Hawa ni watu waliomdhihaki Mungu na kupatwa na shida

Ndiyoooooooh.
 
Hebu nichunguzie hata mwanafalsafa mmoja akiitwa kwa jina la Stephen Hawkins,niliwahi kusikia naye aliwahi kukana kuwa hakuna Mungu...
Si kna mtu kamleta huyo Stephen had picha yake akiwa mgonjwa, bado watu wamempa za uso had kakimbia ni uongo uongo tyuuh.[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Genesis 6:6 Mwenyezi-Mungu alisikitika sana kwa kumuumba binadamu duniani. Mwenyezi-Mungu alihuzunika sana moyoni mwake

Hivi mimi na huyo Mungu wako nani fala?
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Naona unatengeneza hoja ionekane mtu mwenye afya bora ya akili ni yule ambaye atajibu hayo maswali kulingana na majibu yako ya mfukoni yalivyo

tulia hii haitaji mawenge ya akili majibu yapo na wala si yangu ya mfukoni ila wale mumaizi tu ndio waelewawo.
 
tulia hii haitaji mawenge ya akili majibu yapo na wala si yangu ya mfukoni ila wale mumaizi tu ndio waelewawo.
Majibu yapo mfukoni mwako na hayo majibu ni fallacy, huna hakika nayo unasukumwa tu na hisia

Najua kwasababu wengi wenu mnao amini Mungu ni kutokana na kukosa majibu ya hayo maswali na hapo ndipo mlipoanza kuja na wishfully thinking
 
Mungu yupi unayemwongelea wewe? Kwa sababu wewe hutambui uwepo wa Mungu kwa hiyo in simplicity wewe kiranga ulijiumba mwenyewe
Kwani kama mimi sijajizaa mwenyewe hilo linamaanisha ni lazima baba yangu ni George W. Bush?

Unatoka vipi kusema mtu hajajiumba mwenyewe mpaka kusema mtu lazima kaumbwa na Mungu?

Huoni kwamba hapa kati kuna steps kibao za kuthibitisha umeziruka?

Unaweza kuthibitisha Mungu yupo?

Kusema mtu kaumbwa na Mungu kwa sababu hajajiumba mwenyewe ni "logical non sequitur".

Logical non sequitur ni kosa la kimantiki la kuunganisha vitu viwili ambavyo havina uhusiano wa moja kwa moja.

Hata kama mtu hajajiumba mwenyewe, hilo halina maana ni lazima kaumbwa na Mungu.

Ukisema mtu ni lazima kaumbwa na Mungu kwa sababu hajajiumba mwenyewe, unafanya kosa la kimantiki la non sequitur.

Kwa sababu inawezekana mtu hajajiumba mwenyewe na hajaumbwa na Mungu pia.

Sasa, thibitisha mtu kaumbwa na Mungu na hajatokea kwa njia nyingine yoyote.
 
Nashindwa kuelewa Kwanini linapokuja swala la kuthibitisha uwepo wa Mungu inakuwa ni vigumu sana na mwisho wa siku watu kukimbilia kusema mtalaanika na mambo kama hayo

Miongoni kwa majibu mepesi kabisa ya kuthibitisha kuwa Mungu yupo ni kama haya, mtu atakuuliza we umetokea wapi? Nani kaumba dunia au dunia imetokea wapi? Na utaskia Kila kitu kina mwanzo wake

Sasa linapokuja swala la mie nimetokea wapi, au dunia imetokea wapi hivi ndo kweli uthibitisho wa uwepo wa Mungu? Inajulikana kuwa maandiko yanasema Mungu hakuumbwa Wala hajazaliwa, ila hapo hapo tumetoka kuambiwa Kila kitu kina mwanzo wake kwahiyo mwanzo wa Mungu ni upi?

