Hatimaye ndoa yangu imevunjika

Hatimaye ndoa yangu imevunjika

Baba jayaron

JF-Expert Member
Joined
Jun 29, 2015
Posts
4,324
Reaction score
5,933
Asalaam,

Ndoa yangu ilikuwa nzuri saana kwasababu tulianza tukiwa vijana wadogo maskini, kutokana na hivyo tuli inspire vijana wengi na ndoa nyingi kusimamia.

Tuka barikiwa watoto wazuri. Mungu alitubariki na unafuu wa maisha wa kupata tunachokita kwa level ya maisha ya kawaida. Basi ghafla maisha yakabadilika nikaanza kupitia magumu kiuchumi hata jero mtihani kupata.

Balaa lilianza hapo kudharaulika, kununiwa, Visa vya kila aina mpaka hatimaye Mimi ndiye nikawa "mama wa nyumbani" na yeye akawa anarudi nyumbani ka guest house ni kulala tuu bila kujali hata watoto wana hali gani.

Biashara nimemfungulia mwenyewe, na hata kodi nimekua nikimsaidia kulipa. Pamoja sasa Sina shughuli maalumu lakini Mungu ananisaidia kumudu kutimiza mahitaji muhimu ya familia yangu.

Sasa amepata mwanaume mwingine na amenithibitishia na nilipohitaji aende kwao akapumzika akaniambia hawezi atabaki Dar aendeleze maisha yake kwakua anashida saana ya hela. Kumbe nia yake ni kuendelea kuishi na huyu mwanaume.

Leo nimethibitisha. Ndoa yangu haitakuwepo tena baada ya kukamilisha taratibu za kisheria.

Roho inauma kwakua sikutegemea kama wanangu wataishi na mzazi mmoja.

Wanaume tutafute hela, ndo thamani yetu!

#Mwanamkemkwelinimamayakotuu

1624427604959.png

 
Pole kwa yaliyokukuta mkuu! Huna budi kukubaliana nayo na kujipa muda siku utampata mama mwingine bora mtakayewalea watoto wenu pamoja kwa upendo, kuhusu pesa nadhani kuna wanawake wanaweza vumilia waume zao na kuwaombea Mungu aruhusu baraka za kipato ktk familia, si wote wanaonuna na dharau eti sababu mume amefulia.

Pia tujitahidi kuwa na vyanzo vingi vya mapato ili ukikosa huku unapata sehemu nyingine maisha yanaendelea. Itasaidia kuepusha kisirani
 
Mtihani wa kimaisha uliokupata umekusaidia sana kumfahamu aliyekuwa mkeo, bila huo mtihani hayo yote yasingefichuka.

Shukuru umepata la kujifunza, endelea kupambana mambo yatakaa sawa
 
Sasa umekua. Masingo father tuko wengi na maisha yanasonga. Kama ulivyosema cha muhimu ni kutafuta pesa na kuwekeza vizuri sehemu mbalimbali. Hata usipokuwa tajiri, mwanaume kuwa na uwezo wa kuwatimizia mahitaji ya msingi wanao pamoja na wewe mwenyewe ni muhimu sana.

Naam! Kwa sasa chapa kazi sana. Tunza hela zako. Walee wanao kwa upendo mkubwa wala usichukie wanawake wote. Hii ni changamoto tu unapitia. Na ukisimama imara katika misingi sahihi utashangaa hata huyu mtalaka wako akatamani kurudi huko mbele ya safari.

Mungu hatakuacha mkuu. Been there done that. I am rooting for you [emoji1545]
 
Pole sana mkuu, lakini mimi kaa mtaalamu wa mambo ya ndoa na mambo kaa hayo, nimesikia upande wako tu, siwezi kusema lolote kabla sijasikia toka kwa aliyekuwa mwenza wako, i mean your x, i am someone who never ever allows my emotions to overide my knowledge and intelligence, so ningependa sana kwanza kusikia toka kwa your x kabla ya kusema lolote, naona watu wanakupa pole, lakini mimi i came to conclusions and make rulings after i hear from both parties, its unfair to hear from only one side
 
Pole kwa yaliyokukuta mkuu! Huna budi kukubaliana nayo na kujipa muda siku utampata mama mwingine bora mtakayewalea watoto wenu pamoja kwa upendo, kuhusu pesa nadhani kuna wanawake wanaweza vumilia waume zao na kuwaombea Mungu aruhusu baraka za kipato ktk familia, si wote wanaonuna na dharau eti sababu mume amefulia.

Pia tujitahidi kuwa na vyanzo vingi vya mapato ili ukikosa huku unapata sehemu nyingine maisha yanaendelea. Itasaidia kuepusha kisirani
Nashukuru saana kwa ushauri hata hivyo Mungu mwema maana nilikua napitia mateso saana kwa huyu mwanamke Mungu ameniweka huru.

Kuhusu mke mwingine hapana wanangu ni wadogo saana
 
pole sana mkuu, lakini mimi kaa mtaalamu wa mambo ya ndoa na mambo kaa hayo, nimesikia upande wako tu, siwezi kusema lolote kabla sijasikia toka kwa aliyekuwa mwenza wako, i mean your x, i am someone who never ever allows my emotions to overide my knowledge and intelligence, so ningependa sana kwanza kusikia toka kwa your x kabla ya kusema lolote, naona watu wanakupa pole, lakini mimi i came to conclusions and make rulings after i hear from both parties, its unfair to hear from only one side
Your right japo nafasi hio sidhani kama unaweza kupata.

Ila jua sisi ni wakristo inapotokea mwenzako anasema ametoka nje ya ndoa sababu kutafuta faraja kwakua si mjali (kumtoa date) na yeye ana uhitaji mkubwa wa pesa or kwa sababu yeyote ile kutoka nje ya ndoa tunaamini si suluhisho.

Nilimwambia aande nyumbani kwao apumzike akasema hapana atapanga kumbe shida aendelee na hawara wake waishi pamoja kama sasa wanavyoishi
 
Dah pole sana mkuu, hakika una busara na hekima japo umepitia jambo zito ila hujaonesha dalili ya kumkufuru mungu wala kutokwa na matusi wala kupanga njama dhidi yao. Ila huwezijua mungu amekuepusha na nini kutoka kwa huyo mkeo, pengine mungu amekuepusha na maradhi au kifo (Kuuliwa Kwa Sumu n.k).

Kumbuka haya maneno yangu, huu mwaka hautoisha bila ya wewe kufanikiwa kimaisha kama utauvuka huu mtihani. Pia jiandae, ipo siku atarudi na kukupigia magoti huku akilia kama mtoto mdogo kwa makosa aliokufanyia.

Leo nimeamini ile kauli "Mke mwema ni kuku peke yake, kwasababu hulea vifaranga vyake bila kumtegemea wala kumsumbua kwa lolote jogoo".
 
Back
Top Bottom