Hawa ni watu maarufu duniani ambao viatu vyao vimekosa mvaaji

Ndugu, Bob Marley ni level tofauti sana na hawa,ukivuta kumbukizi na kufatilia hata kama ni binadamu kama hawa lakini yeye alikua na kitu special zaidi, elewa ya kwamba Peter Tosh alikua mwamba wake sana ktk tunzi za muziki lakini Marley alitunukiwa kivingine kuleta ushawishi duniani

Ukimuondoa Yesu na Mohammed ni huyu Bob Marley anayefuata kwa kua na watu wengi zaidi duniani kama wafuasi na wwaliofatilia maisha yake, toka amefariki 1981,kuanzia hapo mpaka leo kaburi lake na makao yake ni eneo linalotembelewa na tu karibu kila siku ama kila wiki toka kipindi hicho mpaka leo hii

Hii inamfanya kua tofauti na hawa kina Alli, maana kidogo kidogo wanaanza kupotea lakini si Bob,fatilia utajua
 
Aliyevaa viatu vya Mohammedi Ali ni IRON MIKE TYSON


Aliyevaa viatu vya Bob Marley ni LEGEND LUCKY DUBE
Kwa umaarufu sawa. Kwa uwezo Tyson yuko overrated sana.

Kumfananisha Bob Marley na Lucky Dube ni sawa na kumfananisha Prince na Trey Songz.
 
Soma vizuri mkuu. Mohammed Ali nimemzungumzia kwa upande wake wa ngumi (boxer)
Bruce Lee nimemuweka kwenye kung fu au karate na..
Bob Marley amesimama kweny mziki wake mkuu.
Huyu alisoma kweli uzi kule juu????jaman jamani
 
Wewe jamaa acha kuongea bila takwimu mwenye ngumi hamna anayemfikia Mike tyson kaangalie talwimu zake na uwaaulize wataalamu katika hiyo fani.inawezekana kabisa Mohammed Ally anapenda lakini hamzidi Tyson katika fani.
Mkuu unaota ndoto za mchana. Tafuta rekodi zao, angalia kila mmoja alipigana na nani ndio uwafananishe.
 
Google sio reliable source,google ni search engine,hata wewe unaweza ukaandika chochote na kupost google.
 
Alejandro Pele wa Brazil naye Ni level nyingine kbsa.Naamini mpaka Dunia inaisha Hakuna mchezaji wa Sola atakaye kuja kufikia viwango vya Pele.

Duru zinasema katika kipindi chake Cha uchezaji jamaa alifunga mabao zaidi ya 1,500
 
Uzi wako umekosa maana kwa kukosa jina la mfalme wa Pop, Michael Jackson hapo ndipo ulichemka. Tena alitakiwa kuwa namba moja hapo. Hawa umewataja kuna watu wameweka rekodi za kuwafunika.

Mfano, Mohamed ali ukimuweka na Tyson, hivi nani katika ujana wake ameweka rekodi kali?!

Bruce lee ni mkali wa karate moves miaka hiyo ila ukitazama kuna mtu kama Don Yen,Jet Lee, ana moves kali balaa brucelee anasubiri.

Bob Marley raggae yake siwezi kusemea maana ni ya tofauti na reggae za sasa sababu yake ilikuwa politically motivated. Wenzake ni kama akina 2pac kwenye hip-hop hakuna wa kumlinganisha nae tokana na mistari yake na style ya delivery. So kwa bob Marley nitakupa pass.

Michael Jordan pia ukitazama League ya NBA kuna madogo wanapiga kikapu hadi unaogopa yeye mwenyewe Jordan ana appreciate uwezo wao na kukiri angekuwapo kwenye court miaka hii angetolewa jasho.

Ila nionyeshe msanii anayeweza match legacy ya Michael Jackson hadi leo hii tokea jamaa amefariki au hata alipokuwa hai! Huyo mtu hayupo.

Ntafutie mtu anayeweza kufunika legacy ya 2pac kwenye hip-hop?

Nitafutie mtu wa kufunika legacy ya Anold Schwarzenegger kwenye cyborg figure?

Nani anamfunika Kenny G katika uimbaji kwa kutumia tarumbeta?!




Sent using Jamii Forums mobile app
 
So unataka kutuaminisha kuwa Mohammed Ali alikuwa anashinda mapambano yake ndani ya dakika 1,2 au 3?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu nakubaliana na ww kwamb Bob Marley ana heshima kubwa sana ukimlinganisha na hao wengine.
Lkn post yang haikuwa ya kumlinganisha na hao ma legendary wengine, bali ilikuwa inazungumzia wasanii na wanamichezo mbali mbali walioacha alama kubwa ktk tasnia zao, ndio nikagawa makundi kwa upande wa mziki na makundi kwa upande wa michezo.
Mfano kwenye michezo nimeweka makundi ma3 na wafalme wao hapo chini πŸ‘‡
1) Boxer au masumbwi- Mohammad Ali.
2) Kung Fu au karate- Bruce Lee.
3)Basket ball- Michael Jordan.

Kwa upande wa mziki nimeweka makundi ma3 na wafalme wao hapo chini πŸ‘‡
1) Reggae- Bob Marley.
2) Pop music- Michael Jackson.
3) Rap& Hip hop- 2Pac Shakur.

Nafikiri hapo utakuwa umeelewa mkuu!
 
So unataka kutuaminisha kuwa Mohammed Ali alikuwa anashinda mapambano yake ndani ya dakika 1,2 au 3?

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu haya mambo nimeshayatolea ufafanuzi kwa baadhi ya post huko juu.
Iwe mpira, masumbwi, mziki nk tayari kuna wale ambao washapewa heshima ya ufalme na wahusika wa hiyo michezo. Haijalishi hawa vijana wa sasa au baadae wanaweza kufikia au kuzidisha rekord za hawa ma legends au not. Soma post namb 34 na 36 mkuu naambatanisha na picha hapo chini.

Kama chama cha ndondi duniani kimeamua kuwa Mohammad Ali ndio mfalme wa masumbwi wa miaka yote, mimi na ww ni kina nani mpaka tupingane na wajuzi hao.
Si waliwaona kina Lewis, Tyson na wengine wengi waliokuwepo kabla na baada ya Mohammad Ali?
 

Attachments

  • Screenshot_20220826-172228.jpg
    40.1 KB · Views: 18
  • Screenshot_20220826-160611.jpg
    36.6 KB · Views: 16
  • Screenshot_20220826-193449.jpg
    49.7 KB · Views: 15
Hii list yako pia ni swadakta kabisa mkuu.
 
Ukimwacha magufuli sijakuelewa
Mkuu hawa niliowaandika hapo juu ni wasanii na wanamichezo tu.
Kwahiyo hata ukimuongeza sio mbaya, lkn nahisi Magufuli yeye alivaa viatu vya baba yetu wa taifa mw Nyerere.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…