Hatimaye kikokotoo chalegezwa, Serikali imepandisha Malipo ya Mkupuo kwa Wastaafu kutoka 33% hadi 40%

Hatimaye kikokotoo chalegezwa, Serikali imepandisha Malipo ya Mkupuo kwa Wastaafu kutoka 33% hadi 40%

Monthly pension itashuka sema waliobeza kikokotoo hawajielewi kuwa kadri unavyochukua Hela ya mkupuo kubwa monthly pension inashuka na Maisha ni monthly pension sio Hela ya mkupuo

Hela ya mkupuo hukata upesi
Hiyo ya mkupuo kama huwezi hata kujenga, utaweza jenga lini tena kwa kutumia monthly pension? Warejeshe tu kikokotoo cha swali. Pia ni wajibu wa mifuko kuongeza monthly pension kwa kadri maisha yanavyozidi kupanda.
 
Kuna mwalimu mmoja alichukuwa hii ya mkupuo, akakimbilia kujenga kijijini anakoishi, akagaiwa watoto kidogo na iliyobaki akawa ananywea pombe mpaka ikakata. Sasa hivi anaishi kimaskini kweli kweli. Nadhani huyo angepata hii ya kila mwezi ingemsaidia zaidi.
Sahihi Maisha ni monthly pension Sio mkupuo Kwa umri wa miaka 60 monthly pension ya muhimu sana Kwake kuliko mkupuo
 
Wajinga wanaostaafu Miaka 60 halafu wanadhani ndio mwanzo WA maisha wakistaafu wakati wamefanya KAZI serikalini au taasisi zake Miaka kibao wakiwa na mishahara na marupurupu kibao na heshima kibao na connection hawajufanya lolote la maendekeo kujipanga wakisubiri kustaafu

Mitaani MTU serikalini au taasisi zake akistaafu hata awe bosi anaonekana bwege Tu hakuna WA kumnyeyekea tena mitaani wala kijijini wala kujikomba kwake His or her glory days are over hata akigombea ujumbe wa nyumba Kumi aweza pigwa chini

Sasa kama kuna bwege mstaafu anategemea Kikokotoo kimtoe kimaisha mjinga hajielewi MTU umefanya KAZI Miaka yote hujatoka kimaisha unasubiri kikotoo jiandae kufa mapema Kwa frustration kama huna Cha maana ulijiandaa omba tu Hela ya mkupuo iwe ndogo ila monthly pension iwe kubwa ili Cha mwezi kiwe kikubwa

Nashauri kama mtaalamu
🤣 sure
 
Hiyo ya mkupuo kama huwezi hata kujenga, utaweza jenga lini tena kwa kutumia monthly pension? Warejeshe tu kikokotoo cha swali. Pia ni wajibu wa mifuko kuongeza monthly pension kwa kadri maisha yanavyozidi kupanda.
Pension kazi yake Sio kujenga nyumba kama hukujenga ndio maana ulaya na marekani wazee miaka 60 hutaka monthly pension zao ziende nyumba za kulea wazee mstaafu huenda kuishi huko na huhudumiwa Kila kitu kuanzia chakula malazi,matibabu ,mavazi nk ili asisumbue ndugu nk kuwa akistaafu Hela inaishia kujenga nyumba na kuaanzisha vimiradi Koko vya kumpa presha afe haraka

Miaka 60 ndio unajenga nyumba na kuanzisha biashara akili kichwan zimo wewe? Una uhakika zimo ? Wewe umri huo ni WA kuishi na monthly pension tu
 
Wajinga wanaostaafu Miaka 60 halafu wanadhani ndio mwanzo WA maisha wakistaafu wakati wamefanya KAZI serikalini au taasisi zake Miaka kibao wakiwa na mishahara na marupurupu kibao na heshima kibao na connection hawajufanya lolote la maendekeo kujipanga wakisubiri kustaafu

Mitaani MTU serikalini au taasisi zake akistaafu hata awe bosi anaonekana bwege Tu hakuna WA kumnyeyekea tena mitaani wala kijijini wala kujikomba kwake His or her glory days are over hata akigombea ujumbe wa nyumba Kumi aweza pigwa chini

Sasa kama kuna bwege mstaafu anategemea Kikokotoo kimtoe kimaisha mjinga hajielewi MTU umefanya KAZI Miaka yote hujatoka kimaisha unasubiri kikotoo jiandae kufa mapema Kwa frustration kama huna Cha maana ulijiandaa omba tu Hela ya mkupuo iwe ndogo ila monthly pension iwe kubwa ili Cha mwezi kiwe kikubwa

Nashauri kama mtaalamu
Wewe inaonyesha huna kabisa hata ndugu walio ajirikuwa serikalini! Mtumishi kama mwalimu ana marupurupu gani ya kujiwekea kimaisha?
Usichukuliwe watumishi wote wana fulsa za marupurupu! Kuna watu toka aagiriwe hadi anastaafu hajapata safari hata moja ya kulipwa na serikali! yeye ni mshahara tu, mshahara wenyewe wa serikali, mtumishi aliye soma na kupanda cheo cha mwisho juu hazidi milioni 2 na kidogo! Hapo unawatoto wanasoma, ndugu wategemezi nk. Unajiwekezaje hapo?
Hoi ndio sababu ya kutegemea malipo ya mkupuo kujiandaa na maisha ya kustaafu!
 
