Ngoja nikueleze kitu kimoja chepesi kama wewe ni mtu wa reasoning utanielewa na kujua hatari iliyopo mbeleni .vitakuja vyama vyote afrika hii unavovijua ila ccm kutoka ni ngumu mno! infact ni chama cha 10 duniani kina mchango mkubwa sana kwenye siasa za afrika, kama unasubiria kitoke aisee we andaa tu sehem ya kuzikwa
Huyo mwanajeshi kazungumia moja ya vitu ni kodi mpya za mawinga, mimi binafsi neno uwinga nililijulia mitandaoni katika kudadisi nikagundua winga ni kama "mtu wa kati/kiunganishi" katika ufanyaji biashara yaani winga anaunganisha muuzaji na mnunuzi huku yeye akijipatia pato dogo kama commission baada ya mauzo , ni majuzi hapa tumesikia TRA wameanza kuwapiga hao mawinga kodi katika kutafiti niligundua kuna hasira imejaa maana uwinga ilionekana kama kifuta jasho kwa watu waliohitimu shahada wengi wamejishikiza huko kujipatia riziki zao huku wakijipanga na masuala ya ajira .
Ok nimeelezea point ya uwinga , nikija point ya pili serikali hiyo hiyo imeanzisha kodi za biashara mitandaoni na ndio serikali hiyo hiyo inafungia mitandao sasa unafikiri kwa mfano leo naambiwa YouTube iko blocked ni watu wangapi hiyo ndio ofisi yao na wamepoteza mapato kiasi gani leo sababu ya watu wanaozuia kapteni Tesha asiongee?
JamiiForums kuna watu walikuwa wanapata vipato vyao humu tangu September 6 imefungiwa bila sababu zenye mashiko nikimnukuu Melo anasema traffic imepungua kutoka milioni 4 hadi 1 kwa siku je watu wangapi humu ndio ofisini kwao wamepoteza pesa hizo kodi wanalipaje tena? halafu wanaona watoto wa viongozi wananua vigae kwa bilioni 2.4 na wengine wameshika madola ambayo hawajayahangaikia kihalali wanawaonyesha dole la kati unafikiri vijana wachakarikaji wanapata ujumbe gani?
Ukiangalia katika kampeni za Samia ni wapi aliongea kwa uchungu na kuonyesha nia ya dhati kupambana na ufisadi kutokana na taarifa ambazo tunaziona mtandaoni jibu ni hakuna bali ndio kwanza anataka kuwazima wanaozileta na kuonyesha nchi inavyohujumiwa.
Pia kwa kukusaidia huyu Tesha na Polepole wataendelea kusikilizwa kwa umakini na watu wengi sababu wanaongelea mambo yanayowagusa wananchi moja kwa moja na sio hadaa tunazosikia katika hayo matamasha yanaitwa kampeni na kupitia hivyo tu ndio tunarudi katika ile kauli wananchi wakiamua jambo lao hawashindwi hivyo mnapaswa kuiona hatari sana pale wananchi wanapokuwa wanaona ni upande upi unawasikiliza na upi umewapuuza.
Mimi hili ndio jibu langu la mwisho kwako kama hujaelewa sina mifano zaidi.