Hatma ya Muslim University of Morogoro na Maono ya Aga Khan kuwasaidia Waislamu kujenga Chuo Kikuu

Stux...
Kama nilivyokwisha kukueleza kuwa Waislam wamefikisha ushahidi wao serikalini.

Serikali ina hofu kubwa katika somo hili.

Haina majibu kwa nini ilizuia EAMWS kujenga Chuo Kikuu mwaka wa 1968 wala haina majibu kwa nini waliinyima OIC kibali cha kujenga Chuo Kikuu Tanzania katika miaka ya 1970.

Halikadhalika haina majibu ya yaliyokuwa yakifanyika Wizara ya Elimu wala haina majibu ya yaliyokuwa yakifanyika NECTA.

Muhimu ni kuwa tunayajadili haya hadharani na yanafahamika.
 
Hii inabidi FaizaFoxy na adriz wajipe ilim vizuri zaidi.
 
Nusu ya Wakristo wa Ujerumani ni Protestants, Waingereza ni Waangelikana sasa waliwapendeleaje Wakatoliki?!
 
Wala usihangaike sana katika hili, wewe angalia tu shule za mwisho kitaifa katika mitihani ya ngazi zote nyingi huwa zinatokea mikoa au kanda ipi.
 
Huu uzi ungefungiwa hapa
 
Nga...
Nyerere analaumiwa kwa kuivunja EAMWS na kuunda BAKWATA ili Waislam wasiwe na Chuo Kikuu kwani wakati ule EAMWS ilikuwa inajenga Chuo Kikuu.

Akamkamata Mufti wa Tanganyika Sheikh Hassan bin Ameir na kumfukuza Tanganyika asirejee tena.
Baada ya hapo mmejenga chuo kikuu kipi na hospital ipi ya maana?
 
Mzee maelezo uliyonukuu hayana ushahidi wowote kuthibitisha hujuma za kielimu dhidi ya Uislamu. Aidha hayajibu hoja iliyowasilishwa hapo juu
 
Mzee maelezo uliyonukuu hayana ushahidi wowote kuthibitisha hujuma za kielimu dhidi ya Uislamu. Aidha hayajibu hoja iliyowasilishwa hapo juu
Uzalendo...
Wanaostahili kutoa majibu kuwa hakuna ushahidi ni serikali ambayo Waislam wamefikisha malalamiko yao huko.

Serikali haitaki kulijadili tatizo hili kwani kwao huko ni kukubali kuwa lipo tatizo.

Hili linawatisha.

Waislam wanataka majibu kwa nini serikali iliipiga marufuku EAMWS wakati inajenga Chuo Kikuu?

Waislam wanataka majibu kwa nini OIC walijimwa kibali kujenga Chuo Kikuu?

Na mengi mengine.
Baada ya hapo mmejenga chuo kikuu kipi na hospital ipi ya maana?
Nyio...
Waislam hawapokei fedha kama za Memorandum of Understanding zinazotolewa na serikali kwa makanisa.
 
Kwahiyo hata shule zetu bora ni fedha za zinazotolewa na serikali? Be serious
 
Kwahiyo hata shule zetu bora ni fedha za zinazotolewa na serikali? Be serious
Nyio...
Jinsi ulivyoniuliza hili swali tayari ushatoa jibu.

Zaidi umeniambia niwe "serious," yaani nisifanye maskhara.

Mimi ni "serious" sana kiasi kalamu yangu imefika mbali.

Kitabu changu kuhusu Abdul Sykes kinajadiliwa hapa JF toka 2008 na kimechapwa mara nne tunakwenda toleo la tano.

Nimekuwa Mwandishi Bora JF Jukwaa la Historia kwa miaka miwili mfululizo 2021 na 2022.

Nimefanikiwa kubadili historia nzima ya uhuru wa Tanganyika.

Nimesomesha hapa watu mambo ambayo hawakupata kuyajua.

Mimi ni mtu "serious."
 
Hapana, jitahidi kuwa accommodative na kujua kwamba you ain’t infallible.
Tatizo la Mohamed Said liko hapa


Swali la kizushi kwako, unaamini Necta ikiongozwa na waislamu, fursa za waislamu kielimu zitabadilika?

Kwa sasa inaongozwa na Muislam wala sijaona Waislam wakifanya vizuri kuliko wa dini nyingine. Waislam wanaojali ubora wa elimu wanapeleka watoto wao shule za Wakristu vyuo vya kanisa
 
Hayo matatizo bado yapo? Mbona hamjengi hicho chuo?
 
Rava...
Hizi si hadithi.
Soma utatambua.

EAMWS ilikuwa inajenga Chuo Kikuu mwaka wa 1968 ikapigwa marufuku na serikali na BAKWATA ikaundwa.

Hii si hadithi ni historia ya Waislam wa Tanzania.
Huu upumbqvu wa kupigwa marufuku kujengwa chuo hapa tanzania umekuwa ni kilio kila mwaka hebu zeeka vizuri na wajukuu wako huna cha maana na mawazo ya kujenga kwa miaka ijayo wewe kilio chako chuo chuo
Amengia mwinyi kafanya kitu gani cha maana
Jakaya?
Na huyu s100 bado tu unalilia chuo sio kutoa ushauri kama taifa kwenda mbele zaidi wewe kulilia chuo tu ?
 