Kuna mstaafu ulimuona analalamikia hicho kikokotoo cha zamani? Au ni nyinyi wenyewe tu ndiyo mliamua kuzikwapua hela za michango ya wafanyakazi na kufanyia mambo yenu mengine nje ya utaratibu?
Waliostaafu Kwa kikokotoo Cha asilimia 33 au 25 nani ulimsikia akillalamika ? Wanaolalamika ni wale wanaotarajia kustaafu wasiojua lolote wanadanganyana huko maofisini kwao

Hicho kikokotoo Cha kulipwa asilimia 40 mtu akistaafu atashangaa akienda mtaani au kijijini kuona mtu aliyestaafu Kwa kikokotoo Cha asilimia 33 au 25 analipwa monthly pension kubwa kuliko aliyechukua mkupuo asilimia 40

Ukisikia maisha fainali uzeeni ni pamoja na kiwango Cha monthly pension Sio mkupuo
 
Hivi wale watumishi wa zamani "Permanent and pensionable" waliokuwa wanalipwa na Hazina laki na kelele ikapigwa sana hadi Mwigulu akatoa tamko bungeni kuwa Juni jibu litatolewa wameshafikiriwa budget hii? Na hapaswi kusahau kuwa hawa wanalipwa na wizara yake Hazina.
 
Tatizo la kikokotoo siyo hizo asilimia peke yake, bali limeanza na fomula ya mwanzo ya kufikia hizo asilimia. Badala ya 1/540 waliweka 1/580 na badala ya miaka 15.5 wakaweka miaka 12.5. Kimahesabu hizo namba zinashusha kiwango cha pensheni. Kwa hiyo hata hiyo asilimia 40% ni siasa tu...!!!!
 
Hapo ndipo anayejua anajua kuwa hajui
 
Why umlazimishe mtu kumshikia hela zake?
Kwani amelukwa na akili na je kuna aliezifuja hela zake akarudi kuisumbua serikali ama kudai? Matendo na sheria zingine zinatoa indicators kwa jamii na raia kwa ujumla kuwa serikali yetu imefilisika
 
Akiwasilisha Bajeti Kuu ya Serikali Bungeni, Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Nchemba amesema Serikali imesikia kilio cha Wastaafu na hivyo imepandisha Malipo ya Mkupuo kutoka 33% hadi 40%

Pia, Dkt. Mwigulu amesema Rais Samia ameagiza kuongezwa kwa malipo hayo kwa Wastaafu waliokuwa wakilipwa 25% sasa watalipwa 35% katika Mwaka huu wa Fedha

====

Pia soma: LIVE - Hotuba ya Bajeti Kuu ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025, leo Juni 13, 2024 Bungeni, Dodoma
Tatizo hamjui impact yake.
maana yake ni kuwa monthly pension inaenda kushuka.
shangilieni tu ila kale ka mwezi katapungua
 
Monthly pension itashuka sema waliobeza kikokotoo hawajielewi kuwa kadri unavyochukua Hela ya mkupuo kubwa monthly pension inashuka na Maisha ni monthly pension sio Hela ya mkupuo

Hela ya mkupuo hukata upesi
wanachekelea ujinga
tatizo mifuko haikuwa ikitoa semin na maelezo ya kina kuhusu kikokotoo walitangaza na kuacha kwenye makaratasi
 
Hii 40% (malipo ya mkupuo ya kiinua mgongo) bado haitoshi, serikali haijasikia bado, msitudanganye

Tunataka kikokotoo cha awali kabla hiki cha 33% kuanza kutumika.

Serikali iache wizi mara moja kuibia wastaafu fedha zao. Wabunge kama mnajipenda kwenye hili, kataeni pendekezo hili la serikali. Wastaafu Tunataka kikokotoo cha 50%. Otherwise tutajiunga na CHADEMA kuuwasha moto wa kuwakataa.!!

Serikali iache wizi wa kuiba kupitia kwa wastaafu na kufanyia anasa pesa zao!

Lipeni madeni ya Trl 4.6 mlizokopa kutoka kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii Ili wastaafu tulipwe malipo stahiki ya kiinua mgongo cha 50% kama awali kabla hamjaanza kuchota fedha za mifuko hii!!
usiongee kam mtu asiyesoma.
 
Ishu
Monthly pension itashuka sana waulize wastaafu waliolipwa mkupuo asilimia 25 wanaishi maisha ya Raha sana pension ya Kila mwezi hawapishani sana na walioko ofisini sababu monthly pension ni kama 75 percent ya mshahara walikuwa wanapata

Ukiweka asilimia 50 maana yake unataka monthly pension Yako iwe nusu ya mshahara uliokuwa Ukipata kazini haiko vizuri Kwa mstaafu

Binafsi ningepekeza wastaafu walipwe asilimia kumi tu mkupuo ili monthly pension Yao iwe asilimia 90 ya mshahara waliokuwa wakipata kazini

Lakini mtoto akililia wembe mpe ndicho serikalli imefanya
Ishuke tu,mtu apewe hela yake yote ajue afanyie nini.
 
Monthly pension itashuka sema waliobeza kikokotoo hawajielewi kuwa kadri unavyochukua Hela ya mkupuo kubwa monthly pension inashuka na Maisha ni monthly pension sio Hela ya mkupuo

Hela ya mkupuo hukata upesi
Unaijua kesho na uliwahi kuiona?Kwa nini mstaafu asipewe nyingi hata kizazi chake kifaidi kuliko hiyo ya kila mwezi?
 
Back
Top Bottom