Hawa ndio Wenye Kurithi Pepo ya Firdaus

Hawa ndio Wenye Kurithi Pepo ya Firdaus

Binadamu ni nini? Hata Mungu akukumbuke jamani japo kuna Mungu ila dunia inafanya nisione thamani ya kuwa binadamu
Biandamu ndio khalifa au kiongozi wa duniani hii hivyo ni lazima akumbukwe na Muumba wake na kuangaliwa je anaishi katika muongozo anao takiwa aishi au ndio anajifanyia mambo kama anaavyotaka?

Kwanini dunia inakufanya usione thamani ya kuwa mwanadamu mkuu?
 
Aisee mtu amekwambia haswali hlf unamuitikia dua eti muingie peponi

Apo mm naona pana mushkila kidogo
Mkuu natambua unajua fika kuwa si swala Tu ambayo itampelekea mtu peponi,na ndio maana mwenye ulimwengu wake anasema si wema Tu huo kuelekea qibla na kuswali Bali kuna wema mwingine zaidi ya huo,mfano ni kutoa vile tulivyo rudhukiwa na Allah.

Na natambua unajua fika kuwa siku zote Tunatakiwa kuomba tuwe na mwisho mwema, kwani ambaye haswali Leo huenda akaswali kesho na unayeswali Leo huenda ukaacha kesho na umauti ukakukuta katika Hali hiyo,Mungu atuepushe na Hilo.

Kwahiyo ni jukumu letu kuombeana mema kama wanadamu
 
Usisahau kutafuta pesa mkuu
Mkuu kuna watu walitafuta hela mpaka wakawa hawajui watazitumia vipi

Lakini kumbuka Mali na watoto hakika ni starehe ya dunia na vitendo vizur vibakiavyo ndio Bora zaidi baada ya kufa kwako
 
Bro, Mungu hawez kuwa mmoja unless tukubaliane kati ya wakristo na waslamu kuna either kundi moja limepotoka and most likely wote kwa pamoja,Na km wote tuko sahihi bas kila dini ina Mungu wake,msiogope kusema ukweli kwasabb ya hofu ya imani zenu

Ukiwa tayr kwa huu mjadala naomba ukireply apa unambie kabsa
Mkuu asante Kwa maoni yako

Kwanza huwa siku hizi sipendi Sana mijadala ya Dini kwasababu moja, watu huwa hawajadili hoja Bali huleta matusi na kejeli kitu ambacho ni upuuzi.

Sasa siwezi kukuhukumu kuwa nawe ni mmoja wapo labda mpaka nikusikilize.

Sasa kama ni mjadala naomba tujikite Kwa nini unadhani kuna Mungu wengi, tusijadili Mungu yupi ni sahihi kwasababu Imani yangu inaniambia Mungu ni mmoja Tu.

Kama unaafikiana na hili basi naomba
Usimame kwenye Podium na uchukue microphone.

Nakusikiliza.
 
Nani alisema hayo? Namaanisha Mtume gani katika mitume yote aliyoileta Mwenyezi Mungu?
 
Uzuri nikwamba mada nzuri kama hizi uwa hazina wachangiaji. Lakini ndiyo mambo ambayo mwanadamu anatakiwa ayasikie muda wote kwenye sikio lake.

Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema na baraka akujalie hekima zaidi na baraka katika maisha yako.

Ahsante sana kwa maneno mazuri ya Mwenyezi Mungu.🙏
Yani tuache kujadili siasa inayoaffect maisha yetu 24/7 on a daily basis tuanze kujadili stori za kusadikika ambazo sio tu hatuna ushahidi nazo, ila hatuwezi kubadilisha chochote, wewe pepo hata uijadilije, huwezi kuitengeneza au kuibadilisha.
 
Biandamu ndio khalifa au kiongozi wa duniani hii hivyo ni lazima akumbukwe na Muumba wake na kuangaliwa je anaishi katika muongozo anao takiwa aishi au ndio anajifanyia mambo kama anaavyotaka?

Kwanini dunia inakufanya usione thamani ya kuwa mwanadamu mkuu?
Kiongozi gani hana nguvu hata ya kupeperuka , kupotea kuaffect vitu bila kushika bado kunaadui yake ambaye ananguvu mara billion zaidi yake
 
Kiongozi gani hana nguvu hata ya kupeperuka , kupotea kuaffect vitu bila kushika bado kunaadui yake ambaye ananguvu mara billion zaidi yake
Kuhusu kupeperuka na kuaffect sina neno hapo kwakuwa sijui unamaanisha nini

Ni adui gani ana nguvu mara billion
 
Najua fika unajua nazungumzia Nani

Labda kama Una jambo lingine
Mkuu ,uislam ulikuwepo kabla ya ujio wa Mtume Muhammad SAW.

kwamba waislam wa mwanzo hawakujua juu ya uwepo wa hizo pepo kwa vile tu Mtume Muhammad alikuwa hajazaliwa?
 
Shetani na Mapepo
Mkuu shetani na mapepo hawana nguvu Kwa mwanadamu ambaye amejikita katika kumwabudu Mungu wake na akashikamana nae kisawasawa..

