Basi siku moja nilikuwa India nilienda kwa ajili ya matibabu, wakati narudi nipo Airport pale pale India akatokea mama mmoja ni Mtanzania lakini mwenye asili ya India, alikuwa kaenda kwao huko India sasa anarudi Tz. Pale Airport aliniona na passport ya Tz hivyo akanijua akaja kunisalimia wakati tumepanga foleni ya kucheki in, alikuwa na mizigo mingi kweli kweli basi akaanza kuniomba nimsaidie baadhi ya mabegi yake yawe kwa jina langu sababu mabegi yake yamezidi inatakiwa isizidi kg 100 ikizidi unalipia.
Nikamkatalia kabisa nikamwambia lipia akasema hana pesa akaniomba kuongea na mimi pembeni ananibembeleza sana nimsaidie nikakataa kabisa.
Wakati nakaribia kucheki in akaja tena kuniomba nimsaidie akaanza kufurusha mabegi yake anatoa nguo moja moja na kuzikunguta ili nione hajabeba kitu kibaya. Kweli niliona alikuwa na nguo za watoto lakini bado nilisita.
Baadae kabisa akakaa pembeni kama kachanyikiwa hajui afanye nini na hana pesa ya kulipia, nikajikuta namuonea huruma nikamsaidia begi moja lakini nililifanyia upekuzi tena kujiridhisha.
Tulipofika bongo alinishukuru sana, na mimi nikamshukuru Mungu kwa kuweza kumsaidia japo nilikuwa nina hofu
ila nimekoma siwezi tena kumsaidia mtu nisiyemjua Airport na hadi sasa siamini kama nilimsaidia yule mama na sikupata tatizo lolote.
Imagine umetoka hospital ni mgonjwa mara unajikuta upo selo tena nchi ya watu kwa madawa ya kulevya..