Hatimaye kikokotoo chalegezwa, Serikali imepandisha Malipo ya Mkupuo kwa Wastaafu kutoka 33% hadi 40%

Monthly pension itashuka sema waliobeza kikokotoo hawajielewi kuwa kadri unavyochukua Hela ya mkupuo kubwa monthly pension inashuka na Maisha ni monthly pension sio Hela ya mkupuo

Hela ya mkupuo hukata upesi
Hiyo ya mkupuo kama huwezi hata kujenga, utaweza jenga lini tena kwa kutumia monthly pension? Warejeshe tu kikokotoo cha swali. Pia ni wajibu wa mifuko kuongeza monthly pension kwa kadri maisha yanavyozidi kupanda.
 
Sahihi Maisha ni monthly pension Sio mkupuo Kwa umri wa miaka 60 monthly pension ya muhimu sana Kwake kuliko mkupuo
 
🤣 sure
 
Hiyo ya mkupuo kama huwezi hata kujenga, utaweza jenga lini tena kwa kutumia monthly pension? Warejeshe tu kikokotoo cha swali. Pia ni wajibu wa mifuko kuongeza monthly pension kwa kadri maisha yanavyozidi kupanda.
Pension kazi yake Sio kujenga nyumba kama hukujenga ndio maana ulaya na marekani wazee miaka 60 hutaka monthly pension zao ziende nyumba za kulea wazee mstaafu huenda kuishi huko na huhudumiwa Kila kitu kuanzia chakula malazi,matibabu ,mavazi nk ili asisumbue ndugu nk kuwa akistaafu Hela inaishia kujenga nyumba na kuaanzisha vimiradi Koko vya kumpa presha afe haraka

Miaka 60 ndio unajenga nyumba na kuanzisha biashara akili kichwan zimo wewe? Una uhakika zimo ? Wewe umri huo ni WA kuishi na monthly pension tu
 
Wewe inaonyesha huna kabisa hata ndugu walio ajirikuwa serikalini! Mtumishi kama mwalimu ana marupurupu gani ya kujiwekea kimaisha?
Usichukuliwe watumishi wote wana fulsa za marupurupu! Kuna watu toka aagiriwe hadi anastaafu hajapata safari hata moja ya kulipwa na serikali! yeye ni mshahara tu, mshahara wenyewe wa serikali, mtumishi aliye soma na kupanda cheo cha mwisho juu hazidi milioni 2 na kidogo! Hapo unawatoto wanasoma, ndugu wategemezi nk. Unajiwekezaje hapo?
Hoi ndio sababu ya kutegemea malipo ya mkupuo kujiandaa na maisha ya kustaafu!
 
Kuna mstaafu ulimuona analalamikia hicho kikokotoo cha zamani? Au ni nyinyi wenyewe tu ndiyo mliamua kuzikwapua hela za michango ya wafanyakazi na kufanyia mambo yenu mengine nje ya utaratibu?
Waliostaafu Kwa kikokotoo Cha asilimia 33 au 25 nani ulimsikia akillalamika ? Wanaolalamika ni wale wanaotarajia kustaafu wasiojua lolote wanadanganyana huko maofisini kwao

Hicho kikokotoo Cha kulipwa asilimia 40 mtu akistaafu atashangaa akienda mtaani au kijijini kuona mtu aliyestaafu Kwa kikokotoo Cha asilimia 33 au 25 analipwa monthly pension kubwa kuliko aliyechukua mkupuo asilimia 40

Ukisikia maisha fainali uzeeni ni pamoja na kiwango Cha monthly pension Sio mkupuo
 
Ni kama mchezo wa draft ukizubaa na kete kuna jamaa anaingia kingi...
Sahihi hao waliodai kikokotoo Hela ya mkupuo ipande kiwango kipande hawajielewi kuwa monthly pension itakuwa ndogo

Mchezo wa draft umewashinda
 
Hivi wale watumishi wa zamani "Permanent and pensionable" waliokuwa wanalipwa na Hazina laki na kelele ikapigwa sana hadi Mwigulu akatoa tamko bungeni kuwa Juni jibu litatolewa wameshafikiriwa budget hii? Na hapaswi kusahau kuwa hawa wanalipwa na wizara yake Hazina.
 
Tatizo la kikokotoo siyo hizo asilimia peke yake, bali limeanza na fomula ya mwanzo ya kufikia hizo asilimia. Badala ya 1/540 waliweka 1/580 na badala ya miaka 15.5 wakaweka miaka 12.5. Kimahesabu hizo namba zinashusha kiwango cha pensheni. Kwa hiyo hata hiyo asilimia 40% ni siasa tu...!!!!
 
Hapo ndipo anayejua anajua kuwa hajui
 
Why umlazimishe mtu kumshikia hela zake?
Kwani amelukwa na akili na je kuna aliezifuja hela zake akarudi kuisumbua serikali ama kudai? Matendo na sheria zingine zinatoa indicators kwa jamii na raia kwa ujumla kuwa serikali yetu imefilisika
 
Tatizo hamjui impact yake.
maana yake ni kuwa monthly pension inaenda kushuka.
shangilieni tu ila kale ka mwezi katapungua
 
Monthly pension itashuka sema waliobeza kikokotoo hawajielewi kuwa kadri unavyochukua Hela ya mkupuo kubwa monthly pension inashuka na Maisha ni monthly pension sio Hela ya mkupuo

Hela ya mkupuo hukata upesi
wanachekelea ujinga
tatizo mifuko haikuwa ikitoa semin na maelezo ya kina kuhusu kikokotoo walitangaza na kuacha kwenye makaratasi
 
usiongee kam mtu asiyesoma.
 
Ishu
Ishuke tu,mtu apewe hela yake yote ajue afanyie nini.
 
Monthly pension itashuka sema waliobeza kikokotoo hawajielewi kuwa kadri unavyochukua Hela ya mkupuo kubwa monthly pension inashuka na Maisha ni monthly pension sio Hela ya mkupuo

Hela ya mkupuo hukata upesi
Unaijua kesho na uliwahi kuiona?Kwa nini mstaafu asipewe nyingi hata kizazi chake kifaidi kuliko hiyo ya kila mwezi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…