Hawa ndio Wenye Kurithi Pepo ya Firdaus

Hawa ndio Wenye Kurithi Pepo ya Firdaus

baby zu haya mambo mengine yanataka ukae darasani kabisa, anyway kuna fursa ya zaka huko? ili tuiwahi hahahaah.
images - 2022-12-09T165426.714.jpeg

Akhy ni moja ya kumi? Kuna shekh niliwahi kumsikiliza alisema sijui kile kiasi unakigawanya mara nne kama sio nane sasa ile moja ya nane ndo unatoa zaka, elimu hii ya zaka sijawahi kuisoma kwa mazingatio
 
Ukhty ni asilimia Kumi

Kuna masheikh wengine utasikia wanasema ukiwa na milioni moja waeza Toa zaka,kitu ambacho sio Sawa lazima kuna hesabu ifikie Kwa kulinganisha na thamani ya dhahabu kwasasa wanasema ni gramu 85 za dhahabu lakini hii ni Kwa pesa.

Sio mbaya ukhty ukifanya home work huenda tukapata jingine la kujifunza
Hapana mkuu sio 10% bali ni moja ya 4 ya 1 ya 10.
 
Ukhty ni asilimia Kumi

Kuna masheikh wengine utasikia wanasema ukiwa na milioni moja waeza Toa zaka,kitu ambacho sio Sawa lazima kuna hesabu ifikie Kwa kulinganisha na thamani ya dhahabu kwasasa wanasema ni gramu 85 za dhahabu lakini hii ni Kwa pesa.

Sio mbaya ukhty ukifanya home work huenda tukapata jingine la kujifunza
Nilivyomaliza kukoment nilangalia sahihi muslim hadithi kama tati nimeona zimesema 1/ 10 shukuran pia maana umenifanya nifungua app ya sahihi kuangalia hadithi zinasemaje
 
M
baby zu haya mambo mengine yanataka ukae darasani kabisa, anyway kuna fursa ya zaka huko? ili tuiwahi hahahaah.View attachment 2440802
Mwenyewe natafta watoa zaka waniletee 🤣🤣🤣🤣
Naam elimu hii inahitaji ukae isome niliwahi kuisoma mda lkn wakti huo hata kula yangu ilikua ya shida hvyo hata mazingatio siku nayo maana sikua najiona kama ntafikia hatua ya kutoa zaka😂😂😂😂
Naam nimepitia sahihi muslim nimeona ni 1/10 shukran sana. Huku tunapata elimu kwa kwel
 
Hahaha uko wapi kwanza nikuelekeze darasa mambo ya kujifungulia swahih muslim peke yako utakuja kukutana na nyota nyota tukukose.
 
Mkuu natambua unajua fika kuwa si swala Tu ambayo itampelekea mtu peponi,na ndio maana mwenye ulimwengu wake anasema si wema Tu huo kuelekea qibla na kuswali Bali kuna wema mwingine zaidi ya huo,mfano ni kutoa vile tulivyo rudhukiwa na Allah.

Na natambua unajua fika kuwa siku zote Tunatakiwa kuomba tuwe na mwisho mwema, kwani ambaye haswali Leo huenda akaswali kesho na unayeswali Leo huenda ukaacha kesho na umauti ukakukuta katika Hali hiyo,Mungu atuepushe na Hilo.

Kwahiyo ni jukumu letu kuombeana mema kama wanadamu
Sasa basi ungemuombea kwanza Aswali ety
Mna hadithi ile ipo wazi
Kitakachohesabiwa cha mwanzo siku ya qiama ni swala
 
Mkuu asante Kwa maoni yako

Kwanza huwa siku hizi sipendi Sana mijadala ya Dini kwasababu moja, watu huwa hawajadili hoja Bali huleta matusi na kejeli kitu ambacho ni upuuzi.

Sasa siwezi kukuhukumu kuwa nawe ni mmoja wapo labda mpaka nikusikilize.

Sasa kama ni mjadala naomba tujikite Kwa nini unadhani kuna Mungu wengi, tusijadili Mungu yupi ni sahihi kwasababu Imani yangu inaniambia Mungu ni mmoja Tu.

Kama unaafikiana na hili basi naomba
Usimame kwenye Podium na uchukue microphone.

Nakusikiliza.
Nimefny reasoning kupitia maswali yangu nilohoji apo ,i hope unaweza kuwa mwanzo mzuri wa hoja
 
Vipi yule al hajji muuza madawa ya kulevya?
Hakuna mwanadamu anaeweza sema huyu wa peponi au laa hvyo atakae muhukumu ni Allah, na Allah alichotubainishia ni kua pepo yake hawakai wenye dhambi hvuo akasema tufanye kadha wakadha ili tuipate pepo na tukiteleza ametufungulia mlango wa toba hvyo anaweza kua muuza dawa lkn hujui hatma yake itakuaje, anaweza akatubia na ukamkuta peponi, japo hata sijui ni al hajji yupi unamzungumzia
 
Yani roho inakutoka
Alhamdulillah ijumaa imeingia tayar na ningependa tukumbushane mawili matatu ili tujiweke tayari kukutana na hiyo siku ya Mwisho tukiwa tumeridhiwa na Mwenyezi Mungu.

