TAFSIRI YANGU ISIYO RASMI YA SIMULIZI HII KWA AJILI YA KUJIFUNZA
Kila dini inafundisha waamini wake kushika na kutii sheria zake..
Mungu anatuzuia kabisa binadamu kutilia shaka nguvu na mamlaka yake. Haijalishi mtu ni maarufu kiasi gani, tajiri kiasi gani au amefanikiwa kiasi gani, haya yote hayampi mtu yeyote kibali cha hata kudhania tu kuwa yuko au anaweza kuwa juu ya Mungu..
Katika Biblia, Mungu alimwadhibu mfalme Nebukadneza aliyejiinua na kujiona kuwa yeye ni Mungu kiasi cha kuamuru watu aliokuwa anaowaongoza wamwabudu yeye..
Ifuatayo ni orodha ya matukio maarufu ya watu duniani waliojaribu kufanya dhihaka dhidi ya Mungu kwa nia ya kushusha hadhi, nguvu na mamlaka yake, kilichowatokea ni historia ya kutufundisha sisi..
Hata hivyo, ikumbukwe kubwa, sisi wanadamu tunaweza kuja na nadharia tu, lakini ni Mungu yeye pekee yake ndiye ajuaye sababu halisi za kifo cha mtu...
1. TANCREDO NEVES.
Huyu alikuwa ni Rais wa Brazil.
Ilikuwa ni wakati wa kampeni za uchaguzi wa Urais na alidhihaki kwa kusema kuwa, iwapo angepata kura 500,000 toka chama chake na kushinda Urais, basi hata Mungu mwenyewe hataweza kumtoa katika Urais wake..!
Hakika alipata kura zote alizotaka na kushinda Urais. Bahati mbaya, aliugua vibaya na baadaye kufariki siku chache kabla ya kuapishwa...!
2. JOHN LENNON.
Huyu alikuwa mwanamziki wa kundi la muziki maarufu la Beatles miaka ya 1960s na 1970s
Lennon na wenzake katika kundi lao kina Paul McCartney, George Harrison na Ringo Star ⭐⭐ waliandika mamia ya nyimbo zilizopendwa na kuwapa umaarufu sana miaka hiyo..
Ikatokea siku moja na wakati fulani mwaka 1966 Lennon akihojiwa na jarida maarufu la Marekani alisema maneno haya;
"...
ukristo utafika mwisho na utatoweka. Siwezi kujadili kuhusu hili hata kidogo kwa sababu nina uhakika na ninchosema..
Aliendelea kusema;
"
...Yesu Kristo alikuwa mkamilifu. Lakini wafuasi wake walikuwa ni watu wa kawaida na rahisi tu. Leo hii, sisi BEATLES ni maarufu zaidi kuliko yeye (yaani Yesu Kristo)..."
Desemba 8, 1968 John Lennon alimiminiwa mvua ya risasi 6 kichwani na mpenzi wa mziki wake mbele ya nyumba yake na kufa hapohapo..!
3. CASUZA..
Huyu alikuwa Mbrazil mwenye jinsia mbili (bisexual), mwandishi wa nyimbo, mwimbaji na mshairi maarufu na mbobezi..
Ilitokea wakati mmoja wakati wa shoo yake huko Caneiro [Rio de Janeiro] akiwa stejini akivuta sigara yake, alibunda pafu ya moshi wa sigara hiyo na kuuachia juu angani huku akitamka maneno haya;
"...Mungu, hiyo ni kwa ajili yako...!"
Casuza alikufa katika umri wa miaka 32 tu kwa ugonjwa wa kansa ya mapafu ktk namna ya kutisha sana..
4. THOMAS ANDREWS..
Huyu ndiye mjenzi wa meli maarufu ya TITANIC iliyozama miaka kadha iliyopita nyuma...
Mara baada ya kumaliza kazi ya ujenzi wa meli hiyo, akihojiwa na ripota mmoja wa habari aliyemuuliza ni kwa kiwango gani anaamini meli ya TITANIC itakuwa salama..?
