Hawa Wabrazil wa Singida Big Starz si wa kitoto

Hawa Wabrazil wa Singida Big Starz si wa kitoto

Moja ya ushamba wetu ni kutojua nini Mchezaji anatakiwa kufanya uwnajani, tukidhani chenga na danadana ndio uwezo

Mchezaji kama Fraga Vieira alikuwa imara sana kama defensive/holding midfielder , wasiojua mpira wakawa wanasema Mbrazil gani hapigi chenga 😆😆😆, hawajui sio kila Mchezaji ana lazimika kupiga piga chenga. Ndio maana wapo Wabrazil kama Fernandinho au Casemiro wangekuwa Tanzania wangetukanwa maana hawana mbwembwe
 
Cha kushangaza Deus Kaseke aliyeoneka kuchokwa Yanga, kwa sasa anakinukisha vizuri tu na kwa dakika zote 90 za mchezo!

Amis Tambwe naye anamuweka benchi Meddie Kagere! Na ndiye aliyetoa assit ya goli kwa mechi ya pili mfululizo!

Hii timu ya Singida Big Stars inashangaza wengi kwa kweli.
 
Wachezaji wa kawaida sana

Hizo Tepsi Evance wa Azam anafanya mara 10 ya hao
Wabongo kwa shobo utawaweza kuna feisal pale yanga kama hawamuoni wao kila siku mayele striker anavizia kama anacheza chandimu vile.
 
Mwangalieni a raw and pure talent, achaneni na magalasa yaliyojichokea

Dogo ana kipaji kikubwa lakini nashangaa huwa hachezi mara kwa mara....msimu uliopita alikuwa anaingia dk za mwisho game kuisha na unaona kabisa anabadilisha mchezo....akili za kiafrika ni shida sana,Ulaya vijana wenye talent hupewa nafasi mara kwa mara lakini sio huku...hata ile mechi na zesco juzi dogo alikiwasha sana..msomali amtumie sasa msimu huu.
 
Moja ya ushamba wetu ni kutojua nini Mchezaji anatakiwa kufanya uwnajani, tukidhani chenga na danadana ndio uwezo

Mchezaji kama Fraga Vieira alikuwa imara sana kama defensive/holding midfielder , wasiojua mpira wakawa wanasema Mbrazil gani hapigi chenga 😆😆😆, hawajui sio kila Mchezaji ana lazimika kupiga piga chenga. Ndio maana wapo Wabrazil kama Fernandinho au Casemiro wangekuwa Tanzania wangetukanwa maana hawana mbwembwe
Kumbe we umeona chenga tu,hujaona kasi ya kupeleka mashambulizi,hujaona penetration pass za uhakika,hujaona uwezo wa kuhamisha mpira upande mwingine wa uwanja(ambacho wa bongo wengi awawezi,mara kibao mpira huchezwa upande mmoja),hujaona eye contact na wenzake mtu akiwa uwanjani..ILA UMEONA CHENGA TU ..Hivi unafikiri kip humbeba mo Salah?
 
Sasa mbona hao wehu wenu ni wa kawaida sana...tena saaana,,,hayo mambo dogo tipsie wa azam huwa ndo mambo yake mara mia nane tena!!!WA TZ TUACHE USHAMBA ..
 
Back
Top Bottom