Firdaus ndio pepo ya juu zaidi kuliko zote Kwa maana nyingine hii ndio pepo ambayo ni first class,na hii watairithi Mitume na Wacha Mungu.

Kwa taarifa yako Tu inasemekana zipo takribani daraja Mia Moja za pepo (100) na mkubwa wao ni huyo Firdaus.

Lakini cha kusikitisha zaidi pamoja na kuwepo hizo pepo zenye daraja takribani Mia Moja bado kuna watu hawatofanikiwa kuingia na matokeo yake wataingia motoni, Ewe Mwenyezi Mungu utujaalie tusiwe miongoni mwao Amiin.

Je watu wenye sifa gani ambao watairithi au kuingia katika hii pepo?

Kwa mujibu wa Qur'an watu wenye sifa hizi ndio ambao watairithi pepo hiyo;

WA Kwanza ni waumini ambao ni wanyenyekevu katika sala zao,hawa ni Wale ambao wanapokuwa ndani ya sala basi mawazo Yao na fikra zao zote zinakuwa ndani ya ibada ya swala,hawa hakika wamefanikiwa,

lakini kuna baadhi yetu wawapo ndani ya swala basi wanajikuta wanawaza hiki na kile na mambo kibao yanatawala swala yake,ingawa ni vigumu Kwa asilimia Mia moja kutotoka kimawazo,lakini hata ukitoka basi iwe kidogo na mara moja ujikumbushe kuwa upo ndani ya swala na ujue unawasiliana moja Kwa moja na Mola wako.

Sifa ya pili ni ambao wanajiepusha na mambo ya kipuuzi

Sifa ya tatu,na ambao wanatoa zaka,hapa inaingia na sadaka pia,maana zaka ni sehemu ya sadaka. Kwahiyo hakika kutoa sadaka ni Jambo muhimu Sana na ni ibada ambayo ina faida kubwa Sana,kuna maradhi mengine unapona Kwa kutoa sadaka Tu,

Na sadaka ndio ibada ambayo mja ataikumbuka mara Tu atakapoanza kutokwa na roho, ataomba Ewe Mwenyezi Mungu naomba walau unipe nafasi kidogo niweze kutoa sadaka. Sasa usisubir mpaka wakati huo ufike huenda usipate huo Mda wa kutoa sadaka.

Sifa ya nne, ni ambao wanazilinda tupu zao, hapa ndio wale wanachama WA jukwaa la MMU wajitafakari vizuri Sana,maana Yale mambo ya kulana kimasihara basi ujue nawe utaikosa pepo kimasihara,wazee wa Michepuko hapa kazi kwenu,hapa inakatazwa Zinaa Kwa nguvu zote,kwahiyo tujitathimini Sana.

Sifa ya tano,ni Kwa wale ambao wanazitimiza Amana zao na ahadi zao,kuna watu Jambo la kuahidi wanalichukulia kimchezo mchezo Tu,tena hawa wanasiasa hawa mjue Mungu anawaona! Maana nyie Kwa kutupiga sound hamjambo basi endeleeni Tu kutupiga sound halafu muone huko kwa Mungu kama mtafanikiwa.

Hapa Napo Jambo la Amana limeingia pia,mtu amekupa Amana yake umuhifadhie basi fanya hivyo usiingie tamaa ya kuitumia Bila ridhaa au idhini yake.

Na sifa ya sita ni Wale ambao wanazihifadhi swala zao,inamaana ambao wanadumisha swala zao siku zote,maana kuna watu huwa wanaswali ijumaa mpaka ijumaa Tu,au idi mpaka idi Tu,au akiwa na shida basi yeye ndio utamuona anaswali na mambo yake yakiwa fresh Tu basi ndio nitolee na kuswali bye bye.

Hope sauti yangu imetosha na kusikika vizuri kabisa.

Ijumaa Mubaraka!

Ni hayo Tu!
Yani roho inakutoka ukumbuke hujatoa sadaka tutolee uongo wako.
 
naomba Makamba sr, Kikwete na Kinana wasisahaulike
 
Yani roho inakutoka

Yani roho inakutoka ukumbuke hujatoa sadaka tutolee uongo wako.
Unajua kwanini unakumbuka kutoa sadaka kwasababu ndio ibada nyepesi Kwa utekelezaji na unajutia haukuifanya
 
Alhamdulillah ijumaa imeingia tayar na ningependa tukumbushane mawili matatu ili tujiweke tayari kukutana na hiyo siku ya Mwisho tukiwa tumeridhiwa na Mwenyezi Mungu.