Kama unaambiwa kuwa Mungu hakuumbwa na wala hakuzaliwa kwahiyo maana yake alitokea tu from no where na unaamini Kwanini ila kwa nini ukiambiwa kuwa dunia pia imetokea tu na yenyewe from no where hutaki? Kwanini namie nikisema nimetokea tu from no where hutaki kuamini ilihali unaamini Mungu ametokea tu from no where?

Huwezi kuthibitisha ulikotokea wewe pamoja na dunia uliyopo ila unataka kutetea na kupambaba kuthibitisha uwepo wa aliekuumba wewe na dunia uliyopo kwa kigezo cha Imani, hapo ndio shida inapokuja, acheni tuendelee tu kuishi na kuabudu tu hakuna namna labda kuna siku majibu ya kuridhisha yatakuja
 
Kwa hiyo mababu zetu Africa waliokuwa wakiabudu mizimu hawakuwa na afya nzuri ya akili? maana kabla ya kuenezwa kwa dini, lazima kuna wale ambao ndiyo the smartest walioanzisha utaratibu wa kuabudu mizimu.
Kama jibu lako ni sahihi, kwa nini dhana ya kifo imekinzana kwa imani tofauti kwa ulimwengu mzima?
Kama mkoloni asingekuja Africa akakuletea dini, halafu tukakutana mimi na wewe na tukafanya mazungumzo haya, ungenipa jibu hilohilo?
 
Mambo ya dini kuchelewa kuwafikia babu zetu hizo ni logistics tu lakini haimaanishi kuwa dini haikuwepo.Mpaka muda huu tunazungumza kuna maeneo dini bado haijafika pia.

Pengine swali lako lingeuliza Status ya waliotangulia kabla ya Ujio wa Dini lingekuwa swali sahihi zaidi ambalo jibu lake pia lipo.
 

Ndipo niliposema unatakiwa uwe na afya bora ya akili [emoji15][emoji15]
masuala ya kuabudu mizimu sijui mkoloni kuja na dini yanahusiana na lolote katika maswali hayo 4?
Halafu mbona unajichanganya sana hueleweki unacho sema. wale wanao abudu mizimu halafu kabala ya kuenezwa kwa dini kwani hao walio abudu mizimu ilikua sio dini yao na utaratibu wa kuamini kwao? kama ilikua ndio dini yao na kuabudu kwao hii smartest imetoka wapi? inabidi utulize kidogo akili ktk masuala haya.
dhana ya kifiko kukinzana kwa imani tofauti sawa narejea papohapo kwenye afya bora ya akili katika tafsiri ya hicho kifo.kwa tafsiri yako au kama ya mleta mada hii. ni tafsiri potofu na yenye maswali mengi baadae.
 
Brother [emoji41] upo Sawa?
 
Yaani Mungu kawaacha waliobariki Ndoa za jinsia moja kwa hilo kanisa akaja kumuua aliyeudhihaki Msalaba!? Tena unaouita Mtakatifu!!!! Unahitaji Akili zimekwisha kabisa!!!
 
Wakubwa Muaminio katika Dini, hebu niwaombe jambo moja tu la msinfi sana. Tujadiliane kwa hoja na si Matusi wala Vitisho. Hoja tunazozihoji mzijibu na sio kumshambulia mtu binafsi!


Hotep
 
Hili linanistaajabisha mno! Kuna watu wanakwambia Mungu aliumba kiumbe(mwanadamu) kikiwa na Utashi, Uyakinifu, Umakini na Ustaarabu lakini hao hao waamini ukiwauliza kwa Uyakinifu na Utashi juu ya Mungu wanakujibu Mungu hajadiliwi hivyo. Hiyo Rational Logic ya Mungu ndiyo tunayoitaka hapa! Kuuliza na kuishi katika kufahamu sio dhambi waungwana!
 
Nipo nasubiri wapenda story za mavampure , majini ,mungu, shetani ,vibwengo,wachawi na vinyamkera niwafumbue macho kuwa hizo ni story za kutunga[emoji1787][emoji1787][emoji1787]

Sent from my JSN-L21 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…