Asalaam aleykum wana Jf.
Leo Mkuu wa Majeshi, General Mkunda amegusia kuwa kuna baadhi ya wakimbizi wameshikilia nafasi nyeti serikalini kulingana na taarifa za kiintelijensia.
Sasa lengo la uzi huu ni kuwarahisishia vyombo vyetu vya ulinzi na usalama ili kuwabaini wakimbizi wote ambao wameteuliwa kwenye nafasi za maamuzi.
Hii itasaidia kudumisha ulinzi na usalama wa Taifa letu kwani ni hatari sana kukabidhi nafasi nyeti kwa wageni/wakimbizi kwa sababu kuna wale ambao hata kama wameishi miaka 1000 sehemu nyingine, huendelea kuwa wazalendo kwa Taifa lao la asili. Mfano hai ni Mh. PK, Rais wa nchi mojawapo jirani, ambaye ni kama tu alizaliwa na kukulia Uganda, lakini bado kilichotokea wote tunakifahamu.
Kwa wasiofahamu tu ni kwamba huyu Mh. PK alishikilia nafasi nyeti sana katika nchi ya Uganda ikiwemo Mkuu wa kitengo cha Intelijensia Jeshini, lakini bado tu roho yake na akili yake ilikuwa katika nchi yake ya asili!
Chonde chonde kwa vyombo vyetu vya ulinzi na usalama, siyo kwamba hawa watu hawajulikani, wanafahamika vyema ila kwa sababu ya rushwa na mambo mengine, basi kunakuwa na ile hali ya kufumbia macho.
Naomba kuwasilisha.
View attachment 2879699