Firdaus ndio pepo ya juu zaidi kuliko zote Kwa maana nyingine hii ndio pepo ambayo ni first class,na hii watairithi Mitume na Wacha Mungu.

Kwa taarifa yako Tu inasemekana zipo takribani daraja Mia Moja za pepo (100) na mkubwa wao ni huyo Firdaus.

Lakini cha kusikitisha zaidi pamoja na kuwepo hizo pepo zenye daraja takribani Mia Moja bado kuna watu hawatofanikiwa kuingia na matokeo yake wataingia motoni, Ewe Mwenyezi Mungu utujaalie tusiwe miongoni mwao Amiin.

Je watu wenye sifa gani ambao watairithi au kuingia katika hii pepo?

Kwa mujibu wa Qur'an watu wenye sifa hizi ndio ambao watairithi pepo hiyo;

WA Kwanza ni waumini ambao ni wanyenyekevu katika sala zao,hawa ni Wale ambao wanapokuwa ndani ya sala basi mawazo Yao na fikra zao zote zinakuwa ndani ya ibada ya swala,hawa hakika wamefanikiwa,

lakini kuna baadhi yetu wawapo ndani ya swala basi wanajikuta wanawaza hiki na kile na mambo kibao yanatawala swala yake,ingawa ni vigumu Kwa asilimia Mia moja kutotoka kimawazo,lakini hata ukitoka basi iwe kidogo na mara moja ujikumbushe kuwa upo ndani ya swala na ujue unawasiliana moja Kwa moja na Mola wako.

Sifa ya pili ni ambao wanajiepusha na mambo ya kipuuzi

Sifa ya tatu,na ambao wanatoa zaka,hapa inaingia na sadaka pia,maana zaka ni sehemu ya sadaka. Kwahiyo hakika kutoa sadaka ni Jambo muhimu Sana na ni ibada ambayo ina faida kubwa Sana,kuna maradhi mengine unapona Kwa kutoa sadaka Tu,

Na sadaka ndio ibada ambayo mja ataikumbuka mara Tu atakapoanza kutokwa na roho, ataomba Ewe Mwenyezi Mungu naomba walau unipe nafasi kidogo niweze kutoa sadaka. Sasa usisubir mpaka wakati huo ufike huenda usipate huo Mda wa kutoa sadaka.

Sifa ya nne, ni ambao wanazilinda tupu zao, hapa ndio wale wanachama WA jukwaa la MMU wajitafakari vizuri Sana,maana Yale mambo ya kulana kimasihara basi ujue nawe utaikosa pepo kimasihara,wazee wa Michepuko hapa kazi kwenu,hapa inakatazwa Zinaa Kwa nguvu zote,kwahiyo tujitathimini Sana.

Sifa ya tano,ni Kwa wale ambao wanazitimiza Amana zao na ahadi zao,kuna watu Jambo la kuahidi wanalichukulia kimchezo mchezo Tu,tena hawa wanasiasa hawa mjue Mungu anawaona! Maana nyie Kwa kutupiga sound hamjambo basi endeleeni Tu kutupiga sound halafu muone huko kwa Mungu kama mtafanikiwa.

Hapa Napo Jambo la Amana limeingia pia,mtu amekupa Amana yake umuhifadhie basi fanya hivyo usiingie tamaa ya kuitumia Bila ridhaa au idhini yake.

Na sifa ya sita ni Wale ambao wanazihifadhi swala zao,inamaana ambao wanadumisha swala zao siku zote,maana kuna watu huwa wanaswali ijumaa mpaka ijumaa Tu,au idi mpaka idi Tu,au akiwa na shida basi yeye ndio utamuona anaswali na mambo yake yakiwa fresh Tu basi ndio nitolee na kuswali bye bye.

Hope sauti yangu imetosha na kusikika vizuri kabisa.

Ijumaa Mubaraka!

Ni hayo Tu!
Mkuu naomba kujua katika quraan nitakapoweza kusoma habari za mfalme suleiman.asante
 
Hahaha uko wapi kwanza nikuelekeze darasa mambo ya kujifungulia swahih muslim peke yako utakuja kukutana na nyota nyota tukukose.
Umekumbusha jambo muhimu sana akhy.

Hili nalo ni muhimu sana kulizingatia, na Maulamaa wanasema

من دخل في العلم وحده خرج وحده
Mwenye kuingia kwenye elimu(vitabu) pekeyake basi atatoka pekeyake.

Mambo ya kujifungulia vitabu pasi na muongozo wa wenye elimu, utatokana ufahamu usio sahihi.
 
Back
Top Bottom