Hata siku 1 usimsaidie mtu kubeba mzigo Airport, wema utakuponza

Mimi sio airport hata nikipanda public transport iwe kivuko, daladala sijui mwendokasi sibebi kifurushi cha mtu hata mtoto .
Nikikuonea huruma kama una mtoto nasimama nakupisha ukae na mtoto wako
Nazidi kujifunza, mimi kwa kujikuta pawa mabula kusaidia kila naemuona ana mizigo mingi hasa ferry kumbe najihatarisha sana.
 
Wale jamaa wanaoomba watu wawasaidie kuwasafirishia mizigo airprt kwa nje wahesabiwe kama waarifu. Wakamatwe.
 
Aisee.
Kumbe ndio huwa hv jamani.
Inasikitisha sana.
 
Tuliwahi kumpa mama mmoja lift maeneo ya Hedaru, kumbe yule mama alikuwa amebeba mirungi aieee Kufika Korogwe tukakamatwa sitahasau ile kadhia.
Aisee.
Sasa huu msala si unawaangukia nyie wote kwenye gari!
 
Kuna wale jamaa airport wanaojifanya wana mizigo mingi sasa wanakuomba uwasaidie kwa vile wewe wamekuona una kibegi kidogo ambacho hata kilo 15 hakifiki! Kwa kweli itabidi niwaogope!
 
Sio Airport tu, Usikubali kirahisi kumbebea mtu usiyemjua mzigo, furushi, bahasha, mtoto mdogo au hata pesa kwa sababu zama za ucha mungu wema na kusaidiana kwa kuamini kuwa mtenda ana nia nzuri ....Zimepita na waharifu wabobezi wanapita humo humo ... epuka kitu kinachoitwa "Naivety"
 
Itakuwa NI wewe Tu
 
Nakumbuka miaka kama 9 nyuma .........kwenye dala dala za kawe kuna mwanangu mmoja alipokea mzigo kwa mzee hamjui ila ilikuwa tu kusaidia kiaina bana bana ..... ..kumbe lile furushi lina nyayo za binadamu ...... yule jamaa alikuwa na mambo kama ya shirki huyo (msaidiwa mzigo) sasa pale kawe jirani na clouds gari likakaguliwa baada ya kuhisiwa kile kiroba kama kilikuwa na magendo sijui wale polisi walipata taarifa wapi.........si kakamatwa mshikaji wangu bana..........yule mzee kamkana kabisa hati hamjui na wala ule mzigo sio wake..........ila uzuri kuna abiria waliona wakati anampa amsaidie kubeba ...............basi akakamatwa mshikaji na yule mzee wote mpaka kawe polisi..........mkuu wa kituo kuja akasema wee mzee ndio mwenye kifurushi huyu kijana bado mdogo na hana hatia hata kwa kumuangalia tu hakuna hanachokifahamu kuhusu ili furushi ...........kwa hiyo beba furushi lako na uwekwe ndani......ndio mwana kuachiwa maana alikuwa kama akili isharuka tayari aelewi
 
Hehe kuliko kutoa 200m si heri wangewasaidia famili ya mtuhumiwa tu ye wamwache huko ndani. Si sawa kabisa 200m ukalipe kwenye plea bargain unless uwe kweli umecommit a crime
Freedom ya mtu ni kubwa kuliko 200m, unasema hivyo sababu you are on the other side of the bars...ila freedom ikienda imeenda ila 200m zinatafutika, na kitu kingine hujui hawa jamaa wanaomlipia 200m wanauwezo gani....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…