Tuwe wakweli ndugu zetu katika imani swala la elimu kwao ni kama dhambi hawajitambui na hawana bidii tumesoma nao wengi tu tena elimu ilee ya miaka ya nyuma unaona kabisa hawana juhudi hata ufuatiliaji nyumbani wazazi hawana muda zaidi ya kuhamasisha kwenda madrasa na kujifunza judo πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ wajuzi wa kulalamika ila wanapewa feva nyingi na hawawezi zitumia
 
Nina marafiki wengi waislam na wengi elimu kubwa kubwa wamezipata taasisi zisizo za kiislam.

Baadhi wanakiri ni wazazi wao kufunguka tu ndio kuliwasadia , ukweli usemwe waislam hawatumii nguvu kuwekeza kwenye elimu ya kawaida kuliko dini.

Nimewahi kuona mashindano ya kuhifadhi quran yakiwa na promo kubwa au ufadhili wa safari za hija ila sijawahi kuona waislam hawa wakitoa ufadhili wa masomo kwa watoto wasio na uwezo kwenda kusoma shahada nchi za ughaibuni(kama rekodi ipo naomba iletwe hapa)

Waislam wote tuliokutana masomo ya juu na wengine nje ya nchi ukiwauliza hizi habari za kutumia almost masaa mengi madrasa watakuambia wazazi wao walikataa na kuamua kuwapeleka shule point yangi ni kwamba wanatakiwa wajifunze kubalance dini na mfumo wa maisha wa kisasa.

Leo hii waarabu kibao toka Saudia,Qatar, Yemen,Palestine n.k wanagombea fursa adhimu kwenda Ulaya na Amerika na wakifika huko wanaorudi makwao hawazidi 10%
 
Mh mzee Said nafikiri ni muhimu ukawa unajiridhisha haswa kwenye takwimu

Yaani waislamu 71% na wakristo 29% wapo shule moja. Matokeo yanakuja 71% wakristo wamechaguliwa na 29% waislamu wamechaguliwa.

Kabla hatujahukumu.

Totala number ya wanafunzi ilikua wangapi? Katika hii total waislamu wangapi na wakristo wangapi?

Waliofanya mtihani walikua wangapi? Katika hawa waliofanya, wakristo wangapi na waislamu wangapi?

Waliofaulu mtihani wangapi? Hapa waislamu wangapi na wakristo wangapi?

Waliofeli mtihani wangapi? Waislamu wangapi na wakristo wangapi?

Ambao hawakufanya mtihani wangapi? Wakristo wangapi na waislamu wangapi?

Hizi factors zote zizingatiwe. Haiwezekani mtu anakuletea namba tu hizo na wewe unaziwasilisha kwetu, hii siyo sawa.
 
Sema dingi umekula kitabu ila nashangaa huu upuuzi wa kuwachukia watu wasio waislamu umeanzia wapi!!... yaani pamoja na kuwa msomi mkubwa ila harakati zako ni kama za wale ambao hawakwenda hata chekechea. Udini wa kipumbavu sana.
 
Wamekudanganya elimu ya madrasa ina vitu vingi ila sio ndefu kwa mfano ukisoma ukiwa darasa la kwanza yaani miaka 7 mpaka ukifika darasa la saba unakuwa mbali sana.

Hakuna sehemu ambayo waislamu wanapuuza elimu kwa hawaweki mkazo wapo wanaosoma na kufadhiliwa na taasisu ila haya mambo yakuwa chinu ya taasisi husika...Pia kusoma vyuo ambavyo sio vya kiislamu hakuna mtu kalazimishwa kusoma chuo cha kiislamu ni jukumu la mtu binafsi kusoma popote ....Vyuo ni biashara kama biashara nyingine wapo wanaoenda kusoma mpaka iran nawajua kibao ila wanakuwa chini ya taasisi kama ni mtu wa taasisi utapata fursa.

Hao wenzio wanakudanganya na hakuna ukweli yupe Ally hapi kasoma madarasa na wapo kibao,ukisoma ukiwa mdogo ukifa form four basi unakuwa unajua vingi sana wapo watota wana miaka 10 wanajua Qur an yote ....Hao wamekudanganya hakuna kitu kama hicho Qur an unasoma kutokana na akili yako wewe unaweza kuruka madarasa kibao kwa miaka 3 tu ,kama una kichwa kizuri unamaliza kila kitu..

Kwa vile elimu ya uislamu ni utekelezaji yaani mafunzo makubwa kama ndoa unaweza kusoma ukiwa form one yaani miaka 14,15 hata kuosha maiti ..Shariq zote unless otherwise utake kusoma upate degree ,masters na lazima uende nje ya
nchi kusoma kwa sana...

Kufundishwa kwa level ya chuo ni haki kwa vile ni ubobezi kama masomo mengine mbona programms za udaktari mpaka miaka minne ,kuna masters za miezi 18 wengine ni miaka 2 ..


Unachotaka ni hicho kama unataka kubobea kweny fani fulani.


Mdogo wangu yupo SUA yeye elimu ya madrasa mpaka kuwa mkubwa alisoma akiwa na miaka 5 mpaka anaanza form one kamaliza kitu ni shekhe anafundisha akiwa na miaka 15 tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…