Hatma ya Muslim University of Morogoro na Maono ya Aga Khan kuwasaidia Waislamu kujenga Chuo Kikuu

City...
Hapana hilo ndilo jibu lake sijakwepa.
Ikiwa wewe hukulipenda jibu hili mimi sina jibu lingine.

Ikiwa hukupendezewa na huo waraka ni bahati mbaya kwako.

Muhimu ni kuwa waraka huo ni sehemu ya historia ya Waislam wa Tanzania.
Mzee Said, waraka nimeusoma na kuuelewa. Lakini, haujibu swali hilo uliloulizwa. Ukweli ni kwamba hakuna ubaguzi wowote wa kidini unaofanywa na NECTA. Hasa katika nyakati hizi.
Uwezo wa mwanafunzi ndiyo utampeleka mbele au la, safari yake itakoma.
 
Sawa. Sasa mzee, kwanini Bakwata haijajenga chuo chochote?
Au la, kwanini hamjaanzisha taasisi mbadala wa EAMWS ili mtimize mpango uliokuwepo. Kama shida ilikuwa Nyerere na serikali yake, alikoma kuwa rais miaka takribani 40 iliyopita.
City...
Inaelekea wewe ni mgeni katika historia hii.

Usipate tabu.

Bakia hapa hapa Jukwaa la Historia na usome post za nyuma.
 
City...
Ikiwa unaona hapakuwa na ubaguzi yote sawa.
 
Shida ya waislam wao main focus yao ni dini, kwa hio hata kwenye taasisi zao ni mwendo wa kufocus na dini tu
 
Tunataka tufundishwe kufuga majini na kuroga kwa albadili
 
Haya ndiyo huyu mfiadini mjahidina Mohamed Said hataki kusikia. Ila ukweli ndiyo huwo
 
Huyu mzee anapaswa awahimize wenzake kwamba:-

Wapeleke watoto wao shule Bora na vyuo Bora hio ndio harakati muhimu anayopaswa ifanya wakati huu.

Ili kupata jamii ya waislamu wasomi kutosha kwenye soko la Ajira.

Haya makelele yao ya sijui walionewa sijui wanaonewa Kilikwenda kilirudi ni time wasting campaign. At the same time wakristo wanapeleka watoto shule Bora na vyuo hadi nchi za nje kwa wingi.

Waache hizi mbanga zao hazitowasaidia.

Alhaj Ally Hassan Mwinyi aliwahi waambia hivi hivi pelekeni watoto wakamnasa kibao kwenye vikao vyao walivyomualika wenyewe.

Shida inaanzia kwao siku zote.
 
Zanzibar ni shida.

Nina mchumba wangu aliwahi fundisha field huko anakuambia shuleni wakija hawafiki saa tisa jioni

Saa Tano washasepa

Ijumaa ndio hawaonekani kabisa.

Class ndio kabisa vilaza wa kutupwa.
 
Mangungo II,
Naomba nikufunze uandishi na heshima katika mjadala.
Kwanza mjadala nia yake ni kuelimishana si kutoleana kejeli na jeuri.

Mathalani ungeweza kuandika hivi:
''Mzee angewahimiza Waislam kuwapeleka watoto shule.''

Hapo nimeondoa, ''Huyu Mzee.''

Sentensi ina maana ile ile iliyokusudiwa lakini kuna adabu na kuheshimiana.

Unasema, ''Haya makelele...''
Haipendezi si uungwana.

Mimi sipigi kelele na haiwezekani niwe napiga kelele kwa ilm ya somo hili ninavyoijua.

Nataka nikuambie kitu kuwa Waislam si kama unavyowaeleza.

Waislam wamepigania uhuru wa Tanganyika hadi umepatikana kwa salama.

Wameishi na Nyerere ndani ya majumba yao wakati Nyerere hana ndugu mjini Dar es Salaam.

Wametaka kujenga Chuo Kikuu 1968 serikali ikavunja taasisi yao.

Waislam si watu wa leo akasimama mtu ati anawaeleza umuhimu wa elimu na kuwapeleka watoto wao shule.

