Hatimaye Chief Godlove abambwa. Adaiwa kupost hela feki mitandaoni ili kuwahadaa watu kwamba ana hela

Wapo watu wanaotaka masifa
Ni sawa na kuwapa wasanii nyumba yako washutie movie

Ova

Come on chief, wasanii wanajulikana au mnaweza kubaliana malipo kwa namna fulani. Huwezi mpa mtu nyumba na gari yako bure kila siku, simjui huyu bwana wala simtetei ila something isn't adding up. Ili uwe karibu na watu wenye majumba na magari tena hadi kutumia mali zao utakavyo lazima uendane nao kwa namna moja au nyingie. Birds of the same feather .......
 
Wahuni tu hawa wanasababisha vijana wajione hawafai kisa hawana hela.
 
Itakua ni stori kubwa kwasababu asili ya masikini ni kuona mwenzao bado yuko kwenye umasikini kwahiyo kama alijidai tajiri na akashtukiwa hana pesa hiyo ni sherehe kwa maskini.
 
Itakua ni stori kubwa kwasababu asili ya masikini ni kuona mwenzao bado yuko kwenye umasikini kwahiyo kama alijidai tajiri na akashtukiwa hana pesa hiyo ni sherehe kwa maskini.
Masikini unawajua masikini wenzako vizuri sana🀣🀣🀣
 
Naipataje?
 
Kutoka FB

NJEMBA WA KINYAKYUSA AUMBUKA BAADA YA KUGUNDULIKA ANATUMIA MBAO KUWADANGANYA WATU KUWA YEYE NI MILIONEA.

Hatimae siku 40 zimemfikia jemba huyo pichani kwa jina la Chief Godlove kama anavyojiita mtandaoni. Jamaa ni Mnyakyusa wa Mbeya na mara zote amekuwa akijitapa kuwa yeye ni milionea lakini pia amejiunga na chama cha Freemason.

Kwenye video zake za Instagram na Tiktok amekuwa akijigamba kwa kununua pombe za bei ghari na kuzimwaga kama maji, lakini pia amekuwa akijinadi kuwa yeye ni mnyakyusa wa kwanza kujiunga Freemason na kumiliki pesa za maana, amekuwa akiwatukana wanaume ambao bado hawajafanikiwa kimaisha kuwa wao ni sawa na wanawake tu.

Sasa siku ya jana kupitia ukurasa wake wa Instagram na Tiktok aliposti video akiwa ametandaza mamilioni ya pesa na kuendelea kujinadi kama kawaida yake. Macho ya walimwengu yalifanikiwa kupenya na kufanikiwa kugundua kuwa jamaa huyo kumbe ni tapeli wa kutupwa. Anachokifanya anachukua mbao anazichonga usawa wa noti ya elfu 10, anazipaka rangi ya pink kisha anaweka noti ya elfu 10 juu na chini ambapo usipoangalia kwa umakini unaweza dhani ni bunda la pesa kiasi cha milioni tano.

Baada ya kuumbuka tapeli huyo wa kienyeji ameendelea kujitetea kwa maneno dhaifu na kupokea matusi mfululizo kutoka kwa Wananchi.
 

Attachments

  • FB_IMG_1696249539369.jpg
    41.8 KB · Views: 5

Duh!
Ova!
 
Mi nilidhani amebambwa na mkono wa sheria kwa tuhuma za kihalifu, kumbe ni dhania ya rangi ya picha za noti!

Na anazozitawanisha akizichezea kwa kuzirusha rusha nazo siyo pesa?

Maana yake kupata noti moja nyekundu kwa kufanya kibarua kwa mtu, kibarua hicho hauwezi kukimaliza kwa siku moja, ndipo ilipo thamani ya pesa.

Mimi sielewi mantiki ya kusema mtu hana hela ama hela za bandia huku katandaza mihela chumba kizima huku akizichezea kwa kiburi na majigambo!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…