Hatimaye ndoa yangu imevunjika

Hatimaye ndoa yangu imevunjika

Mkuu kila siku tunasema huku ila hukusikia.
hawa viumbe sio wa kuamini.
mwanamke akipata pesa....anawaza kuishi pekee yake ila mwanaume akipata pesa ..anawaza kuongeza wa kuishi naye.

wanawake wengi wana tabia inayofanana
 
Mhusika asije akawa kajinyonga kwa spana alizopigwa jaman. Anayemjua amchek tafadhali... maana loh
 
Your right japo nafasi hio sidhani kama unaweza kupata.

Ila jua sisi ni wakristo inapotokea mwenzako anasema ametoka nje ya ndoa sababu kutafuta faraja kwakua si mjali (kumtoa date) na yeye ana uhitaji mkubwa wa pesa or kwa sababu yeyote ile kutoka nje ya ndoa tunaamini si suluhisho.

Nilimwambia aande nyumbani kwao apumzike akasema hapana atapanga kumbe shida aendelee na hawara wake waishi pamoja kama sasa wanavyoishi
Pole Sana mkuu, kama huyo hawala alikuwa a najua uyo ni mke wa mtu trust me Ata muacha tuu uyo mkeo,.

mala nyingi sio mala zote watu wanao date na wake za watu huwa hawana malengo nao.

, pia hawana Imani nao kwakuwa Wana Pima kama ni mke wa jamaa na Ana nipa mimi time vip akiwa na mimi hawez kuwapa wengine?
 
Pole sana mkuu, lakini mimi kaa mtaalamu wa mambo ya ndoa na mambo kaa hayo, nimesikia upande wako tu, siwezi kusema lolote kabla sijasikia toka kwa aliyekuwa mwenza wako, i mean your x, i am someone who never ever allows my emotions to overide my knowledge and intelligence, so ningependa sana kwanza kusikia toka kwa your x kabla ya kusema lolote, naona watu wanakupa pole, lakini mimi i came to conclusions and make rulings after i hear from both parties, its unfair to hear from only one side
Hakuna kitu kinanikera kama mtu kujitambulisha ati "mtaalamu wa ndoa"! Seriously 🤣😂🤣! Mtaalamu wa ndoa 😂🤣😂!? You 're serious joking 😡!
 
Kama wewe uko matured na umekutana na matured woman be thankful. Kuwa ndoani miaka 10 si sababu kwamba sijui nini. Kwani hatuwaoni ndugu zetu ama?

Acha kutetea ujinga wa wavulana. Wanawake wnawavumilia miongo na miongo tu for the sake of their kids. Usijifananishe akili zako na wavulana. Bye
Huyu hajui ndoa yaweza kuvunjika Hadi uzeeni mwache ajishaue tu, Kuna ndoa ya mke 65 na 75 mume imevunjika na talaka juu
 
Pole kwa yaliyokukuta mkuu! Huna budi kukubaliana nayo na kujipa muda siku utampata mama mwingine bora mtakayewalea watoto wenu pamoja kwa upendo, kuhusu pesa nadhani kuna wanawake wanaweza vumilia waume zao na kuwaombea Mungu aruhusu baraka za kipato ktk familia, si wote wanaonuna na dharau eti sababu mume amefulia.

Pia tujitahidi kuwa na vyanzo vingi vya mapato ili ukikosa huku unapata sehemu nyingine maisha yanaendelea. Itasaidia kuepusha kisirani

@financial services nikuambie tu mama kua...
Huwezi kuigiza unanjaa wakati umeshiba,na huwez kuigiza umeshiba wakati unanjaa
Kuna wakati unajisahau unarud kwenye hari yako harisi
Leo hi utasema atapata mtu mwingine atakae kubali hali zote
Ila kumbuka haya unasema leo!
Mambo haya hayana format
Muhimu kuishi tu
 
Asalaam,

Ndoa yangu ilikua nzuri saana kwasababu tulianza tukiwa vijana wadogo maskini, kutokana na hivyo tuli inspire vijana wengi na ndoa nyingi kusimamia.