Shetani ana nguvu Kwa mtu ambaye ni muovu na ambaye yupo mbali na utukufu WA Mungu

Mara baada ya shetani kuhukumiwa kwenda motoni,alimwomba Mola wake Ampe wasaa WA kuishi Mda mrefu kidogo na Mungu akampa wasaa,na shetani akasema Hakika nitawapoteza waja wako ili niingie nao Motoni.

Mola wake akamwambia hauna nguvu ya kuwalazimisha kukufuata isipokuwa wale wachache ambao watakuwa radhi kukufuata.

Kwahiyo shetani Hana nguvu juu yako Bali anachofanya ni kukushawishi na wewe mwenyewe unaingia katika anga zake.

Kwahiyo Mwanadamu ana mamlaka juu ya shetani labda atake mwenyewe
 
Alhamdulillah ijumaa imeingia tayar na ningependa tukumbushane mawili matatu ili tujiweke tayari kukutana na hiyo siku ya Mwisho tukiwa tumeridhiwa na Mwenyezi Mungu.

Firdaus ndio pepo ya juu zaidi kuliko zote Kwa maana nyingine hii ndio pepo ambayo ni first class,na hii watairithi Mitume na Wacha Mungu.

Kwa taarifa yako Tu inasemekana zipo takribani daraja Mia Moja za pepo (100) na mkubwa wao ni huyo Firdaus.

Lakini cha kusikitisha zaidi pamoja na kuwepo hizo pepo zenye daraja takribani Mia Moja bado kuna watu hawatofanikiwa kuingia na matokeo yake wataingia motoni, Ewe Mwenyezi Mungu utujaalie tusiwe miongoni mwao Amiin.

Je watu wenye sifa gani ambao watairithi au kuingia katika hii pepo?

Kwa mujibu wa Qur'an watu wenye sifa hizi ndio ambao watairithi pepo hiyo;

WA Kwanza ni waumini ambao ni wanyenyekevu katika sala zao,hawa ni Wale ambao wanapokuwa ndani ya sala basi mawazo Yao na fikra zao zote zinakuwa ndani ya ibada ya swala,hawa hakika wamefanikiwa,

lakini kuna baadhi yetu wawapo ndani ya swala basi wanajikuta wanawaza hiki na kile na mambo kibao yanatawala swala yake,ingawa ni vigumu Kwa asilimia Mia moja kutotoka kimawazo,lakini hata ukitoka basi iwe kidogo na mara moja ujikumbushe kuwa upo ndani ya swala na ujue unawasiliana moja Kwa moja na Mola wako.

Sifa ya pili ni ambao wanajiepusha na mambo ya kipuuzi

Sifa ya tatu,na ambao wanatoa zaka,hapa inaingia na sadaka pia,maana zaka ni sehemu ya sadaka. Kwahiyo hakika kutoa sadaka ni Jambo muhimu Sana na ni ibada ambayo ina faida kubwa Sana,kuna maradhi mengine unapona Kwa kutoa sadaka Tu,


Na sadaka ndio ibada ambayo mja ataikumbuka mara Tu atakapoanza kutokwa na roho, ataomba Ewe Mwenyezi Mungu naomba walau unipe nafasi kidogo niweze kutoa sadaka. Sasa usisubir mpaka wakati huo ufike huenda usipate huo Mda wa kutoa sadaka.

Sifa ya nne, ni ambao wanazilinda tupu zao, hapa ndio wale wanachama WA jukwaa la MMU wajitafakari vizuri Sana,maana Yale mambo ya kulana kimasihara basi ujue nawe utaikosa pepo kimasihara,wazee wa Michepuko hapa kazi kwenu,hapa inakatazwa Zinaa Kwa nguvu zote,kwahiyo tujitathimini Sana.

Sifa ya tano,ni Kwa wale ambao wanazitimiza Amana zao na ahadi zao,kuna watu Jambo la kuahidi wanalichukulia kimchezo mchezo Tu,tena hawa wanasiasa hawa mjue Mungu anawaona! Maana nyie Kwa kutupiga sound hamjambo basi endeleeni Tu kutupiga sound halafu muone huko kwa Mungu kama mtafanikiwa.

Hapa Napo Jambo la Amana limeingia pia,mtu amekupa Amana yake umuhifadhie basi fanya hivyo usiingie tamaa ya kuitumia Bila ridhaa au idhini yake.

Na sifa ya sita ni Wale ambao wanazihifadhi swala zao,inamaana ambao wanadumisha swala zao siku zote,maana kuna watu huwa wanaswali ijumaa mpaka ijumaa Tu,au idi mpaka idi Tu,au akiwa na shida basi yeye ndio utamuona anaswali na mambo yake yakiwa fresh Tu basi ndio nitolee na kuswali bye bye.

Hope sauti yangu imetosha na kusikika vizuri kabisa.

Ijumaa Mubaraka!

Ni hayo Tu!
Mbona wewe unajenga hoja hata unatamani kujifunza,hao wenzio wanakazhifi na kubeza na kukebehi ni waislam Kama wewe au wanakosa Moja ya sifa tajwa?
 
Back
Top Bottom