Huyo mzungu ni miika mwamba na sababu ya kuacha production wakati ule ghafla tu ilikua ni hiyo kutopata pesa. Nyimbo zinaenda lakini pesa hakuna. Hata pa kulala tu ikawa shida kwake, mwisho akaamua kurudi kwao
P funk na mj nao wamepitia hayo hayo wasanii kurekodi bure, pesa wanapata pale ambapo album inaenda kuuzwa. Sasa album mauzo yakiwa kidogo hasara kwao. je wangapi waliuza album vizuri? Show, hapo napo huchukua percent lakini mikono inakua mingi Kuna meneja, kuna mtu Kati, kuna msanii na Kuna ww producer. Show ngapi atarudisha pesa yako? Tena zamani show nyingi walikua wanakopwa na mwisho wa siku hawalipwi kabisa
Kingine kinacholipa ni deals za wasanii wako kutoka kwenye makampuni, but hapo kuna/kulikua na mtu wa Kati. Huyu mara zote ndio anakula kikubwa, sasa ukileta ujuaji na kutaka muende sawa anakuzima, nyimbo zote kutoka studio yako hazipigwi redioni. P funk alipitia hayo, master j alipitia pia hayo. Mwisho utafunga tu mwenyewe studio hata iwe kubwa vipi, ndio maana uliona bongo records ikafa chali