Richard
JF-Expert Member
- Oct 23, 2006
- 15,692
- 23,038
Bila kupiga chenga naingia kwenye mada na leo nazungumzia kujitambua kwa wanachama na wapenzi wa CHADEMA.
Mara kadhaa nimekuwa hapa JF nikiuponda upinzani khasa CHADEMA kwamba wapo kuisindikiza CCM kwenye siasa tangia mwaka 1992 upinzani ulipozaliwa rasmi kwa maana ya vyama vingi vya siasa.
Pia katika mara zote hizo nimesisitiza kwamba upinzani wapaswa kujitambua kuwa ni mwelekeo upi ni sahihi kwao ama wa kusindikiza na kulambishwa asali au kuwa upinzani wa kweli usonunulika na usotishika na yale yote yanoendelea katika nchi hii.
Juzijuzi nikaja na ushauri kwa mara ingine tena nikisisitiza CHADEMA kujitambua na kuwa tayari kufanya mabadiliko mazito khasa kwenye uongozi wake.
Pia nikashauri kiongozi wa juu wa sasa yaani Mwenyekiti wa taifa mheshimiwa Freeman Mbowe kuketi pembeni na kuwa mshauri wa chama hicho ili kumpisha mwanachama mwenzao Tundu Lissu awe mwenyekiti wa chama hicho taifa.
Sina mengi ya kusema juu ya CHADEMA na endapo kitamchagua Tundu Lissu kuwa mwenyekiti wao wa taifa isipokuwa pongezi zangu za dhati kwamba ushauri wangu umewafikia CHADEMA na wameamua kufanya mabadiliko ya kweli.
CHADEMA kimepoteza jukwaa rasmi la kisiasa kutokana na madhila inofanyiwa na vyombo vya serikali hususan polisi na idara ya Usalama na makundi mengine ya wahuni wanolipwa ujira uchwara kwa kazi chafu.
CHADEMA kupoteza wigo, jukwaa na nafasi ya kisiasa kwaletwa na serikali na chama kinotawala cha CCM ambacho wanachama wake wengi khasa vijana wa chama hicho kuendesha kampeni ya kutia hofu wananchi na wale wenye kutaka mabadiliko. Hadi leo hii haifahamiki vijana wa CHADEMA akiwemop Soka wapo wapi na ni serikali mpya na makini itayoptikana kutoka upinzani ndo itayokuwa na nafasi kubwa ya kuwaeleza wananchi walipo watanzania hao walotekwa, kupotezwa au kushikiliwa maeneo fulanifulani ya ncih hii.
Leo hii nchini Syria na Bangladeshi kumegunduliwa maelfu ya makaburi ambayo wananchi wa nchi hizo khasa wale wanaharakati za kisiasa walikuwa wametekwa na kupotea kwa miaka kadhaa. Nchini Bangladeshi watu wasojulikana walikuwa na jukumu la kuwateka raia na kuwasweka katika magereza ya siri ili tu kuhakikisha kiongozi wao nchi hiyo Sheikh Hasina ambae leo hii aishi uhamishoni India habugudhiwi.
Lakini siasa ni sehemu ya maisha na pia ni wakati wa kuwapa wananchi nafasi ya kusema watakacho ilimradi hawavunji sheria kama katiba ya nchi inavyosema. Katiba ya nchi yatoa haki ya uhuru wa kutoa maoni kama sehemu ya haki mbalimbali ambazo raia wa Tanzania wanazo.
Baada ya tukio la leo la Tundu Lissu kuchukua fomu ningependa kuvishauri vyombo vyote vya usalama nchini kumuacha Tundu Lissu afanye siasa kwa uhuru. Vyombo hivyo vitulie vimuache azungumze na wananchi akijaribu kugombea nafasi ya uenyekiti na baadae akiongoze CHADEMA katika uchaguzi mkuu wa uraisi mwaka 2025.
Vyombo vya ulinzi na Usalama vitambue (maana bado hawajajitambua) kwa nao ni sehemu ya watanzania na pia wana familia na ndugu ambao wengi ni waathirika wa masuala mengi kama mfumuko wa bei, maisha kuwa magumu, ukosefu wa ajira kwa wahitimu wa vyuo vikuu na mengine mengi.