Tuka barikiwa watoto wazuri. Mungu alitubariki na unafuu wa maisha wa kupata tunachokita kwa level ya maisha ya kawaida. Basi ghafla maisha yakabadilika nikaanza kupitia magumu kiuchumi hata jero mtihani kupata.

Balaa lilianza hapo kudharaulika, kununiwa, Visa vya kila aina mpaka hatimaye Mimi ndiye nikawa "mama wa nyumbani" na yeye akawa anarudi nyumbani ka guest house ni kulala tuu bila kujali hata watoto wanna hali gani.

Biashara nimemfungulia mwenyewe, na hata kodi nimekua nikimsaidia kulipa. Pamoja sasa Sina shughuli maalumu lakini Mungu ananisaidia kumudu kutimiza mahitaji muhimu ya familia yangu.

Sasa amepata mwanaume mwingine na amenidhibitishia na nilipohitaji aende kwao akapumzika akaniambia hawezi atabaki Dar aendeleze maisha yake kwakua anashida saana ya hela. Kumbe nia yake ni kuendelea kuishi na huyu mwanaume.

Leo nimedhibitisha. Ndoa yangu haitakuwepo tena baada ya kukamilisha taratibu za kisheria.

Roho inauma kwakua sikutegemea kama wanangu wataishi na mzazi mmoja.

Wanaume tutafute hela, ndo thamani yetu!

#Mwanamkemkwelinimamayakotuu

Mapenzi hayalazmishwi ukiona hivyo jua huyo hakua mtu sahihi kwako,mana unaweza lazmisha mwishowe ukapata kesi ya murder
 
@financial services nikuambie tu mama kua...
Huwezi kuigiza unanjaa wakati umeshiba,na huwez kuigiza umeshiba wakati unanjaa
Kuna wakati unajisahau unarud kwenye hari yako harisi
Leo hi utasema atapata mtu mwingine atakae kubali hali zote
Ila kumbuka haya unasema leo!
Mambo haya hayana format
Muhimu kuishi tu
Kwahiyo baba angu unamaanisha hatuwezi kuwavumilia mkiwa hamna pesa? Tupo na nyie for money tu? 🤔
 
Nina rafiki yangu wa karibu, sio kuhadithiwa ni kushuhudia, alifanyiwa vituko hivo vya kufanya tendo la ndoa mpaka siku za hedhi kwa miezi 8 mfululizo. Siku walipoachana yule mwanamke akamtumia kipimo chake alichopima miezi 8 nyuma cha HIV kikisoma ameathirika pamoja na tarehe. Na akamuambia hakuanza dose za ARV kwa makusudi ili amgawie na yeye hayo maradhi.

Jamaa alichanganyikiwa akawa anaongea peke yake, ndugu na marafiki ilibidi tusaidiane kumpeleka kwa daktari wa saikolojia akatibiwe. Dokta alifanikiwa kumshawishi apime ili ajitambue kama ni muathirika aanze kutumia dawa, baada ya kupima kipimo kilitoka HIV NEGATIVE. Baada ya mwezi mmoja akapima tena akakutwa HIV NEGATIVE. Baada ya miezi mitatu akapimwa tena akakutwa HIV NEGATIVE.

Na yeye akamtumia vipimo vyote yule aliekua mke wake, haikupita miezi mitatu yule mwanamke alikonda na kuwa kama mdoli.

#Mungu yupo, halali wala hapumziki, na anawalinda waja wake kwa njama mbaya.
Mkuu kumbe ARV ni kweli inazubaisha virusi? Hata pakitokea mchubuko?
 
Pole Sana mkuu, kama huyo hawala alikuwa a najua uyo ni mke wa mtu trust me Ata muacha tuu uyo mkeo,.

mala nyingi sio mala zote watu wanao date na wake za watu huwa hawana malengo nao.

