Hatari ya kuwalazimisha watoto wa Watu kwenda JKT!

Watoto wa masikini wana stamina. Shida zimewakomaza hivyo ni rahisi kumudu mafunzo ya kijeshi tofauti na watoto wa rulling class. Huo ni mgawanyiko wa majukumu tu ndani ya jamii. No hatred. No malice toward anyone.
 
Ndio maana nimesema hii ishu ya kuwalazimisha watoto kwenda JKT ni zaidi ya uzezeta, ututusa na usengerema. Kwa hii serikali ya wezi, kama JKT ingekuwa na faida, ingejaa watoto wao tu. Lakini kwa kuwa haina faida yoyote huwa wanawasukimiapo watoto wa wakulima tu ilhali watoto wao wakila bata huko Masaki na Oysterbay.
 
Kwa kweli JKT inatakiwa libadilike na kulinda hai Vijana wanaotakiwa kwenda JKt. Iwe wakike na wakiume. Mpe Kijana shughuli Kwa Nia ya kujenga na sio kutweza utu wake. Huko sio kujenga Taifa Bali ni kubomoa Taifa
 
Man hakuna mwanamke mwenye chemistry ya ushupavu wa misuli

Wanawake walipewa feminine energy as Yin kama Tai Chi ya kukonkyua

Kukuta mwanamke anataka kudhihirisha misuli ni ufelia wa kiwango cha Juba
 
Wamejipoteza

Wanajitafuta wajipate ila muongozo hawana

Hata China wanafuga bata kama ng'ombe
 
Kwani wewe unataka madogo waendelee kuishi maisha ya mateso hadi lini mkuu?
Nidhamu ya ufanyaji kazi inatakiwa itiliwe mkazo, tusiwe na akili za kipumbavu za wale wazulu kule South Africa wanaoshambulia wageni kwa sababu ya umaskini wao.

Jeshi ni sehemu mojawapo muhimu katika kuiingiza akili yenye nidhamu kwa vijana wadogo. Hata hii akili ya kuleta maandamano yanayotajwa tarehe 7 July ni matokeo ya uvivu na ukosefu wa kazi.

Kijana mwenye majukumu fulani kwamba anaamka asubuhi anakwenda kufanya shughuli fulani hawezi hata kidogo kuunga mkono ujinga wa kuleta fujo zisizo na sababu.

Wale wahindi tuliosoma nao sekondari miaka ile ya 80 mwishoni na 90 mwanzoni pale Mzizima na Shaban Robert wamekuja kuwa mamilionea na mabilionea hawa kina Mo Dewji wakati sisi tuliosoma nao tunateseka mitaani. Sababu kubwa ni moja tu, nidhamu za kimaisha walizokuwa wakifundishwa majumbani mwao baada ya yale masomo ya shuleni.
 
Huna hoja mzee nchi zote hata hizo mnazosifia kama Israel na zingine zinahuu utaratibu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…