Katika namna ya dhihaka, alijibu swali hili la mwandishi kwa maneno haya;
"...Hata Mungu mwenyewe hawezi kuizamisha meli hiyo...!"
Hatima ya meli ya TITANIC wowote tunaijua...
5. MARYLYN MONROE
Huyu ni mwanamama tajiri na mwenye umaarufu mkuu ndani ya Hollywood nyakati hizo..
Mama huyu [celebrity] alikuwa na maisha kamilifu yanye utoshelevu kimwili ambayo kila mtu huota na kutamani kuyaishi..
Siku moja katika moja ya shoo zake, alitembelewa na mhubiri maarufu wa Injili, Billy Graham..
Billy Graham akamwambia Monroe kuwa, Roho wa Mungu amemtuma aje kwake ili amwambie habari njema za wokovu wa Yesu Kristo..
Hiki ndicho alichojibu Marylyn Monroe;
"...Simhitaji Yesu wako....!"
Wiki moja badaye alikutwa amekufa katika nyumba yake..
6. TUKIO LA CAMPINAS - BRAZIL MWAKA 2005
Kundi la marafiki huko Campinas, Brazil walikuwa wanakunywa na kulewa huku wakiendesha gari...
Wakaendesha gari lao hadi nyumbani kwa rafiki yao wa kike ili kumpitia waende walikokuwa wanataka kwenda...
Huyu rafiki (binti) alitoka ndani akisindikizwa na mama yake na kuelekea kwenye gari la rafiki zake...
Mama yake binti, aliingiwa na mashaka na wasiwasi baada ya kuwaona rafiki za binti yake wakiwa ktk hali ya kulewa chakari..
Akamshika mkono binti yake mkono ambaye tayari alishakaa kwenye kiti cha gari na kumwambia;
"...Binti yangu, tembea na Mungu na akulinde uwe salama..."
Sikiliza alichojibu binti;
"...Iwapo tu Mungu huyo atasafiri ndani ya sanduku, kwa sababu kama unavyoona ndani ya gari yetu, tumeshajaa...!"
Kama saa moja hivi baadaye, taarifa zikaenea kuwa, gari yao imepata ajali mbaya sana kiasi cha hata mtu asiweze kuitambua ni gari aina gani hilo kwa jinsi ambavyo lilivyokuwa limeharibika nyang'a nyang'a..
Wote waliokuwamo ndani ya gari ile walikufa palepale...!
Cha ajabu, ndani ya gari hilo nyuma kwenye buti, kulikuwa na sanduku (trunk) na ndani ya sanduku hilo kulikuwa na tray ya mayai ikiwa nzima bila hata na yai moja kuvunjika licha ya gari ile kuharibika nyang'a nyang'a..!
Polisi walishangaa sana kiasi cha kukiri kuwa, jambo hilo kwa hivihivi tu haliwezekani unless kuwe na nguvu fulani ya ziada iliyofanya mayai hayo yasivunjike..!
7. CHRISTINE HEWITT
Huyu alikuwa ni mwandishi wa habari, mburudishaji [entertainer] Mjamaika ambaye aliwahi kutamka maneno haya kuhusu Biblia - Kitabu cha Neno la Uzima kinachotumiwa na wakristo;
"...Biblia ndicho kitabu cha hovyo kabisa kilichiwahi kuandikwa...!"
Muda mchache baada ya marashi haya, Christine Hewitt aliokotwa akiwa amekufa kwa kuungua vibaya kiasi cha kutotambulikana kabisa akiwa ndani ya gari yake..!
NB: Binadamu hutumia nadharia zaidi juu ya kifo au matukio mabaya yawapatayo wanadamu. Lakini katika yote iwe kifo au tukio lolote lisilo pendeza, Mungu anabaki kuwa ndiye ajuaye sababu halisi ya kila jambo..
Asomaye na ajifunze..