, pia hawana Imani nao kwakuwa Wana Pima kama ni mke wa jamaa na Ana nipa mimi time vip akiwa na mimi hawez kuwapa wengine?
Sure namsikitikia saana, na bado wapo wote hata sasa
 
Pole Mkuu,

Nimepitia hayo miaka michache iliyopita, awali nilikuwa na hofu ya Maisha yajayo hasa kwa upande wa watoto.
nilikwenda Mahakamani na walinishangaa kwamba mwanaume anaomba kumtaliki mke, sasa niko huru.Na uchumi umefurika mpaka nashangaa kwa nini sikufanya maamuzi haya tangu 2015 huko. Upande wa pili mbali ya kazi ya serikali, biashara na wanaume wa hapa na pale lakini naona yuko hoi!

mchungaji wangu, alisema "hakuna kipindi kigumu kwa mwanadamu kama kutafuta mtu wa kuishi naye kwani waweza chagua rafiki wa maisha yako au msalaba wako"

nyakati hizi za uchumi mgumu, ndoa nazo ni ngumu
I hope nami nitakuja kusimulia hiki baadae thanks kwakuntia moyo
 
Jiandae, ukifanikiwa kuimarika kiuchumi tena, atakuja akiomba radhi kwa jicho legevu na machozi mengi, sura yenye huruma na kukwambia ni shetani tu alimpitia!

Nakumbuka miaka kadhaa iliyopita, kaka yangu alilazimika kuvunja nyumba yake bila kupenda!

Wakwe zake walikuwa na ngumu ya maisha, walitaka kuuza shamba ili wanunue bati,(nyumba yao ilikuwa mbovu sana, enzi hizo ni Kijiji,Mlowo Mbozi mkoani Songwe,wakati huo ni Mbeya)

Baada ya wakwe kufanya hesabu wakabaini pesa ya shamba haitoshelezi idadi ya bati wanazohitaji, wakamuomba brother, awanunulie bati then wampe shamba!
Brother kuonyesha ukidume akawanunulia bati, mbao, misumari na fundi akamlipa (wakamshukuru mno na kumuona mkombozi wa familia kwani kwa bei ya shamba kwa wakati huo wasingeweza kununua vyote hivyo).

Baada ya miaka mingi kupita, lile shamba liligeuka Lulu, kwani thamani yake imekuwa kubwa kiasi kwamba watu walikuwa wanatoa offer za mamilioni, kwani palifaa sana kwa biashara, baba mkwe hakuwa na shida alikuwa ameshahamia mashambani huko...

Shida ikawa mke wa brother na mama mkwe, walipata tamaa baada ya tajiri mmoja kuwaambia atapanunua kwa Million 80, wakaliamsha dude wanataka sehemu yao, ndani pakawa hapakaliki, brother ajanusurika kuuawa kwa kuwekewa sumu na mkewe, (hapo walikuwa na watoto 3)

Shem alipogundua issue ya sumu imeshtukiwa aliamua kutoroka kuelekea kusikojulikana,brother kwa hasira aling'oa tofali zote,bati zote akaacha kiwanja tu, mke aliporudi hakukuta nyumba,maajabu zaidi ni jamaa aliykuwa tayari kununua lile eneo alifariki kwa ajali ya gari (hiece ilikuwa inaitwa MTIMA, iliua abiria wote)

Shem akakosa pa kuishi, bro akaanza kujenga upya sehemu nyingine, na huo ndiyo ulikuwa mwanzo wa mpya wa maisha yake.
Wanawake wengi ni wapumbavu
 
Mtihani wa kimaisha uliokupata umekusaidia sana kumfahamu aliyekuwa mkeo, bila huo mtihani hayo yote yasingefichuka.

Shukuru umepata la kujifunza, endelea kupambana mambo yatakaa sawa
👏👏
 
Kisasi muhimu sana ,huyo mwanamke na bwanake hutakiwi kuwaacha kirahisi hivyo. Mungu atakulipia kwa wakati wake na wewe unawalipisha madhambi yao now. Pole sana
 
Back
Top Bottom