Ningependa pia kutoa ushauri kwa waziri wa Mambo ya Ndani mheshimiwa Bashungwa kuwa weye una uwezo wa kiakili na umesoma. Litakuwa ni jambo la kheri endapo utafanya mabadiliko ya kistratejia juu ya uendeshaji wa jeshi la polisi. Jeshi la polisi lipo kulinda raia na mali zao.
Hatuwezi kuwa jeshi la polisi ambalo latumia fedha za walipa kodi wa nchi hii kutumia vyombo vya serikali kama magari kwa shughuli kama za kuteka watu hovyo mabarabarani. Ikumbukwe kuwa mafuta, vipuri na na magari hayo vyote huhitaji kugharamiwa matengenezo na matumizi kwa ujumla, hivyo ni jambo la uzuri kama fedha zilopangiwa bajeti ya wizara na kupitishwa na bunge zikatumika kuboresha mafunzo ya jeshi la polisi na kuwekeza katika kufungua vituo vya kisasa vya jeshi la polisi.
Ushauri mwingine ni kwa idara ya usalama wa Taifa ambayo nayo mara kadhaa nimetoa ushauri wa namna ya kuifanyia mabadiliko idara hii ambayo kazi yake ya msingi kabisa ni kulinda nchi isidhuriwe na majasusi wa nje kwenye maeneo mengi kama rasilimali, miundombinu, uchumi, jamii ya watanzania (social engineering), usalama wa chakula na mengine mengi tu. TISS ijinasue kutoka katika kujikita kutafuta wanaharakati za kisiasa kama digidigi bali kuchambua kutumia muda mwingi kujifunza mambo mapya yanoisumbua dunia leo ambayo yataweza kuiathiri nchi yetu katika kila nyanja.
Ushauri kwa CCM ni kuwa tayari kuwasikiliza CHADEMA na kujifunza kujibizana kwa hoja, hizo ndo siasa za kistaarabu. CCM ipo madarakani kitambo sana lakini kila inaposikia wanokisema CHADEMA huhamaki na kutoa kauli ambazo hazijengi. Ni wakati wa kujifunza kusoma hoja mstari kwa mstari na kuzijibu kisomi. Siasa za kutishana na kutoleana maneno machafu si siasa bali ni ujinga.
Tukirudi kwa CHADEMA ni kwamba huu ndo wakati muafaka kwenukufanya siasa za kweli zisizompamba mtu wala kulambishwa asali. Huu ni wakati wa kufikiria kushinda uchaguzi wa 2025 kutengeneza manifeso na kuanza kukutengeneza kampeni na kufuata njia (tracking to win). Huu ndo wakati wa kutafuta udhaifu wa wagombea wa CCM (finding vulnerabilities) na kuzuia wagombea wa upinzani wasichaguliwe tena (stopping incumbet re-elected) na kulenga kupata kura nyingi majimboni.
Ufikapo wakati wa kampeni itakuwa ni nafasi kwa CHADEMA kufanya kampeni kisasa kwa kumuajiri meneja mwenye uzoefu na mtu wa stratejia ili wasadie kazi hiyo ikiwemo kufungua ofisi ndogo za CHADEMA na kutengeneza vipeperushi vinoeleza makusudio ya wagombea katika uchaguzi huo.
Mwisho ni kuhakikisha CHADEMA inajinyakulia jukwaa la siasa (twaita ground game).
Ground game ni nini?
Kisiasa huu ni uwanja wa kufanya siasa na si uwanja wa sungura kukimbizana huku na kule. Ni pale CHADEMA kinapokuwa kwa umakini kikieleza aina ya siasa na stratejia inakusudia kufanya. NI jambo la uziri kuona leo kumefanyika mahojiano katika Power Breakfast ni hii ni moja ya "ground game". Mitandao ya kijamii ni ground Game na vyombo vya habari vya kimataifa pia na ground Game.. Hivyo kushinda viwanja hivi hakuhitaji lelemama, bali ufanisi, mikakati sahihi na watu wenye kujitambua.
Mwisho napenda kuwapa kongole wanachama wa CHADEMA kwa maamuzi magumu na kuwa tayari kufanya siasa za kweli. Ukifanya siasa za kweli wananchi wataamka na watawaunga mkono.