Hii ni kejeli kubwa.

Watu waliokuwa wanajenga Chuo Kikuu hawahitaji kuhimizwa kuhusu elimu.

Waislam tuna historia ya kutukuka na mimi nimeiandika na inasomwa kwingi ndani na nje ya mipaka ya Tanzania.

Nimeizungumza historia hii kwa mialiko katika Vyuo Vikuu na katika media ndani na nje ya Tanzania.

Nimeandika '' research papers'' kadhaa na zimechapwa katika academic journals.

Mimi niko hapa kazi niiyojipa ni kusomesha historia ya kweli ya nchi yetu ili watu waifahamu.

Hii ndiyo sababu nakuandikia maneno haya kutaka kukufanya ujaribu kusikiliza yale ambayo hukuwa unayajua.

Wewe unaandika uso wako umeuficha.
Mimi naandika jina langu linafahamika na uso na sauti yangu iko wazi.

Sijajificha.

Jiulize kwa nini sijajificha kisha jiulize wewe mwenyewe kwa nini unaogopa kutambulika unaficha uso wako na jina lako?
 
Nataka nikuambie kitu kuwa Waislam si kama unavyowaeleza.
Wametaka kujenga Chuo Kikuu 1968 serikali ikavunja taasisi yao.
Benjamin William Mkapa mwanzoni mwa miaka ya 2000, aliwapa kiluchokuwa Chuo cha TANESCO pale Morogoro,?je munakitumiaje kusomesha Waislamu?

Au mumeamua muwa watu wa kulalamika tu?
 
Nimefanya mtihani wa kumaliza elimu ya msingi mwaka 1985, Mzimuni P/s na tulitumia namba [sikumbuki Waziri wa elimu alikuwa nani], mwaka 1986 nilirudia tena shule ya msingi, na mwaka 1987 nikafanya tena mtihani wa darasa la 7 [tulitumia namba pia].

Mwaka niliorudia shule ya msingi tulikuwa wengi, watatu miongoni mwao walitumia majina ya Kiislamu na wawili [walikuwa na uwezo mzuri darasani] walifaulu. Nilipokuwa kidato cha kwanza, darasani kwetu waliorudia walikuwa 75% na walikuwa na majina ya Kiislamu.

Yawezekana madai yako yakawa na ukweli fulani lakini ukweli ni kuwa mwamko wa Waislamu kielimu hasa ngazi ya chini ni mdogo. Mimi kwetu ni Kigoma, Mwanga Vamia, na mama yangu alikuwa mwalimu shule ya msingi. Aliwahi kufundisha shule ya msingi Kipampa Ujiji. Aliwahi kutusimulia jinsi wazazi wa kule walivyokuwa wanakwenda shuleni saa 4 asubuhi na kuwachukua watoto wao na kuwapeleka chuoni huku masomo yakiendelea.

Ni siku hizi ndio angalau kuna mwamko wa Kielimu miongoni mwa Waislamu maana hata vyuo huanza kufundishwa alasiri.

Vv
 
Huyu mzee siku zote likitokea jambo, huliangalia kwa mlengo wa kidini pale muislamu anapokuwa muhanga. Hivi visa vya nafasi za waliofaulu darasa la saba kupewa watu wengine hata wenye 'majina' ya Kikristo nafasi zao walipewa wengine vilikuwepo vingi, tatizo ni pale mzee Mo anapogeuza na kuliweka kidini. Mimi nilisoma na wanafunzi wengi tu sekondari wenye majina ya Kiislamu ambao walifaulu. Darasani kwetu kulikuwa na 'Wakristo' watano wenye majina ya Kiislamu!

Vv
 
City...
Hapana hilo ndilo jibu lake sijakwepa.
Ikiwa wewe hukulipenda jibu hili mimi sina jibu lingine.

Ikiwa hukupendezewa na huo waraka ni bahati mbaya kwako.

Muhimu ni kuwa waraka huo ni sehemu ya historia ya Waislam wa Tanzania.
Ndio maana tynakuambu unaokoteza hoja..hakuna Mtoto wa Kisslam ambaye Leo hii ananaweza kudai kashindwa kusoma kimfumo! Acha uongo.na kuwapumbaza wachache!
 
