa Samia kutokubaliana na bosi wake.

Kuna maelezo yoyote aliyoyafikisha kwa Magufuli, yenye ushawishi kuhusu hatua zinazotakiwa kuchukuliwa dhidi ya ugonjwa huo, halafu hakusikilizwa maoni yake?

Na kwa upande wa Magufuli, alikaa chini na kueleza kiufasaha kwa nini hapakuwa na ulazima wa kufanya yote yaliyokuwa yakifanywa na dunia ?

Kwa hiyo mfano wako juu ya kutoambiwa kwa Mwalimu ni tofauti kabisa na ya hawa wawili, ambao wote hawakuwa na uwezo wa kueleza chochote kikaeleweka.
Mkuu upo sawa. Lakini mimi nimeweka hii mifano kuthibitisha tu kuwa hata hayati Nyerere aliwahi kushutumiwa na wasaidizi wake juu ya ukaidi.
 
Kumbe wewe bado hujui kwa nini anafanya hivyo?

Huu ni wakati wake wa kujijengea jina, sifa ya kuwa kiongozi mzuri (anadhani hivyo).

Huko alikokwenda kuyasemea haya kuna maana kubwa kwake. Ni kwa wakubwa wa dunia, kwa hiyo hao wakimkubali, anajihisi wengine wote watamtambua.

Huyu ni kiongozi hafifu sana.

Hivi ulishamsikia Pence akilalamika juu ya Trump, pamoja na uhayawani wote wa Trump? Hata Biden haendi Ulaya kulalamika juu ya mtangulizi wake.
Mbona Jiwe alikua anakandia watangulizi wake hasa mzee wa msoga?!
 
….. hata Nyerere ilifikia
Ila yule alianza kabla hata hajaupata Uraisi kwa kusema wakinichagua Watalimia meno
Sisi vibogoyo mkatulimisha pia nyie mna dhambi.

Nyerere hakusema tubaki na mavi yetu nyumbani.

Kila binadamu ana mapungufu yake lakini chuki na visasi ni vibaya sana daima utateseka tu hata uondoke
 
Back
Top Bottom