Hawa jamaa wa Iringa chini ya Producer Ambha walitisha sana

Hawa jamaa wa Iringa chini ya Producer Ambha walitisha sana

Huyo mzungu ni miika mwamba na sababu ya kuacha production wakati ule ghafla tu ilikua ni hiyo kutopata pesa. Nyimbo zinaenda lakini pesa hakuna. Hata pa kulala tu ikawa shida kwake, mwisho akaamua kurudi kwao

P funk na mj nao wamepitia hayo hayo wasanii kurekodi bure, pesa wanapata pale ambapo album inaenda kuuzwa. Sasa album mauzo yakiwa kidogo hasara kwao. je wangapi waliuza album vizuri? Show, hapo napo huchukua percent lakini mikono inakua mingi Kuna meneja, kuna mtu Kati, kuna msanii na Kuna ww producer. Show ngapi atarudisha pesa yako? Tena zamani show nyingi walikua wanakopwa na mwisho wa siku hawalipwi kabisa

Kingine kinacholipa ni deals za wasanii wako kutoka kwenye makampuni, but hapo kuna/kulikua na mtu wa Kati. Huyu mara zote ndio anakula kikubwa, sasa ukileta ujuaji na kutaka muende sawa anakuzima, nyimbo zote kutoka studio yako hazipigwi redioni. P funk alipitia hayo, master j alipitia pia hayo. Mwisho utafunga tu mwenyewe studio hata iwe kubwa vipi, ndio maana uliona bongo records ikafa chali
Studio zilikuwa zinatengeneza pesa kwa matangazo.
 
Yaki namuheshimu sana, enzi anakuja Tosa kwa mdogo wake kwenye graduu na aliwahi kuimba shoo moja nakumbuka.

Oya,
 
Acha kabisa ile ngoma yangu pendwa. Nashukuru ferouz alileta maringo maana ndiye ilikuwa aimbe chorus ikabidi majani akae mwenyewe na nadhani alifanya kitu bora kuliko ambavyo angefanya ferouz.
Kuna na ile ngoma ya wachuja nafaka, ya leo kali ile sehemu ya bridge na intro pale inasema. Ya leo kali ya leo kaliii
ya leo kali kunguru kanyea ugali masela wana njaa kali wakatoa macho utafkiri wamepoteza nauli na ukicheka t utakua umewauzi..unajifanya unasoma unasoma unasoma chekea primary sec ujawai kupata vema...
 
Mkuu, sio kwamba hao kina P Funk na MJ walimsagia kunguni Mikka kuhusiana na working permits nk ndio ikamlazimu kuondoka hapa nchini? Maana huyu si alikuwa ni mwajiriwa wa FM studio za Felician Muta? Means alikuwa na aina ya ujira hivi..
hii ndo sababu ambayo wat wengi hawataki kuiongea..mika ndo best to ever do it hapa bongo..
jamaa waliona threat yake na kuondoka hapa bongo ni figisu tu
 
Ambha anadai kwamba alifanya production lakini hakutoboa akawa ameamua kufunga studio aachane na muziki maana nyimbo zilikuwa hazipigwi na hapati fedha. Sasa akiwa ashaamua kufunga studio, asubuhi kalala kaja yaki anamgongea dirishani anamwita ambha aamke kuwa kaja na faridah anataka wakarekodi. Kama mnakumbuka zama hizo faridah alikuwa ni msanii wa kike ambaye nyimbo zake kama pesa zilikuwa ikipigwa sana RFA ambayo ilikuwa kwenye peak zama hizo.
Basi ambha kusikia farida akaamuka na kwenda studio na yaki na farida ndipo wa karekodi wimbo unaitwa we ni wangu ulikuwa na beat ya crank na crank ndiyo ilikuwa mainstream.
Baada ya hapo akarekodi hits kibao hadi wasanii wakaanza kutoka dar wanamfuata iringa. Moja ya msanii aliyefanya ngoma naye ambazo mpaka leo nazikubali ni Rama Dee ambapo alifanya naye ngoma inaitwa kikao cha family na ngoma nyingine. Ambha anadai ngoma za rama dee zilikuwa zimejaa back vocal zake mwenyewe na rama dee alimkubali jamaa jinsi alivyokuwa anapika nyimbo zake.
Ila kati ya vijana ambao alifanya nao ngoma zikahit kutokea iringa ni yaki, roho saba, na vijana wengine.

View: https://www.youtube.com/watch?v=H6MWWxMkDhM&list=RDH6MWWxMkDhM&start_radio=1

View: https://www.youtube.com/watch?v=PihvQOA_gxo

View: https://www.youtube.com/watch?v=chdP7c91Qs4
Lakni my favorite ni yaki ya tonight.

Wanaonekana ni makatili sana kwa mbwa wa watu mitaani....!
 
Amba alitengeneza ngoma nyingi na ngoma nyingine ni maneno nawafunza ya Temba, ila hasa wengi tulimfahamu kupitia ngoma za Yaki na Roho Saba
Yeah! Beat kali sana,Temba mwenyewe alikuwa na hasira sana kipindi hicho,aliandika verse kali sana mule
 
😂😂
Tonight ya Yaki niliisahau kabisa. Hebu weka namba yako hapa nikutumie hata vocha, Umenikumbusha mbali mno.​
😂😂 mie sikuwahi kujua kama huo wimbo upo Duniani, nimefungua huu uzi nipo Club, imebidi nitoke nje kuusikiliza huu wimbo, nilikuwa naupenda sana aisee
 
Back
Top Bottom