Ndio maana tynakuambu unaokoteza hoja..hakuna Mtoto wa Kisslam ambaye Leo hii ananaweza kudai kashindwa kusoma kimfumo! Acha uongo.na kuwapumbaza wachache!
Maku...
Hakuna tatizo uzuri tumejadili.

Umesoma hoja zangu nami nimesoma zako.

Nimeeleza historia ya Waislam jinsi walivyozuiwa kujenga Chuo Kikuu mwaka wa 1968 kwa kupigwa marufuku EAMWS na kuunda BAKWATA na miaka ya 1970 kwa serikali kukataa OIC kujenga Chuo Kikuu Tanzania.

Nimeeleza matatizo ya ubaguzi katika Wizara ya Elimu na matatizo ndani ya Baraza la Mitihani.

Hii ni historia niliyotafiti na imechapwa katika kitabu na journals.

Vitabu na journals havichapi kazi za kuokoteza kwani huo ni uwanja wa wasomi.
 
Vv,

Hili jibu langu nimempa Makulanga.
Nawe linakufaa pia:

"Hakuna tatizo uzuri tumejadili.

Umesoma hoja zangu nami nimesoma zako.

Nimeeleza historia ya Waislam jinsi walivyozuiwa kujenga Chuo Kikuu mwaka wa 1968 kwa kupigwa marufuku EAMWS na kuunda BAKWATA na miaka ya 1970 kwa serikali kukataa OIC kujenga Chuo Kikuu Tanzania.

Nimeeleza matatizo ya ubaguzi katika Wizara ya Elimu na matatizo ndani ya Baraza la Mitihani.

Hii ni historia niliyotafiti na imechapwa katika kitabu na journals.

Vitabu na journals havichapi kazi za kuokoteza kwani huo ni uwanja wa wasomi."
 
Benjamin William Mkapa mwanzoni mwa miaka ya 2000, aliwapa kiluchokuwa Chuo cha TANESCO pale Morogoro,?je munakitumiaje kusomesha Waislamu?

Au mumeamua muwa watu wa kulalamika tu?
Stux...

Hili jibu nimewapa pia wachangiaji wengine:

"Hakuna tatizo uzuri tumejadili.

Umesoma hoja zangu nami nimesoma zako.

Nimeeleza historia ya Waislam jinsi walivyozuiwa kujenga Chuo Kikuu mwaka wa 1968 kwa kupigwa marufuku EAMWS na kuunda BAKWATA na miaka ya 1970 kwa serikali kukataa OIC kujenga Chuo Kikuu Tanzania.

Nimeeleza matatizo ya ubaguzi katika Wizara ya Elimu na matatizo ndani ya Baraza la Mitihani.

Hii ni historia niliyotafiti na imechapwa katika kitabu na journals.

Vitabu na journals havichapi kazi za kuokoteza kwani huo ni uwanja wa wasomi."
 
Nimeeleza matatizo ya ubaguzi katika Wizara ya Elimu na matatizo ndani ya Baraza la Mitihani.
Wizra ya elimu haina ubaguzi wowote sema waislamu hawapendi kusoma. Kama kuna ubaguzi ni vipi wewe ulisoma, akina Kikwete, Prof Malima RIP, Prof Shivji na Waislamu wote kwa maelfu walio na degree!!

Acheni kuharibu nchi kwa ashiki zenu udini. Baada ya maisha hapa duniani huko ahera/peponi hakuna dini tena
 
Zanzibar ni shida.

Nina mchumba wangu aliwahi fundisha field huko anakuambia shuleni wakija hawafiki saa tisa jioni

Saa Tano washasepa

Ijumaa ndio hawaonekani kabisa.

Class ndio kabisa vilaza wa kutupwa.
Me kule nyumbani watu hawana uchungu kabisa na mambo ya skuli.........uwa natafakari siku tukijitenga na bara sijui nchi tutaiendesha aje
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…