Hati ya Mashtaka dhidi ya Freeman Mbowe iliyotumiwa Julai 26, 2021

Huu ndio ukweli,hapo wasipoe kabisa,huku kesi ya Ugaidi inaunguruma huku makongamano ya katiba yanafanyika,watachanganyikiwa wenyewe
 
Hapana, hayo sasa hayana lazima tena.

Hawa wamekwishaingia ndani ya msitari, hakuna wigo tena wa kufanya kukurukakara za aina hiyo tena.

Mhimu ni kwa CHADEMA kutopoteza lengo tena jinsi watakavyo ihitimisha kazi hii muhimu ya kuliokoa taifa hili.
 
Na ndio maana walimkwepa kibatala wakakimbilia kumsomea mashtaka kimyakimya,subiri vichekesho vya maswali ya Kibatala mahakamani ndio utajua hao waendesha mashtaka ni vilaza
 
Mtu anayeandika "kama hawana makosa njoo utoe ushahidi" hata haelewi where the burden of proof lays!
 
Aache kulia lia na kututakia vikwazo, vikwazo vikiwekwa wanaoumia ni wananchi, yeye anakunywa bia huko ubelgiji. tena si ajabu hata kusali hasali. ukiangalia hati ya mashtaka, makosa yale yalifanywa soon before general election ya 2020. na kipindi kile kweli kuna baadhi ya sheli na maeneo mengine yalipigwa moto kama mabom hivi. selikali huwa inakuwa na ushahidi wa vitu vingi lakini inaamua kuweka pembeni ili kuangalia kama mkosaji hasa maarufu kama dj, kama ana adabu, wakiona analeta dharau, wanafungua tu file. mwaka jana walipanga kuvuruga kabisa hii nchi alimradi tu wachukue nchi.
 
Binafsi siioni kesi hapo Kwa jinsi TU ya uaandaaji wa charge sheet! DPP amefanya kosa moja kubwa la kiufundi ambalo ndilo lililotumika kuwatoa wale mashekhe wa uamsho nalo ni kushitaki nje ya eneo lilikotokea kosa! Ukisoma charge sheet inaonyesha makosa hayo anayotuhumiwa Mbowe yalifanyika Hai mkia wa Kilimanjaro ambayo Ina mahakama za ngazi zote zenye uwezo wa kusikiliza shauri hilo. Kwanini iletwe kisutu ambayo ni mkoa ambao matukio hayo hayakufanyika? Hii ni kasoro ya wazi ambayo inadhihirisha kuwa hakuna kesi hapo Bali kupotezeana muda TU na kuchafuana! Na mkumbuke kuwa Mbowe alikuwa ana kikao Cha Baraza kui kule Mbeya July 31 ya kuwavurusha wale COVID-19! Kwa vyovyote mihimili yote ilikuwa inakwenda kuaibika hivyo wamemshikilia ili kuikwepa aibu hiyo!
 

Hiyo wala sio kesi bali ni utoto
 
Hii inahusiana nini na kichwa chako cha habari?

Amandla...
 

Kweli nimeamini mtu skizeeka akili zinakuwa za kitoto. Kwa jinsi ccm iliyozeeka kwa sasa imejikuta inafanya mambo ya kitoto.
 
Basi aunganishiwe na mioto iliyotokea Kariakoo na kwenye mabweni.

Amandla...
 
Kesi ni kesi bro, hata kama umesingiziwa. Maana hata jela sio wote wana makosa.

Kesi na utoto ni vitu viwili tofauti. Huo uchafu wala hauna hata hadhi ya kesi ya kusingiziwa bali ni utoto, tena wa mijizee huko serikalini. Nyie ndio mnafanya wazungu waendelea kutuita manyani.
 
Ndipo hapo sasa nashangaa aliyekuwa accused anapewa onus of proof.

Huyu original poster anajua hata mantiki ya mashtaka inaendaje na nani anatakiwa kuprove?
Ndio huyu aliyepost. Hapo bado anakazania Lissu atoe ushahidi wa innocence ya Mbowe kwa sababu amepost akisema kuwa Mbowe anaonewa. Go figure.

Amandla...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…